• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

clean.sakamia.com Returning home to a house that’s clean, serene gives you a special and healthy feeling

Saturday, May 30, 2026

Mahitaji ya Msingi ya Mapambo ya Kila Chumba Katika Nyumba Yako

1:41 AM // by Kalma // No comments

Mahitaji ya Msingi ya Mapambo ya Kila Chumba Katika Nyumba Yako
Unaweza kuwa na mtindo wa mapambo ya jumla uliochaguliwa nyumba yako yote, lakini kwa mtindo wa jumla, kila chumba kina kusudio na mtindo wake. Jinsi matumizi ya chumba,kinatumiwa  na nani, inapaswa kuzingatiwa unapopanga kila chumba na kuchagua vifaa,mapambo, na uzuri na aina ya mapambo hayo.

Zingatia mahitaji ya kila chumba na muhusika binafsi, na mapambo kulingana na nafasi ya hicho chumba. Mapambo ya nyumba yanapaswa kuonyesha hisia na ladha yenye maslahi binafsi, lakini lazima pia izingatie kazi maalum  ya hivyo vyumba.

01

Living rooms(sebule ya kupumzika na familia)

Sebule zinaweza kutumika kwa  kazi nyingi, ni chumba rasmi kinatumika kwa kusalimiana na wageni,ni sehemu hata familia inatumia kusoma kwa Pamoja, ni sehemu ya burudani,kufurahia na kucheka Pamoja,na kucheza pia.Kwa nyumba za kisasa, sebule ni chumba kikubwa kimekuwa karibu na kuhusishwa Pamoja na jiko na dining area.Kubwa la kuzingatia ni kuchagua haswa mahala kwa ajili ya sebule au living room na haswa kuweka eneoau sehemu ya mazungumzo. Chaguo lako na mipangilio ya hiyo sebule yapaswa kiuzingatia akilini mwako.Hapo ndipo unaweza kusonga na mipangilio jinsi ya pa kuweka taa,sehemu ya zulia au rugs,marembo ya sanaa na mengineyo.

02 

Vyumba vya kulala(Bedrooms)

Unatumia theluthi moja ya maisha yako kwenye chumba cha kulala, kwa hivyo unapaswa kuzingatia kwa uangalifu mikakati ya kupafanya mahali pazuri. Anza na kuchagua kitanda na fanicha zingine za chumba cha kulala. Wakati unaweza kuokoa pesa katika maeneo mengine,nunua godoro na mito bora na huo n dio  uwekezaji mzuri.Chaguo lako la rangi pia ni muhimu kwenye chumba cha kulala-chagua rangi zisizokolea ikiwa wewe ni mtu wa asubuhi, au rangi zilizokolea kama wewe ni wa kuchelewa. Taa ya chumba cha kulala ni muhimu kwa kuweka mood au hali nzuri, na pia

Ikiwa huna sehemu kubwa,tafuta ideas ya kupamba chumba kidogo kipendeze.Na vyumba vya kulala vya wageni vina mahitaji yao ya kipekee kwenye  kupamba.

03

Vyumba vya watoto

Kwa mapambo ya vyumba vya watoto, bado ni mazoea ya kawaida kutumia mandhari ambayo kwa ajili ya  wavulana na wasichana, ingawa wazazi wa kileo wameazidisha kutengeneza kufanya vyumba vya watoto kuwa vya kijinsia zaidi.

Chumba cha mtoto mchanga kina mahitaji yake ya kupamba, haswa ambapo familia za vijana ambazo bajeti inaweza kuzingatiwa.

04

Bafu ya kisasa

Je! Unataka kubadilisha bafu lako kuwa spa ya kifahari? Angalia ideas za bafu , pamoja kukifanya chumba kihisi ni mapumziko  na cha kisasa, na jinsi ya kuchagua makabati, tile, sinki, vioo, taa, na marembo. Katika bafu dogo, changamoto ni kuliremba ili lionekane kubwa.Ikiwa bafuni yako mpya inajumuisha mradi kamili wa kurekebisha, tafuta vidokezo juu ya kufanya liwe zuri na la kisasa. Maamuzi mengine muhimu yatakuwa kuchagua rangi na kuchagua sink zuri na marembo ya kuvutia.

05

Jikoni

Jikoni kunaweza kuwa ni chumba cha gharama kubwa kurekebisha, kwa hivyo unatakiwa kupanga kwa uangalifu mradi  huo wako. Ikiwa urekebishaji kamili haitoshelezi na budget yako,basi tumia njia rahisi kuleta muonekano,ikiwemo usafi wa kina yaani deep cleaning,kurudia rangi,kuweka taa za kisasa,kubadili makabati,kuongeza mapambo,kubadilisha sink,mifereji na mabomba.Mwishowe, chaguo mapambo pekee na rahisi yanayoweza kufanya jiko lionekane jipya kabisa.Na kwa kweli,kwa  uchaguzi huu wa mapambo ni sehemu kuu ya  uboreshaji wowote wa jikoni ya bajeti  ndogo ya mradi huo.

06

Chumba cha kula(Dining Rooms)

Meza katika chumba cha kulia ni yaani dining room table ni kitu muhimu humo,kwa hivyo chaguo na uwekaji wake ni muhimu katika mapambo. Kuchagua fanicha sahihi inaweza kuwa muhimu sana kwa chumba kidogo cha kulia. 

Vitu vingine muhimu vya kuzingatia ni viti na taa za kuning’inia au  chandelier — ambazo zote husaidia kufafanua mtindo wako na kuweka sauti ya chakula. Mwishowe, zingatia kwenye mapazia na vitambaa vya kutandika mezani na marembo mengine.

 07

Foyers

Foyer inapaswa kuwa nafasi ya kukaribishia ambayo huweka muonekano wa  eneo la kupumzika, lakini pia kuna mambo mengi ya kuzingatiwa unapobuni na kupamba foyer yako. Sakafu, vifaa vya kuhifadhia, na aina ya marembo ni mambo muhimu katika kubuni foyer.

08

 Ofisi ya NyumbaniUtakuwa na mahitaji tofauti ikiwa utaona wateja katika ofisi yako ya nyumbani na kutumia nafasi hiyo kwa sababu za kitaalam. Lakini hata ikiwa ni mahali tu kwako kwa ajili ya kufanya biashara  na familia, kuna vidokezo maalum vya kupanga na kupamba ofisi ya nyumbani. Pale ambapo bajeti inazingatiwa, tafuta chaguzi za kuokoa fedha.


       usiache kulike na kushare @sakamiacleaners

 

Tuesday, January 7, 2025

8 MATUNDA UNAYOFIKIRI NI MBOGA

12:54 AM // by Kalma // No comments

8 MATUNDA UNAYOFIKIRI NI MBOGANyanya zilizokomaa ni nzuri, lakini unaweza kula mbichi? Kwa mkulima sio kitu rahisi.

Wataalamu wa mimea watakuambia nyanya ni tunda, na watu wengi wanajua hivyo. Lakini baadhi yao wengi hatujui haswa hii,nyanya kisheria ni mboga. 

Mnamo 1893, mahakama kuu iliamuru nyanya iwe kundi la Mboga”kulingana na jinsi inavyotumika, na ikawa maarufu kwa kujulikana hivyo mpaka mwishowe.Kama unashangaa kwanini mahakama kuu iliamuru kitu kama hichi , ilikuwa inahusiana na mambo ya kodi yaani Taxes. Kipindi hicho mboga zilikuwa zinalipiwa kodi, lakini matunda yalikuwa hayalipiwi kodi.

Kuna baadhi ya matunda tunafananishwa na mboga, imetokana na fikra za watu na jinsi yalivyokuwa yanatumika . Haya ni mengi yatakushangaza.

OlivesOlives ni matunda kwasababu yanatokana na matunda ya olive tree.Kama ungeniliuliza mimi, ningelikwambia olives yalikuwa ni mboga , na sio matunda. Lakini olive ni matunda kwasababu yametokea kwenye matunda ya olive tree. Matunda yanatokea kwenye ovary iliyopevuka ya mmea na ovary inayopatikana kwenye maua. Kwasababu hiyo mboga zote kwa kitaalam ni matunda-yanaota kutokea kwa maua.

BilinganiBilingani kiufundi ni berries –kweli, haya makubwa ! kweli haswaa  

Tunachukulia bilingani ni mboga. Sijawahi kuona likiliwa bichi. Ni matamu -au wakati mwingine ni chachu au chungu-sio tamu. Lakini sio hivyo kwa bilingani tu kwa  wataalamu wa mimea  ni tunda,wanaichukulia ni berries. Berry kubwa yaani kubwa sana.Sioni mimi binafsi kulitupa moja linapokaribia kuwa laini kwa wakati wowote .Boga,squash na zukini Boga,squash, na zukini yenyewe yanaanzia kwenye maua ya mfano wa mizabibu yaani vines.Boga na aina ya squash ,ikiwemo zukini, yanaanzia kwenye  maua ya vines na kiufundi ni matunda.TangoMatango,ni kama mpwa wa squash,nalo ni tunda. Matango yanafanana sana na maboga na squash, na ni kama mtu na mpwa wake, kiufundi ni matunda. Unapoliona linaning'inia kwenye vines na matunda bado huwa yameshikana mpaka mwisho,  hivi inaleta maana sivyo? 

Maharage ya kijani

Maharage ya kijani yaani haya ndiyo huonekana kama mboga,hili ni kweli? Pindi mtoto mdogo hataki kula maharage ya kijani, nini baba na mama huwa wanasema?  "Kula mboga zako".

Labda kama  maharage ya kijani yaliitwa matunda ,wakati kiufundi  ni sahihi kuwa ni tunda,Watoto wangekuwa wanahamu zaidi kula .

BamiaBamia  —haijalishi inatokana na familia gani -imepata umaarufu kwa miaka sasa.Umaarufu wa kukuza bamia kwa miaka michache iliyopita,na haikuwa na hadhi kivile nayo ni mboga ni yatosha kuwa kama kale au cauliflower,bado inaweza kuwa na umaarufu mkubwa. Na hata kama inayo, utajua ukweli kwamba si Mboga. Nayo ni tunda.

Pilipili

Aina ya pilipili  Habanero inakuzwa kwa mapenzi ya kivuli.Ni ukweli inaonekana sio sahihi  kwamba pilipili kuwa katika hii list,haswa pale unapogundua kitu kama habanero – pilipili ina joto mara 70 ya jalapeno – nayo kiufundi ni tunda. Lakini huenda pilipili iko kwenye upande wa ladha ya tamu mfano pilipili boga au inakuwa upande wa kiungo kikubwa kama habanero,ambayo yote hutokea kwenye matunda na huwa ni tunda.Kwanini tunaita baadhi ya matunda ni mboga?

Ratatouille

kiufundi, chakula aina ya ratatouille ni kitamu, kinaweza kuwa chakula cha kuokwa yaani baked au cha tunda.Kwanini matunda yote haya yamejulikana kama mboga? Kwa hisia nzuri kwakuwa sio matamu ladha yake, na ni kwasababu sukari halisi iliyo ndani yake inapatikana kwa kiasi kidogo, watu wanayopika hayo wanayatenga kama ni mboga kuambatana na ukweli kwamba mboga ya kiukweli inatokea kwenye majani,stalks,mizizi, tubers,na bulb za mimea, au mboga ni matunda ya mimea, kama broccoli.

Lakini fikiria hili. Chakula kama ratatouille kimetengenezwa kutokea kwa nyanya ,bilingani na squash, tukizungumzia kwa kitaalam wa mimea ni kama salad ya matunda ya kuokwa

 Nyanya ni tunda au mboga?

Share and Enjoy !

































 

 

Tuesday, May 23, 2023

10 FAIDA ZA KUSOMA KILA SIKU

4:49 AM // by Kalma // No comments

10 FAIDA ZA KUSOMA KILA SIKU

Lini ilikua mwisho kusoma kitabu,au gazeti,au maandiko yoyote?Je una tabia ya kusoma kila siku kwenye mitandao ya kijamii yaani Tweets,Facebook,au maelekezo katika vitu unavyotumia?Kama ni mmoja wapo ambaye husomi kila mara,kwa hali hiyo unakosa mambo mengi: kusoma kuna faida nyingi sana , na nyingine hizi zifuatazo hapo chini.

1. Kuistua akili

Wasomi wengi wameonyesha kwamba mara zote akili ikiwa inafanya kazi ina uwezekano mkubwa wa kulinda na ugonjwa wa Alzheimer na shida ya akili kitaalamu unaitwa Dementia, kufanya ubongo wako kua hai na huulinda usipunguze nguvu.Na hufanya kazi kama misuli mingine mwilini,akili inahitaji mazoezi ili iwe yenye nguvu na yenye afya.Ni sawa na kucheza michezo mingi kama mchezo wa bao unaochezwa kuanzia watu wawili, ni mchezo ambao husaidia kuifanya akili kuwa yenye nguvu.

2. Huondoa msongo wa mawazo 


Haijalishi una msongo wa mawazo wa kiasi gani inaweza kuwa kazini,katika mahusiano yako binafsi,au katika mambo ya maisha yako ya kila siku,la kufanya ni kutupilia mbali ikiwa utazubaa kwenye hadithi nzuri.Kitabuni au riwaya iloandikwa vizuri itakusafirisha kukupeleka kwingine kabisa,wakati hicho unachokisoma kitakufanya uwe katika hali iliomo humo kwa muda huo,huondoa wasiwasi na uoga na kitabu kitakupumzisha .

3. Maarifa 

Kila unachokisoma kinaleta habari mpya kichwani mwako,na huwezi jua kipi kitakuja mkononi mwako.Kuwa na maarifa mengi ,ndio kuwa na uwezo wa kupambana na changamoto zinazokukabili.
Kwa kuongezea zaidi,hiki ni chakula cha kukifikiria: ushawahi kukutana na hali ngumu,kumbuka yote hayo yanaweza yakapotea –kama hela ,kazi,nguvu,afya,lakini tisa kumi maarifa uliyokuwa nayo hayawezi potea na hubaki milele.

4. Upanuzi wa misamiati

Hii huendana na hiyo nukta ya hapo juu: unaposoma sana,ndivyo unajua misamiati mingi,na huwa ni maneno unayaotumia kila siku.Kujua misamiati mingi na kuongea kwa ufasaha ni msaada mkubwa katika taaluma yoyote,na tambua kwamba unaweza kuzungumza vizuri na ujasiri wote wa hali ya juu na itaongeza kujiamini na thamani yako kupanda pia.Itaongeza thamani ya kazi yako,kama wale wasomi wazuri,huongea vizuri,na wana maarifa ya kutosha katika mada tofauti tofauti huwa wanapata kukua na kujijenga haraka zaidi kuliko wale wenye misamiati kidogo na ujuzi wao udogo wa fasihi,utambuzi wa kisayansi,na matukio ya utandawazi.

Kusoma vitabu ni muhimu pia kwa kujua au kujifunza lugha mpya,kama kujua maneno yalokuwamo kwenye kurasa. Ambayo huongeza ujuzi wa kuyaongea na kuandika kwa ufasaha.

5. Huongeza kumbukumbu

Pindi unaposoma vitabu,unatakiwa kukumbuka wahusika,asili zao,matamanio yao,historia zao,na pia vitu tofauti tofauti vyenye mahusiano na wahusika kwa kila habari.Kwa mfumo wa kumbukumbu,lakini akili ni kipande cha maajabu ambacho huweza kukumbuka vitu na kukumbuka vitu hivyo vyote na hat mwisho wake vilipoishia. Ni jambo la ajabu ya kutosha,kila kumbukumbu mpya inayoingia katika akili hutengeneza ujuzi,na huzidishaukomavu wa akili,ambayo husaidiwa na mfumo wa muda mfupi wa kumbukumbu na kukomaza kukumbuka hizo hisia.Unaionaje hiyo? Imetulia!  

6. Uwezo wa uchambuzi sahihi

Hivi ushawahi kusoma vitabu vyenye hadithi za kusadikika,na ukapata suluhisho wewe mwenyewe kabla ya kumaliza kusoma? kama hivyo ndivyo,ulikuwa na uwezo wa kuchambua na kudadavua mawazo ukayafanyia kazi kwa kuandikamaelezo yote uliyoyapata na kutengeneza matumaini mapya.

Huo ni sawa na uwezo wa kuchambua ambao mikono yako imemiliki inapokuja haja ya uchambuzi. Kwanza kujua ulokiandika kipo sawa,kama wahusika walihusika vizuri, hadithi ilitiririka vizuri n.k. Ulishawahi pata nafasi ya kusimuliana kitabu na wengine,utakua na uwezo wa kuyachambua maoni yako kwa vizuri,kama uliutumia muda wako vizuri kufuatilia kila ulichokisoma.

7.Huongeza umakini wa uono wa maoni  

Katika  uchizi wa dunia ya mtandao,umakini unapatikana katika milioni ya muelekeo tofauti tofauti kwa wakati mmoja kama tunavyovifanyia kazi nyingi kwa kila siku. Kwa kila dakika tano ya maisha,wastani wa kila mtu hugawanya muda wake katika kafanya kazi,kuangalia barua pepe,kupiga soga yaani kuchat na watu zaidi ya mmoja,(kupitia gchat, skype, whatsaap n.k),macho yote kwenye twitter, kuangalia smartphone, na muingiliano baina na kati ya wafanyakazi wenzake. Hii aina ya tabia husababisha kuongezeka kiwango cha msongo wa mawazo,ambayo hupunguza uzalishaji wetu.

Pindi unaposoma kitabu,akili yako yote inakomaa na hadithi-na vingine vilobakia hupotea au  unavipuuza na utajidhatiti zaidi kujishughulisha na undani wa maelezo unayoyapata kutokea kwenye hadithi. Jaribu kusoma kwa 15-20 dakika kabla ya kazi(i.e asubuhi yako,kama unatumia usafiri wa wote),utashangaa kwa ugunduzi, maarifa na akili kuchangamka ambao uutakuwa umeupata ufikapo kazini.

8.Ujuzi wa kuandika vizuri  

Hii huwa mkono kwa mkono na uelewa mzuri kwa upana wake wa misamiati: Utaalam wa kuweka wazi,kazi nzuri ya maandishi huwa ni matokeo ya mwandishi mwenyewe,kama ugunduzi wa maanguko,mtirirriko,na aina ya uandishi wa baadhi ya waandishi,na utaalamu wa mbinu za uchoraji na utunzi wa waandishi tena wakufunzi waliopita, huwa ni matokeo kwa waandishi wameajifunza kutokea kwa kusoma kazi za wengine.

9. Utulivu

Kwa kuongezea kitabu kitakupa mapumziko au furaha ambayo inapatikana katika kusoma kitabu kizuri,na inawezekana somo unalolisoma likakupa faraja ,matumaini na utulivu wa amani ya nafsi. Kama kusoma vitabu vya imani,hushusha shinikizo la damu yaani blood pressure na hukupa upole aamani na utulivu,na pindi unaposoma vitabu vya sifa ya kutatua matatizo vinavyoonyesha jinsi ya kusaidia watu waliopata tabu katika hali fulani,navyo huleta maumivu ya kuumia.

10.Huburudisha bila ya gharama

Japokuwa wengi wetu tunapenda kununua vitabu na tunasoma na kuwa ndiokumbukumbu zetu za baadae,huweza vikawa bei iko juu. Na kwa kuwa na budget ndogo, au unakosa kabisa kiasi cha kukuwezesha kupata burudani ya vitabu ,unaweza tembelea maktaba ilokaribu na eneo lako au kupitia kwenye maduka na ukapata hata vitatu viwili. Maktaba zina vitabu vya kila aina ya somo uanalofikiria,na utakua unazunguka hifadhi yake utapata hata vipya pia,hautaepuka kuacha kusoma.

Kama itatokea utaishi eneo ambalo halina maktaba,au unaeza ukapata kwingine au hata kwa mtu mwingine kwa urahisi,maktaba nyingi zina vitabu vyake kwenye PDF au ePub kwahiyo unaweza soma kupitia mifumo hiyo,iPad,au compyuta yako.Pia kuna vyanzo vingi kwa njia ya mtandaoni ambapo huweza kupata vitabu vya bure, kwahiyo viwinde hivyo vipya na kisha usome!


Kuna utofauti wa tabia za kusoma kwa kila mtu duniani,na huenda ikawa ukaonja ladha tamu na nzuri
 katika fasihi ya waandishi,utenzi,magazeti ya mitindo,maandiko ya dini,vitabu vya vijana,jinsi ya kutoa msaada,mambo ya mitaani,au vitabu vya kimapenzi,hapo kitakuwepo kinachotaka kwenye akili yako na mawazo yako. Kaa pembeni na kompyuta yako kwa muda,fungua kurasa za vitabu,na ukonge moyo wako kwa wakati mwingine.  

usiache kutembelea blog yetu nayo inaburudisha kuisoma.