• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Sunday, September 29, 2013

MBIRIMBI (Averrhoa, Carambola).

2:39 AM // by Kalma // 1 comment

MBIRIMBI
Ukiitamka Mbilimbi au mbirimbi zote sawa, ila sana tumezoa mbirimbi.
   Umetokana na mti mbirimbi na unazaa matunda mbirimbi, asili yake ni Bara la Asia, na hapa kwetu Tanzania maarufu sana visiwani Zanzibar,huko Unguja na Pemba.
Na wahindi wanaupenda sana!! hata bara mikoani upo sana tuu.
Mmea wake kama mwaridi ,mche wake una majani mawili.
   Ni tunda dogo lenye rangi ya kijani iso kooza, na ikiiva huwa rangi njano,ina vimbegu ndani na moyo pia km unopatikana kwenye ndizi mbivu hizi, ina maji mengi ndani yake.
  Hutumika kama kiungo cha mchuzi ili kuleta ladha ya uchachu badala ya ndimu au limao.
    Sie wanapenda sana kututania jamani! Ni kweli tunasema hivi, “Eti bora ukatwe mkarafuu kuliko mbirimbi" kwa jinsi unavopendwa kule Pemba.
Hutumika kwa achari, "appetizer" japo ina matumizi ya kutosha ikiwezekana kila mtu awe nao mti huu.
   Hili tunda lilianzia Malabar na kuenea Portuguese. Hutumika kwa;
          Kutengenezea salad na hata jam kwa ajli ya mkate.
           Kuni zake nzuri kwa kupikia, zina waka haraka na haziishi mara.
           Ina vitamin A na madini ya potasiam hutumika kutengenezea rangi.
           Ni dawa Haluli ambayo ina oxalic acid ndani yake.
           Ni dawa ya ngozi iloathirika  kwa kujipakaa maji yake.
           Inatuliza homa kali pia.
           Huondoa madoa kama ya kutu ktk nguo za aina  linen.
Waphilipino wao hutumia kwa kutibu kuvimba kwa mwili, homa ya mifupa .
            Ina control na kupunguza tumbo,kitambi yaani Obesity.
Hatuna haja ya kuhangaika kutumia dawa za kichina , wakati mbirimbi ni kila kitu .
 

                 ACHARI YA MBIRIMBI
Kuna ya mbirimbi nzima na ya kusaga.
      MBIRIMBI NZIMA
Osha mbirimbi zako kiasi, pasua kati ziwe pande mbili toa moyo wake,pilipili,vitungu maji, karoti,tangawizi, vitunguu saumu .
Sufuria lako tayari tia mafuta yakichemka kaanga vitunguu maji vikiiva tia thoum,na tangawizi ilotwangwa, vikiiva tia mbirimbi,pilipili na karoti  subiri viize kwa dakika saba mpaka kumi.

  YA KUSAGA
Osha mbirimbi zisage kwenye  mashine ya kusagia zisagike vizuri obvious utasaga na maji kiasi iwe sio nzito na sio nyepesi.
Sufuria yako tia mafuta ya kupikia kaanga vitunguu maji vikiiva tia tangawizi na vitunguu thoum vilotwangwa, vikiiva tia nyanya zako upike kama mchuzi na karoti na pilipili,mbirimbi iwe ndo kitoweo chako.
Aina hizi za mbirimbi hukaa kwa muda wa mwezi kama itakua inakaa kwenye friji.
Kama hamna friji ianike juani mara kwa mara.
 
Dalili yake ya kuharibika ni hutokea mapovu juu ya chombo ulohifadhia pia hutengeneza ukungu juu au kwenye mbirimbi zenyewe.

Saturday, September 28, 2013

NYANYA

5:35 AM // by Kalma // No comments

Nyanya, kwa kizungu tomato, kwa kule visiwani Zanzibar al-maarufu kama "tungule".Kinajulikana sana kama "Family food"!.

Hii nyanya ni chakula kimeanzia Mexico zamani na kuenea duniani kote. Kwa sasa Spanish ndo kiungo kikubwa jikoni  ambao wanaongoza duniani.   Kiungo cha vyakula tofauti tofauti, pia ni sauce,  ni kachumbari, na ni kinywaji.

Nyanya ina utata sana imeshindikana kujulikana haswaa ni "tunda" au "mboga".
Nyanya ni nzuri kwa afya na kukinga mwili. Ina kazi ya tunda na inafanya kazi ya mboga vilevile  kwa wakati mmoja.
Waspain wao ndo walikuwa wa kwanza kuisambaza hii nyanya kuipeleka Europe huko.

      Europe mnamo 1544 kutokea kwa mtaliano mmoja aligundua aina ya tunda nyanya na wakaitambulisha Italy na ikaanza kuliwa.
  Fikiria kama ni tunda na ni mboga lazma ina faida za kutosha mwilini;
 Inaongeza kinga ya cancer ya matiti, inalinda ngozi na miale ya jua,inafanya ngozi kuwa soft,ina vitamin c kwa sanaa.

Inashauriwa ihifadhiwe ikiwa haijaoshwa na kusikokuwa na mwanga wa jua. Ikiwekwa frijini hupoteza ladha yake halisia.
Tunda nyanya likiwa na mbegu zake ina kinga ya ugonjwa wa moyo, hulinda mifupa, ini, figo, na kuweka mfumo wa damu vizuri.
Wafaransa nyanya inaitwa "pomme d'amour" kwa maana ya "love apple", wakati Italy wao "promodoro" "golden apple" .

Unajua nyanya haiwezi kuwa kitindamlo (desert) japo ni tunda, kwasababu lina "asidi" na pia sio tamu kama matunda mengine. Kwa sasa China wanaongoza kulima na kutengeneza  nyanya dunia nzima, wakifuatiwa na U.S, Uturuki, India, halafu Italy .

Tanzania na mikoa yke inalima sana nyanya lakini kwa matumizi ya ndani ya nchini humu humu tu.Chagua nyanya yenye rangi nyekundu nzurii uwapo sokoni isiwe imehorojeka,kupondeka,yenye ufa na hata kupasuka. Iwapo utapendelea iloiva sana nayo ni nzuri kwa kupikia masalo na marosti basi utaihifadhi kwenye friza lako kwa siku moja au mbili kabla, ukiitoa iache kwa dakika 30,na huwa rahisi kumenya ganda lake.Mbegu za tunda hili sio nzuri kwa mgonjwa  wa vidonda vya tumbo yaani "ulcers" kwa sababu ya acid inopatikana kwake.Hushauriwa wakati wa kuipika nyanya isitumike sufuria ya aluminium sababu ya acid nyingi ambayo ikichanganyika na metali ndani ya sufuria matokeo yake huwa chakula kitaingia aluminium na ni madhara kwa mtumiaji wa chakula hicho.

Juisi ya nyanya ambayo haina vimbegu ni nzuri kwa mtoto aliyeanza kula na nzuri kuila na maganda yake kwa afya na kinga nzuri mwilini.

   Mbegu za nyanya hutumika  kuwa chanzo cha kupata zao la tunda na mboga nyanya.











Friday, September 27, 2013

CHOYA (Carcade/Roselle)

3:39 AM // by Kalma // 1 comment

Kwa kule Egypt zawadi ya thamani ukipenda kumpelekea mtu au familia,sio nyngine ni "bag of carcade tea" kwa maana nyingine tulozoea Choya. Kule Egypt hii  Choya au Carcade tea ni moja ya kinywaji cha tamaduni yao inayothaminika sana.

 Sifa yake kubwa ya hii ,ni rangi yake nyekundu iko poa kiukweli.  Hili ni jani limetokea kwa mmea Haibisus na hutumika zaidi kama kinywaji.
Majani haya huongezwa kwenye matunda kuleta rangi nzuri na ladha nzuri pia. Ina ladha ya uchachu ambao una tia hamu ya kula, yaani mtamu uchachu wake.
     Ina harufu nzuri ya  kipekee ya Vitamini "C" .
Ni kinywaji kizuri chenye kufurahisha na hunoga kitiwapo sukari.
     Inashauriwa kukiroweka kwa dakika tano(5) kwenye maji ya moto na kwa matokeo mazuri iache kwa dakika kumi(10).
Kwa afya nzuri na kukipata fresh kukiandaa kikiwa baridi yaani kilopoa.
    Choya hii ina muonekano au quality tofauti huanzia majani kama maua hivi madogo hadi  makubwa zaidi nayo yana virutubisho Zaidi.
        Ukitumia hii choya mara kwa mara ina faida hizi;
Ina Vitamin nyingi na mchanganyiko wa madini mengine kwa kidogo dogo kama vile Calcium. Inasaidia kuongeza upungufu wa Vitamin mwilini, Huongeza damu pia kwa mgonjwa alopungukiwa damu, Inapunguza  kiasi cha cholesterol , inakufanya ujisikie mwenye nguvu zaidi, Hupunguza stress na majanga ya nafsi, Hujenga kinga mwilini.
  Hupendeza kuongezea kwenye juisi ya matunda mengine kwa ladha nzuri na chache.

      JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua choya yako chache tia kwenye maji moto acha kwa dakika kumi,kisha chuja maji yake yale kiasi cha glass moja.

Chukua pakiti ya juisi ulonunua ila inapendezea Maaza juisi au hata ya azam mango au ya pendekezo lako.
   Mimina kwenye jagi lako la juisi kisha tia glass ya choya uloichuja , koroga,unaeza tia sukari ukipenda.

Ni nzuri na huokoa muda na gharama pia.
Huwa nawaandalia wageni wangu huifurahia na kuisifu hata kwa wengine.
 


Thursday, September 26, 2013

VINYWAJI

1:53 AM // by Kalma // No comments

VINYWAJI

Kinywaji ni kitu cha maji maji ambacho ni kwa ajili ya kukidhi kiu kwa binaadamu.kuna aina nyingi na tofauti tofauti za kinywaji. Kuna maji, vinywaji  baridi, juisi ya matunda, juisi ya mboga mboga , vinywaji vya moto . 

Na vyote hivo ni kwa sababu ya kukidhi mahitaji muhimu kwa binaadam
Kunywa ni tamaduni ya jamii zote duniani.

Vijue aina za vinywaji na faida zake;
   
         KINYWAJI POA (SOFT DRINK)

Kinywaji hiki ni  hakina kilevi (non-alcoholic) navyo ni kama Soda, Maziwa, Hot chocolate, Chai, Kahawa,Milk shake(sharubati), maji ya bomba, vinywaji vya nguvu, n.k.


           KINYWAJI CHA MOTO (HOT DRINK)


Kinywaji hiki ni cha moto au uvuguvugu kama vile maziwa,maji ya moto, chai , kahawa.


            JUISI YA MATUNDA(FRUIT DRINK)
Kinywaji hiki ni cha asili chatokana na matunda, kama chungwa au dalanzi ni nzuri kunyweka asubuhi yaani (breakfast).

Maji ya madafu ni mazuri matamu halafu ni freshi kabisa na yanajenga afya, na tiba ya kusafisha "mkojo" pindi mchafu. Matunda yanatoa juisi nzuri na tamu ladha yake. Juisi hujenga mwili na kutia nguvu na inaongeza vitamini mwilini.


Parachichi, apple, ndizi mbivu ni juisi nzuri kwa mtoto wa miezi sita na kuendelea husaidia kulainisha choo.

           JUISI YA MBOGA MBOGA
Juisi ya mboga huwa inakua ya moto,mboga tofauti  tofauti,inatengeneza juisi kama vile karoti, nyanya,matango,n.k.


        Juisi nyingine za mboga huchanganywa na matunda kwa ladha nzuri. Juisi hii hulinda mwili na vijidudu, na cancer pia.
Hujenga mwili na kutia nguvu.

           KINYWAJI KISICHO NA KILEVI.


Ni kama Azam malta, Grand malta ,na vingi vingine huwa ni kiburudisho. Vinywaji hivi vinaongeza damu vina vitamini mwilini. Huongeza uzito wa mwili, sio vizuri kwa kujenga afya ya mtoto mdogo, na ukivizoea unakua kama ulevi japo havina kilevi, na huongeza tumbo au kitambi.
   Haishauriwi kumpa mgonjwa  aina ya vinywaji hivi.

Wednesday, September 25, 2013

MATUNDA

2:47 AM // by Kalma // 1 comment

 MATUNDA Matunda ni sehemu ya maua yatokanayo na mbegu tofauti toauti.Kwa kawaida Tunda ni tamu hata kama "chachu"basi lina ladha nzuri na tamu kwa muonjaji.

 Kuna matunda ni Tunda na Mboga pia kama vile; nyanya, tango, zukini.  Matunda yanajenga mwili, yanamaintain afya na uzito, yanalinda mwili na vijidudu(diseases) mbalimbali, ni mlo kamili pia na mazoezi ya mwili. Matunda ni matamu na mazuri kwa mlaji. Yanaongeza vitamini na madini, yanasadia kuyeyusha chakula mwilini kwa haraka. Matunda yanapendezesha sahani kwa rangi zake tofauti tofauti nzuri na zenye kuvutia.

Enjoy and Share !






Monday, September 23, 2013

CHAI

6:09 AM // by Kalma // No comments

Chai

Chai ni kinywaji cha moto yaani HOT. Kawaida huchemsha maji unatia majani, inakua tayari. Wengine hupendelea kuweka viungo kama mdalasini,karafuu,iliki,tangawizi, ina ladha nzuri kwa mnywaji.


Chai inatumika asubuhi kama kifungua kinywa na vitafunio japokua wengi tunapendelea  na mikate. Vilevile chai inatumika pia jioni km kiburudisho koo.
Kawaida huwa inatiwa sukari inakua nzuri na tamu, ila ukiweka asali nayo huwa nzuri pia.

Fuatilia faida za chai;

              1. Ni rahisi kutengeneza .
              2. Huokoa muda na gharama pia.
              3. Kinywaji cha haraka kwa wageni.
              4. Inapunguza uzito.
              5. Inalinda mwili na miale ya jua.
              6. Inajenga mifupa
              7. Inapunguza blood presure.


Hzo chache katika faida ila ni tiba ya kichefuchefu na kiungulia kwa mama mjamzito au mgonjwa anejisikia vibaya.
Hupunguza uchovu wa hapa na pale.


    Wachina wanaona ni dawa kabisa.Na wao walitambulisha Britain mnamo karne ya 17 nao wakaitambulisha India karne hiyo hiyo, ilipatikana faida ya ushindani wa biashara dhidi ya India na China .


   Chai nzuri kwa mtoto wa kuanzia mwaka na miezi sita na kuendelea! Pia sio nzur kuinywa sanaa kupita kiasi,huwa kama kilevi  pindi ukiikosa unajisikia kuumwa hivi.

Sunday, September 22, 2013

CARROTS

1:03 AM // by Kalma // No comments

carrots

Carrots ni tunda la mzizi,ina rangi ya orange,hudhurungi,njano, hata nyeupe pia. Ukiila pindi fresh ni kama kripsi hivi. Ni mboga vilevile ni tunda, ni mboga yenye afya duniani kote. Sahau kuhusiana na vitamin "A" mbayo wengi tunaifahamu pia ina faida nyngi hizi zifuatazo;
          1.  Inaongeza kuona, haswa nyakati za usiku.
           2. Inazuia cancer
           3. Inang'arisha na kutengeneza ngozi imara.
           4. Inakinga ya mwili na uharibifu wa ngozi.
           5. Inapendezesha ngozi na kulainisha pia.
           6. Inazuia maradhi ya moyo
           7. Inasafisha mwili na kutoa uchafu kwenye ini.
           8. Inaimarisha meno na fizi
           9. Inaepusha kiarusi yaani(stroke).
         10. Hutia nguvu na kujenga mwili .

Saturday, September 21, 2013

KAHAWA

4:58 AM // by Kalma // No comments

Unakubaliana na mimi kwamba "mambo hubadilika?" Wachina ndo walikuwa wanakunywa sana chai,kwa sasa wanaongoza kwa kunywa kahawa na kutengeneza zenye ladha tofauti  tofauti kwa mnywaji .

Friday, September 20, 2013

JIKO MIPANGO

12:54 AM // by Kalma // 1 comment

Weka jiko lako liwe simple. Na kama unatumia viungo vilivyo bora,huitaji chochote kingine kufanya chakula chako kiwe kitamu na kizuri; ni kisu,ubao wa kukatia,na vifaa vyako vya kupika vya kila siku.

Thursday, September 19, 2013

USAFI WA VYOMBO

11:40 AM // by Kalma // No comments

Nadhani kubwa ni kuosha vyombo umalizapo kupika. Osha visu vyako, ubao wa kukatia, sufuria, sahani na bakuli, sinki lisionekane limejaa. 
Kufanya hivyo inasaidia kupunguza msongamano wa kazi, na la zaidi kuepukana na bacteria wazaliwao kwenye chakula.

KITCHEN TIPS

10:42 AM // by Kalma // No comments

Always remember; If you are alone in the kitchen and you drop the lamp you can always just pick it up. Who's going to know.

Tuesday, September 17, 2013

Ladha ya cookies

9:52 AM // by Kalma // No comments

Ladha ya cookies





Ya kumung’unya au crunchy,chocolate au nutty,iwe flat au ya maumbo …Cookie au kileja ni kileja tu,lakini inategemea ni sehemu gani asili yake duniani,Cookie inaweza kuitwa kwa jina lingine na inaweza onekana na ladha tofauti kutokana na aina ya cookie unayotumia.

Cookie au kileja ni jina linalotumika kwa ajili ya utamu wa sukari,iliyo okwa,unga na chakula.Lakini inaweza kuwa na umbo lolote ,kipimo au size yoyote,ladha na muonekano pia.Nchi inaweza kuwa na aina yake ya Cookies inaweza kuwa mpauko,laini na mnyambuko,wakati kwingine ikawa ya pembetatu yenye jam au waffle na imewekewa shira au syrup.

Bado ni cookie kwa vyovyote jina ni hilo kwa nchi yoyote,inanukia vizuri kama ni yenye sukari na tamu.

Cookie ya kwanza,haikudhamiriwa iwe cookies.Tarehe za nyuma kwa karne ya saba Persia-nchi ya kwanza kulima na kutumia sukari-iliaminika kwamba cookies ni kitu asili ya kujaribu cake kwa temperature ya oven. 

Lakini kwa kukua kibiashara na vitu vitamu,mbinu za mapishi na ingredients,iliwasababishia kujitengenezea njia mpaka Northern Europe na duniani kote,matokeo yake yakazaa aina tofauti tofauti za cookies tunazozijua leo. Labda kama umesikia mfano wa cookies duniani kote,utakumbuka kwa ladha ya nchi nyingine.Inategemea wapi ulipo,Baadhi ya hizi cookies zinanunuliwa madukani,zinatolewa oda kwenye maduka haswa ya mikate yaani bakery na baadhi ya migahawa ya kahawa,au zinapatikana kipindi cha ndani ya mwaka masokoni.

 Cookies za kitaifa Australia ni Anzac biscuit, yaani “bikkie”inayotengenezwa na oats na nazi na golden syrup,inaokwa kila siku katika moja wapo ya bakery huko Sidney,hutumia unga,ambayo inatengenezwa na aina mbili tofauti za nazi.

Lebkuchen, ni laini aina ya cookies za tangawizi zenyewe ni tamu,zenye ladha ya nutty,zinapatikana wakati wa Christmas haswa masoko ya kipindi hiki.Wengi wetu tunazifahamu .

Macaron zenyewe ni crisp,inawekwa genache, zinayeyuka mdomoni zina kila rangi na ladha.Na mpenzi yoyote wa aina ya  hii macaron lazima atembelee paris ni maarufu kwa jina Ladure’e, ndo kama macarons.

Panellet hii ni cookie ya kispanish ambayo ndo ya asili inaandaliwa Dia de Todos los Santos, or saints day,Huko Spain -inatengenezwa ,na almonds yaani lozi,zinaundwa kwa mduara inazungushiwa cocoa powder,candied cherries,nazi iliyokunwa,pine nuts na ladha na hata ladha ya kahawa au mdalasini.

Sehemu nzuri ya kuipata ladha ya hii ni 

Barcelona’s Foix de Sarria,kwenye bakery ambayo inatoa huduma nyingi yah ii aina ya panellets.

Nertherland ,stroopwafel ndio kitu kitamu cha kitaifa inatengenezwa kwa kuchanaganya aina mbili za waffle za mduara inawekewa shira au caramel,na inachoviwa chocolate.

Inapatikana Amsterdam kwenye mtaa wa soko la Albert Cuyp,ambapo wanaongezea na kidogo na syrup.Inajulikana pia kama vanilla cresent,avanillekipferl 

ni ndogo,lenye umbo inatengenezwa na almond yaani lozi,nuts,au hazelnuts,inatiwa ladha ya vanilla na inawekewa sukari. Inapatikana mgahawa wa Café Central au Demel huko Austria nazo zina ladha nzuri.

Na ukweli cookies za chocolate chip ladha yake ni ya chocolate,inatafunika na gooey hii ni cookies za marekani.

Enjoy and Share !