• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Monday, March 21, 2022

SABABU YA KUPENDA KALE.

9:19 AM // by Kalma // No comments

KALE, 
Imeonekana kale imekua mtoto anaefahamika sana siku hizi.Miaka ya nyuma kidogo sikuwahi kusikia kale hili,na sasa ni mboga ninayoikimbilia mwanzo nikiingia sokoni.
Chakula tofauti huweza kuwa mtindo kwa kipindi fulani hivi,lakini binafsi sidhani kama kale ni kimoja wapo.Mboga hii ipo kwa muda sanaa.
Kama hujawahi nunua mboga hii ya kijani maishani mwako , nakusisitizia kubwa fanya haraka ununue ukijani huu.Lakini iwe baada ya kujua sababu tano hizi!

Ni chakula cha kuondoa sumu.

Kale ina  fiber na sulfur — zote ni kazi kuu katika ini lako,husaidia kutoa sumu mwilini. 

Vitamin A, vitamin A, vitamin A.

Kale ina zaidi ya 100% ya vitamin A inayotakiwa kila siku — 133% ndio haswaa,ambayo ni zaidi ya mboga nyingi za kijani zilizopo.
Vitamin A hufanya maajabu katika mfumo wa kinga mwilini,mpango mzima wa kuona,na husaidia kupambana na cancer kwa kudhibiti uzalishwaji katika seli zinazoweza sababisha cancer.

 Ni anti-inflammatory.

Vyakula vingi tunavokula,kama cereals,nafaka,vyakula vya kutengeneza,na vingi— vinosababisha inflammation katika mwili. Chronic inflammation huweza sababisha maradhi kama uchovu,kisukari,ugonjwa wa moyo,na cancer, kwahiyo ni muhimu kuepuka vyakula ambavo huweza kuleta madhara hayo.
kale kama anti-inflamatory properties ina  omega-3 fatty acids,ambayo inaaminika kuwa na nafsi kubwa katika kupunguza matatizo hayo.

 Ni rahisi kukua.

Sijawahi jaribisha kuupanda mwenyewe.lakini chanzo changu kinanilazimisha nifanye hivyo.Japo kale huota vizuri sahemu za baridi,pia huweza kukua vizuri hata kwa hali yoyote ya hali ya hewa.kama huna garden nje kwako waeza panda pia kwenye pot,La msingi iwe na 6 inches, ya nafasi katika pot kuruhusu kukua. Kale ni pretty skilled katika kupambana na wadudu(disease)- ni ndoto ya mwanzo ya kuwa na garden!.
 Kale chips ni tamu.

Kama hujawahi jaribu kale chips,tafadhali fanya nyumbani kwako kwa mara ya kwanza.
Ni ya ajabu na rahisi kutengeneza,na tafuta soko zuri utayoipata ikiwa fresh huwa yenye ladha nzuri na tamu,inaweza shinda ya kutengeneza mwenyewe nyumbani,ila kwa kwetu huku sina uhakika kama yapatikana iliotengenezwa.

Chips za kale :

Jinsi ya kuandaa:

 Preheat oven kwa 350 degrees F.katakata vipande vya kale ilo lowekwa vya size tu sio vikubwa sio vidogo,changanya na olive oil,tia chumvi na ya vitunguu thom.weka kwenye sahani ya oven yako kisha oka kwa 15 dakika(mpaka ziwe crispy) na inakua kama pie,nzuri ,tamu ladha yake,na virutubisho kibao.

Hizo ni tano katika nyingi zao katika lishe na afya yako tokea mmea kale.Tupia nyingine tujenge afya zetu na familia kwa ujumla!!



Enjoy and Share !