• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, November 6, 2014

4:52 AM // by Kalma // No comments

Kuimarisha afya kwa wazee(watu mzima). 
Kula vyakula tofauti kutokea makundi yote ya chakula yatasaidia kukupatia lishe na afya katika mwili wako inayotakiwa kwa umri.Ulaji wa afya huwa ni kwa mipango ya matunda,mboga mboga,nafaka nzima na au low-fat au fat-free dairy; ikiwemo nyama,poultry,samaki,maharage,mayai na jamii ya karanga; na vyakula vilokuwa havina mafuta mengi,trans fats,cholesterol,chumvi (sodium) na sukari ya kuongezewa yaani ya kukorogea juu.
Kula vizuri haitakiwi iwe complicated.Anza na huu ushauri kutokea kwa wataalam (Dietary Guidelines for Americans):
Kula matunda na mboga mboga.zinaweza kuwa fresh, ziloganda au kwenye makopo.Kula zaidi mboga zilokooza rangi ya kijani kwa mfano leafy greens au broccoli, na mboga za rangi ya machungwa kama karoti na viazi vitamu.


Tofautisha protini yako kwa chaguo tofauti tofauti zaidi samaki,maharage na njegere.

Kula angalau tatu ounces ya nafaka nzima (whole-grain cereals), mikate, crackers, wali  au pasta kila siku.


  • Pata aina tata au hizi za mafuta kidogo ( low-fat) au maziwa yasomafuta( fat-free dairy )(maziwa, maziwa ya mtindi au cheese) ambayo fortified na vitamini D kusaidia kuweka na kuipa nguvu mifupa yako na afya tele.
  • Tengeneza mafuta tokea kwa vyakula vya afya unavyokula (polyunsaturated and monounsaturated fats). Pendelea tokea solid fats kuwa mafuta pindi unapoandaa msosi.
  • Ongezea mazoezi au kazi za mwili.
Wastanisha kazi za mwili yaani physical activity na mlo wenye afya iwe ndo vikorombwezo vyako kwa kutengeneza afya nzuri na kuwa fit.Weka  malengo kufanya kazi au mazoezi angalau kwa dakika 30 kila siku.Unaweza kupumzika kwa hilo zoezi lako au hiyo kazi kwa dakika 10 mara kwa mara kwa  kila siku
Kama hauko active, anza na kwa mazoezi au kazi kwa dakika chache,kama vile kutembea, na iwe unazidisha muda kadiri hali inapokuwa nzuri au fit.
Pata ushauri kwa muuguzi wako wa afya kabla ya kuanza mazoezi mapya au kazi mpya ambayo hukuizoea kuifanya siku zote. 


Wednesday, November 5, 2014

Olive Oil kuondoa Stretch Marks

6:41 AM // by Kalma // No comments

Stretch marks ni kitu ambacho hakipendezi kuwa nacho katika ngozi yako.Kwa bahati mbaya,tunaweza epukana na hali hii mbaya ya marks kwa muda,na sana pale unapo nenepa au unapopungua uzito.Kipindi cha ujauzito,wanawake wengi wanapata hizo marks hata bila ya kutumia aina za cream tofauti tofauti.La zaidi,hizi marks zinakera na haziondoki haraka.Kama unatafuta ufumbuzi kwa hilo la kuondoa hizo stretch marks,Olive Oil huenda ikawa chaguo zuri kwako.
Angalizo:
Olive oil hufanya kazi nzuri kuondoa stretch marks.Kuondoa hii mistari kwenye ngozi sio kwa usiku mmoja tu,kwa uhakika utaona utofauti  ndani ya wiki au wiki mbili
Kupakaa Olive oil mara kwa mara huifanya ngozi kuwa  nyeupe kama sio kuondoa kabisa, hilo ndo linaloifanya Olive kuwa best solution kwa wajawazito wenye stretch marks .
Kumbuka Stretch Marks:
Kabla hatujalizungumzia hili la ufanyaji kazi wa Olive oil ,ni lazima tujue kwanini stretch marks zinatokea kwenye ngozi.
  • Ni geni lakini kweli,wanawake ndo wanatokewa na hizi alama zaidi kuliko wanaume.Wasichana kipindi cha umri wa kukua kama kuvunja ungo,na kipindi cha ujauzito .
  • Haya makovu yako kwa wanawake sababu ngozi zao ni laini na flexible.Japokuwa,wanaume pia wanapata stretch mark kwa kuongezeka uzito au kupungua uzito kwa muda wa kipindi kifupi.
  • Stretch mark in dermatology ni Striae.Hii mistari hutokea zaidi pindi ngozi ya juu ya ngozi hutanuka kuzidi uwezo wake.
  • Specific sehemu za mwili ambayo huwa ni shahidi wa hizi mistari ni juu ya mikono na chini ya mikono,tumboni, thigh,kwenye makalio,na sehemu ya maziwa.
  • Inaaminika zaidi na wataalamu kwamba stretch marks hutokea sana maeneo ya ngozi ambapo mzunguko wa Vitamin ni mdogo au hafifu.
  • Stretching au shrinking ya ngozi tokea katika vipindi vya maisha,kwa zaidi kipindi cha kuvunja ungo na ujauzito,na kipindi cha kujifungua.
Kwa nini Olive Oil kwa stretch Marks?
Unaweza ukajiuliza kwanini  kuchagua olive oil kuondoa stretch marks.Well,mafuta haya ya asili ni tajiri na chanzo kikubwa cha Vitamin E,ambayo ni muhimu kwa afya ya ngozi.
  • Olive oil,na kuwa na wingi wa Vitamin E ni nzuri kupakaa katika sehemu ambazo kuna mistari .Utapata matokeo mazuri kama utaanza kupakaa pindi stage za mwanzoni.
  • Sio tu Vitamin E,Olive oil ni chanzo kizuri cha antioxidants.Husambaza Oxygen katika makovu hufanya ngozi kuwa laini na supple.Kwa muda mfupi, hizo alama zitaanza kupotea kiasili.
Ukweli wa athari za Olive oil kwa Stretch marks
Stretch marks nyingi hutokea zaidi juu ya ngozi.Hata hivyo Olive oil hupakaliwa juu ya ngozi.Ni muhimu kujua kwamba haiwezi kufifisha mistari kwa ndani ,huondoa mistari kwa nje ya ngozi.
Matumizi ya mara kwa mara ya Olive oil huondoa mistari kwenye ngozi na haionekani vibaya.
Ngozi ya binadamu iko flexible,lakini haina uwezo wa kutanuka kuzidi uwezo wake.Ngozi hukua kwa haraka kipindi cha ujauzito ambapo ngozi haiwezi tena kuhimili kubanwa.
Olive oil hufanya kazi lubricant ambayo husaidia kutanuka kwa ngozi bila ya kupasuka.Kutumia Olive oil hufanya ngozi kuwa laini na huwa haina maumivu kwa kutanuka kwake.  Jinsi ya kujisugua au massage na Olive oil kwenye stretch marks.
Olive oil kwa stretch marks kipindi cha ujauzito ni solution nzuri ambayo utakua umeipata.Tumia maji ya uvuguvugu na olive oil kwa kujisugulia maeneo husika.Hii itasaidia kwa haraka kusambaza mzunguko wa damu katika  hizo sehemu kwa upana zaidi.Acha olive oil kwenye ngozi kwa muda wa saa nzima ili ngozi ifyonze Vitamins kwenye mafuta vizuri.Fanya hivi kila mara kwa muda wa wiki .

SHARE!

Tuesday, November 4, 2014

FAIDA ZA HILIKI

1:09 AM // by Kalma // No comments

HILIKI
Hiliki ni asili ya ukijani katika misitu huko India.Kiungo hiki hutumika sana katika misosi India,pia hutengenezwa kama dawa katika Ayurvedic kama tiba ya ulcers ya mdomo,tatizo la uyeyushwaji chakula,na uchovu.Baadhi ya faida za kiafya za hiliki ni kali lakini tamu,uchachu pia, kwa sasa inachunguzwa kisomi zaidi.Ni vizuri kutumia hiliki katika vyakula vyetu sio kwa sababu ya ladha peke yake ,lakini faida za kiafya ndo kubwa la kuliangalia hapa.
Hiliki ,kiungo kikuu kitumikacho zaidi India sio kuongezea ladha bali ni tiba kuu pia.
Hizi ni faida chache za kiafya za hiliki:


  1. Huongeza au husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.Ni kisababishi kikuu,husaidia kupunguza acid na bloating.Kunywa chai ya hiliki huondoa maumivu ya kichwa ambayo yamesababishwa na tatizo la uyeyeushwaji wa chakula.
  2. Huongeza,huleta hamu ya kula na hurahisisha au kutibu mchefuko wa tumbo.
  3. Kutafuna hiliki huondoa harufu mbaya ya mdomo.
  4. Huongeza na kurahisisha mzunguko wa damu kwenye mapafu na husaidia kulinda na spasms or convulsions. Imeshauriwa kwa kiasi kidogo kula hiliki kwa mtu anaesumbuliwa na pumu na kifua kama kifungua hewa katika mirija ya hewa .
  5. Kujikanada au kujichua kwa kutumia mafuta ya hiliki hutibu shida ya viungo na hutuliza maumivu pia. 

Tuesday, March 18, 2014

VITU 4, NJIA 3

6:58 AM // by Kalma // No comments

VITU 4, NJIA 3
 Utakuwa ni mdau mkuu mmoja wapo wa hii blog,kwa vyovyote umejifunza mengi kuhusiana na matumizi na faida ya vyakula tofauti tofauti japo kwa uchache wake.Kipindi hiki badala ya kulist au kushare kimatumizi au faida ya aina moja ya chakula,nilifikiri iwe tofauti kwa topic hii kidogo:  Vitu 4, njia tatu.

 Oats: 
kwa Maana ya kuila tu,oats  ina fiber nyingi ya kutosha,protein,na antioxidants.Iko vizuri katika masuala ya afya ya moyo.Kwa mwili,oats ni ya ajabu sana inaleta moisture kwenye ngozi na nwele,na nzuri kwa kinga pia.
Maziwa yenye lozi(Almond milk): 
Maziwa ya lozi ni hayana dairy,yana antioxidants nyingi,ni mazuri kwa afya ya moyo.Yana vitamin na madini kama copper,zinc,magnesium,madini ya chuma,na calcium-na sio tu mazuri kwa ndani hata  kwa kuyatumia nje mazuri,sana tu!

 Apples: 
Hili tunda pia lina antioxidant ya kutosha!Apples inasaidia kuboost immune system,inaboost kumbukumbu sana,na huweza kupambana na cancer,hutosheleza hamu ya kula.Apples ina vitamins A,B,na C,ambayo huipa ngozi yako muonekano mzuri fresh na wa kuvutia.
Asali
Asali ni yenye utamu wa asili pamoja nayo ni anti-bacterial na antifungal pia.Husaidia kwa kutuliza maumivu ya kifua na tumbo ,pia ni kilinzi cha vijidudu vya moyo na cancer.Asali ni nzuri kwa nywele na ngozi ikitumiwa kwa nje,huleta joto na hujenga afya nzuri.
Na sasa… hizi njia  3 za kutumia kwa 4 vitamu !
1. Tumia vikiwa vya moto
Vinne hivyo ukitumia kwa kifungua kinywa huwa ni vitamu sana.Chemsha oats na maziwa yenye lozi,kisha tia lozi zilokatwa katwa,nyunyizia asali juu,chora mchoro wowote kutumia asali juu ya hayo maziwa.Ni ladha tamu,rahisi,afya na ya moto.Enjoy it! 
2. Tumia vya baridi
Hiki ni kipya ila ni kitamu jaribu utaipenda nakuhakikishia,hautajutia hayo maamuzi yako!Weka hivyo vyakula vinne vya ukweli,yaani oats,apple,asali na maziwa ya lozi, katika blender na barafu kama utapata,zisage mpaka ziwe laini.Nyunyizia au mwagia mdalasini unaweza kuwa unga au ulotwangwa vipande vidogo dogo kama unapenda,kisha furahia ! This is such a treat to the taste buds. Utapata wakati mgumu kuamini kwamba ni mlo wenye afya tele. 


3. Pakaa usoni.
Kama zilivyotajwa hapo juu,hivyo vinne ni vya ajabu sana na vina faida lukuki sana tuu pindi utapotumia kwa nje,na hufanya kazi vizuri.Changanya vyote kwenye blender(bila ya barafu,isiwe ya moto),tumia kupakaa usoni,kwa dakika 10 halafu osha uso.Utona uso wako uko mlaini,msafi,na ngozi nyororo.
Unaweza tumia nafaka nzima pia kutengeneza kwa ajili ya kusafishia uso.Itumie kama singo mwilini.Kwa wale mnaotarajia kufunga ndoa  singo ndo hiyoooo! Kazi kwako.



Friday, February 21, 2014

FAIDA 7 YA CHAI YA KIJANI.

2:28 AM // by Kalma // 1 comment

CHAI YA KIJANI
Kikombe cha chai ya kijani ni kizuri kwa kuianza siku yako.
"Ni kitu chenye afya naweza fikiria kukinywa," by Christopher Ochner, PhD. He is a research scientist in nutrition at the Icahn School of Medicine at Mount Sinai. "Green tea is beyond a super food."
Kwa miaka 20 ilopita sasa,maelfu ya wasomi walionyesha faida za chai ya kijani.

Seli zenye afya
Kwanini chai ya kijani nzuri kwako?Ni kwasababu ya catechin iliyokuwamo," amesema Beth Reardon, RD, a Boston nutritionist. Catechins ni antioxidants ambayo hupambana na vile vile huzuia uharibifu wa seli.Chai ya kijani huwa sio ya kutengenezwa kabla haijawekwa katika kikombe chako,kwa hiyo ni tajiri wa catechins.
Afya ya moyo
Chai ya kijani imeonyesha kuongeza msukumo wa damu na kushusha cholesterol. Mnamo  2013 studies nyingi zilionyesha chai ya kijani au green tea husaidia kulinda na issues nyingi zihusianazo moyo,kutokea high blood pressure hadi congestive heart failure.

Afya ya akili
Kizuri kwa moyo huwa ni kizuri kwa akili pia,na akili yako huitaji mishipa ya damu yenye afya nzuri pia.Moja ya studies kule Uswiss,imeonyesha kwamba mtu anaekunywa chai ya kijani ana ufanisi mzuri wa kumbukumbu katika ubongo au akili yake.Chai ya kijani husaidia kuziba kujengwa kwa Plaques ambayo inaunganishwa na vijidudu vya Alzheimer’s.

 Kisukari
Chai ya kijani imeonekana kusaidia kuweka sawa blood sugar kwa watu wenye kisukari.Kwasababu catechins hushusha cholesterol na blood pressure,hulinda na kuharibika kwa kisababishi kutokana na high-fat diet .

Kupunguza uzito
Chai ya kijani husaidia kuongeza na kubadilisha pia metabolism,kwahiyo unaunguza calories nyingi tokea kwenye mafuta .Chai ya kijani pia husaidia kuongeza uzito uliopotea.
Ni fagio la kusafisha vyakula vya sukari au vinywaji vya sukari.Kila kitu hubakia sawa,kama 1-2 kikombe cha chai ya kijani kwa soda moja ya kopo,kwa mwaka mwingine utakua umesave zaidi ya  calories 50,000 . Ambayo ni zaidi ya pounds 15.

Hulinda na cancer
Chai ya kijani imeonyesha athari kwa cancer.Lakini chai ya kjani imejulikana na imetambulika kisomi zaidi huongeza seli zenye afya katika stage zote za ukuaji.Kuna dalili za kuwa chai ya kijani husaidia kuangamiza seli za cancer.
 Hupunguza stress
Kufyonza au ile style ya kunywa chai kwa kuifyonza husaidia kuwa mpole na kupumzika.Amino acid inayoitwa amino acid theanine hupatikana kwenye chai ya kijani huleta afueni ya mapumziko na calming.

Tips za afya:
  • Usiongeze chai ya kijani kwenye maji yanayochemka sana.Utaziua catechins. Vizuri maji yafikie 160-170 degree
  • Weka ndimu Vitamin C hutengeneza compounds ambazo rahisi kuyeyuka katika chai ya kijani.Maziwa kwa maana nyingine kwenye chai ya kijani huleta ugumu ya kuyeyusha catechins.
  • Kipimo cha compounds za afya kwenye chai ya kijani hutofautiana. Rule of thumb: Ya kutengeneza mwenyewe ina faida za kiafya nyingi zaidi kuliko chai ya kijani ya kopo.
Unaweza kunywa kwa siku vikombe 4 ,viwili unaweza ongezea caffeine na viwili usiweke. Japokuwa huonekana sio nzuri kiafya.Na pia sio njia nzuri ya kujenga afya yako.

Tuesday, February 4, 2014

KUONDOA WEUSI CHINI YA MACHO.

10:31 AM // by Kalma // No comments


 Kulala na kupumzika ni muhimu kwa kuwa na afya nzuri na muonekano bomba.Kuanzia kwenye kuboresha akili,kuongeza ufanyaji kazi mzuri wa moyo,kuongeza ubunifu katika ufanyaji wako wa kazi,faida zake huwa hazina mwisho.Lakini sio rahisi kuupata usingizi wa kutosha kwa kila usiku-na wakati mwingine huonesha usoni chini ya macho huitwa(miwani)na puffy eyes.Japo kuwa tiba yake ni kutibu chanzo cha hilo tatizo ambao ni usingizi na kupumzika vya kutosha.Hizi njia za asili chache,hufix macho ya usingizi….kwa usiku pindi haukupatikana usingizi kama ulivyotakiwa katika mipango.
Viazi.
 Viazi vina asili ya enzymes wanaong’arisha ngozi huitwa catecholase, ambao husaidia kufifiza weusi chini ya macho.Weka kiazi kibichi katika hiyo sehemu ya machoni unaweza kukikata vipande vidogo vyembamba au kwa kusaga kupakaa kama uji.Weka kwa 30 dakika kisha toa,osha uso kwa maji ya kawaida tu ukihisi ulazima.


 Mint leaves
Pakaa majani ya mint kwenye sehemu hiyo ya machoni huleta kuwakwa moto ile kama ukali wa mfano vicks,huongeza msukumo wa damu katika hiyo sehemu na kuondoa weusi.Rahisi ponda majani ya mint kidogo na pakaa machoni hapo kwa dakika 5.Osha uso kwa maji ya kawaida yaani cool water .Unaweza tumia majani ya mint ukachanganya na asali au olive oil kabla hujapakaa kwenye macho .Nayo ni kwa dakika tano . 

Tea bags
Caffeine ndani ya  caffeinated teas,kama chai ya kijani (green tea)kwa muda kukazisha ngozi chini ya macho kuiachia mishipa ya damu kuondoa maji yalozidi, pindi  herbal teas (kama chamomile)huondoa kuungua na m-badiliko wa rangi na kuondoa udhia .Kupaakaa,weka tea bags mbili ilowanishe kwenye chai na  uiache zipoe.Weka kila tea bag moja kwenye macho yako yakiwa yamefungwa kwa kuilaza kwa dakika 15 pindi umekaa mkao wa kujilaza.


Rose water
Rose water ina vitamins kama A na C, ina antiseptic, anti-inflammatory na anti-bacterial pia,na vile vile ni kama balancing effect,ni chaguo zuri la kutumia kwenye ngozi.Unapakaa hayo maji chini ya mcho kwa dakika 10 kwa kulowanisha pamba na kutumia kupakaa.




Matango
Weka vipande vya  matango ya baridi kwenye kila jicho husaidia kuondoa uchovu ,puffy eyes kwa kuyapooza kwake,na husaidia kulainisha ngozi ya machoni mwako.La kuongezea,matango hufanya kazi ya toner na kung’arisha uso,husaidia kuondoa mabadiliko ya rangi katika ngozi.Wengine husema kutumia matango machoni ni tiba ya kizamani lakini hiyo ni wewe kama utaiweka akilini,lakini wengine na mimi nikiwemo ni njia tuliyojiaminisha kuwa nzuri na inasaidia. 
Ni muhimu kunote kwamba weusi chini ya macho husababishwa na upungufu wa usingizi,na sio kama ni lazima hiyo kuwa ndo chanzo. Allergies, matatizo ya pua(nasal congestion), na stress ni sababu za kawaida, nazo pia. Kuligundua tatizo itakupa njia rahisi ya kutibu kwa urahisi na ndani ya muda.