• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, May 27, 2015

VYAKULA VINAVYOBORESHA KUMBUKUMBU

7:25 AM // by Kalma // No comments

Ni jambo zuri kujua aina ya vyakula vinathamani zipi katika miili yetu.Chakula ni jinsi tunavyokitumia sisi wenyewe ,na bora zaidi kukiangalia faida ya chakula,kama ni chanzo cha nguvu mwilini mwetu.Tukiwa na ufahamu wa faida za chakula itatusaidia kula vyakula vizuri zaidi katika ubora wa afya,kwa kujisikia tuko vizuri,kiafya na kiakili pia.Nilikua naangalia njia za kukuza na kuboresha kumbukumbu,nilichogundua ni kwamba vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha hili.La msingi tule vyakula vyenye kuujenga mwili vizuri.
 Chai(tea)
Faida ya chai huonekana kama ina mwisho-lakini huathiri kumbukumbu chai imehusika.Antioxidants inayopatikana kwenye chai ina  polyphenols –huboresha kumbukumbu,na hufanya kazi ya utambuzi katika akili.Chai ya kijani na nyeusi inazuia kazi ya enzymes wawili (acetylcholinesterase na butyrylcholinesterase), ambao wanashabihiana na ukuaji na maendeleo ya vijidudu vya Alzheimer.Kama unataka kuboresha kumbukumbu tumia sana chai,na ni vizuri ya kutengeneza mwenyewe,unaweza kuweka viungo vya asili unavovipenda na chai yako ikawa tamu ladha yake.




Rosemary
Kisomi zaidi ilionekana hata harufu tu ya rosemaru huboresha kumbukumbu ya muda mrefu na mfupi pia,na hata mahesabu ya kiakili,kutokea na compounds zinazopatikana kwenye harufu yake.Unaweza ukapanda nyumbani kwako ukawa unaipata harufu hiyo au kwenye chakula kwa kutumia mimea inapatikana kwenye olive oil.


 Kiazi sukari(beets)
Vyakula vyenye Nitrate nyingi kimojawapo ni kiazi sukari,huongeza msukumo wa damu,hufanya akili yako kuwa nyepesi na sharp na hulinda na matatizo ya akili.

 Mbegu za alizeti
Karanga na mbegu inasambaza mwilini omega-3 fatty acids,ambayo ni maarufu kwa kuboresha akili.Mbegu kama za alizeti ina chanzo kizuri cha vitamin E, husaidia kulinda seli za mishipa ya akili isiathiriwe.Kula karanga na mbegu hujenga afya na mwili pia.

Vyakula vyote ni vizuri kupata katika mlo wako wa kila siku.Uwezo wa kuboresha akili ni sehemu ndogo ya ujumla ya faida za kiafya mwilini.Tuweke mikakati ya kuangalia chakula tunavyokula na familia zetu kiwe ni njia mojawapo nay a muhimu katika kujenga afya,kutia nguvu,na tuwe wenye furaha katika maisha yetu ya kila siku. 


 cake yenye mbegu za alizeti.
 mbegu za alizeti zilorostiwa.


SHARE !

Friday, May 22, 2015

VIUNGO NA FAIDA ZAKE

10:06 AM // by Kalma // No comments

VIUNGO, 
Ni mpenzi wa viungo sana,na jiko langu limerembwa na aina tofauti tofauti  pia ya viungo.Zinavutia rangi zake,na vyenye mvuto wa asili harufu yake yenye kuleta hamu ya kula.
Visiwani haswa Zanzibar, Tanga siwezi kuiacha Morrocco hutumia sana viungo,Sio tu kuongeza ladha ya chakula bali pia vina faida nyingi za kiafya na urembo pia.Ni kitu kizuri kujifunza vipi viungo vitatusaidia katika maisha yetu ya kila siku. 
Viungo maarufu vinatumika sana,na Morrocco zaidi katika upishi wao ni: 



Chumvi,pilipili,tangawizi,manjano,(turmeric),pilipili mbuzi(paprika),jira au binzari nyembembe au uzile(cumin),zafarani(saffron) .
Hizo chache hapo juu huenda zikatusaidia katika afya zetu….
Tangawizi  
Njano isokooza rangi yake na harufu kali,inasifika kuwa ni kiungo kizuri chenye  faida nyingi kiafya.Kama unahisi uchovu,au tumbo limevurugika,tangawizi husaidia kutoa hayo udhia.Kuanzia mmeng’enyo chakula mbaya au uliokuwa slow,kutibu joints pia,tafuna kipande kidogo au weka kwenye kinywaji cha moto italeta nafuu.

Manjano (Turmeric)
Hiki ni kiungo kimojawapo kinatumika sana kipindi cha baridi kali huleta ujoto na harufu yake nzuri.Manjano ni yenye asili ya anti-inflamatory hutumika sana kwenye dawa za ayurvedic.Husaidia kuboost immune system,na pindi usikiapo baridi kali mwilini.Na hutumika kupakaa usoni na ni kujisugulia mwilini,hutoa uchafu,hufanya ngozi kuwa laini na hung’risha rangi ya ngozi kuwa yenye mvuto.huleta rangi kwenye chakula.




Pilipili mbuzi au boga(Paprika)
Hii ina lishe nyingi za kiafya katika mwili wetu,na sana Vitamin A.Kijiko cha chai kimoja cha rangi nyekundu ina zaidi ya 100%  ya mahitaji ya kiafya mwilini ya kila siku.Kama vitamin A  husaidia kuona,huongeza madini ya chuma ambayo hutia nguvu mifupa.
 supu yenye paprika.
  Jira (Cumin)
Jira ina nguvu sana,huwa ni kama badala ya chumvi.Ina kiasi cha Sodium kidogo,tumia zaidi hii badala ya chumvi husaidia kushusha blood pressure,ni yenye ladha nzuri katika chakula.Jira ni chanzo kizuri cha Vitamin B,ambayo inasaidia kuleta usingizi.Jaribu kula ndizi iliyochanganywa na jira kabla ya kwenda kitandani kama una shida ya kupata usingizi. 



Zaafarani(Saffron)
Japokuwa hiki kiungo ni cha gharama ,ni kizuri kwa chenye afya nyingi nyingi.Husaidia digestion na inflammation,unaweza ukatumia zaafarani kwa njia nyingi na kuweka kwenye chakula pia.Tengeneza mask ya  maziwa ya zaafarani,chukua zaafarani weka kwenye maziwa mabichi ambayo hayajachemshwa.Kisha iache zaafarani kwa saa mbili kabla ya kuyatumia,maziwa yatakuwa rangi nyekundu.kisha pakaa usoni,iache kwa dakika kumi10 kabla ya kuosha uso.Kiungo hiki husaidia kusafisha uso na ngozi iliokauka na huondoa madoa! 
 Cake ya strwabery na zaafarani.



Thursday, May 14, 2015

Tips bora za kuhudumia mwili.

9:06 AM // by Kalma // No comments

Tips bora za kuhudumia mwili
Kwa kiasi kikubwa sana tunaangalia zaidi urembo wa uso  na muonekano,wakati kuna sehemu huwa zina uvivu kuzihudumia katika  miili yetu.Japokua make-up na marembo mengine unawezesha muonekano wetu,labda na mpaka mara moja moja  kujiangalia zaidi miili yetu,matokeo ya mwishoni hayatupambi muonekano wetu sanaa.Kwahiyo hizi ni Tips chache za kuujali mwili wako katika kujihakikishia muonekano mzuri na wa kuvutia wa  mwili zaidi ndani na nje. 

Tips za kuujali mwili kwa mwanamke.
1. kuondoa weusi katika kiwiko na magoti:
  • Kamua ndimu kupata juisi yake  
  • Kata vipande vya ndimu
  • Sugulia hizo katika weusi /sehemu yenye rangi kwenye kiwiko na magoti
  • Acha kwa dakika 20
  • Lowesha taulo ndani ya maji ya moto kisha sugulia kwenye hizo sehemu. 
2. kulainisha mng’ao wa ngozi:
  • Chukua rose water kijiko kimoja cha kula,kijiko kimoja cha glycerine na kijiko kimoja cha kula cha juisi ya lime.
  • Changanya pamoja weka kwenye chupa
  • Pakaa  kila siku kwa muda wa nusu saa kabla ya kuoga au muda wa kulala hufanya ngozi kuwa laini na ya kung’aa.

3. kuondoa chunjua(warts)kuzunguka vidoleni:
  • Chukua viazi kizima kikate vipande pande
  • Pakaa maji yake kuzungukia hilo eneo la kucha kunako chunjua (hukausha ngozi ilo haribika)
  • Tumia kipande cha pamba,sugulia kwa upole
  • Osha baada ya dakika kumi

4. kuondoa puffy macho ya uchovu:
  • Chukua kipande cha pamba na rose water
  • Lowesha pamba kwa maji ya rose kisha weka hapo machoni
  • Weka kwa dakika 20
  • Lala chali ukiwa umepumzika
  • Husaidia kuondoa macho yenye uchovu na kuleta kupumzika
5. kuifanya ngozi laini:
  • Vijko 5 vya chai vya olive oil na 50gm paste  ya papai
  • Changanya pamoja
  • Pakaa kwenye sehemu kavu za ngozi
  • Fanya hivi mara mbili kila siku kupata ngozi asili na laini


6. mask ya uso kuondoa mikunjo kwenye macho:
  • Vijiko vya chai 3 vya maziwa na 3 vya chai vya asali
  • Changanya pamoja
  • Pasha kidogo huo mchanganyiko
  • Pakaa kuzunguka machoni kwa dakika 30
  • Osha kwa maji ya uvuguvugu 
  • Hii ni njia ya asili ya kupunguza na kulinda na mikunjo ya machoni au chini ya macho

7. Conditioner ya asili ya nywele:
  • Chukua maziwa yanapendekezwa yawe baridi
  • Kabla ya kuoga,pakaa mchanganyiko huo kwenye nywele tumia chanuo kuzichana ,au vidole vyako kuzichambua chambua au spray bottle
  • Acha kwa dakika 30
  • Osha kwa shampoo unayoitumia
  • Maziwa huwa kama conditioner ya asili,hufanya nywele zako kuwa soft na silky

8. kupunguza madoa meusi:

  • Chukua  kikombe kimoja cha curd na yai moja
  • Changanya pamoja 
  • Pakaa usoni, na sana sehemu yenye doa 
  • Acha kwa saa moja
  • Osha uso na maji  
  • Husaidia kutakatisha na kupunguza madoa meusi usoni   
  • Hufanya ngozi  ing’ae kiasili 

9. kupunguza m-ba:

  • Chukua ua  la hibiscus na lisage kupata juisi yake
  • Pakaa kwenye ngozi ya kichwani ,na zaidi sehemu zenye m-ba   
  • Acha kwa saa 1-2 
  • Osha  na maji baridi 
  • Fanya hivi mara mbili kwa wiki kupunguza m-ba 


10.kulainisha mikono migumu na nyayo:
  • Chukua nusu kikombe cha curd na nusu kijiko cha chai cha vinegar 
  • Changanya pamoja  
  • Sugulia  mikononi,viganja na nyayo   
  • Iache kwa dakika 5-10  
  • Osha kwa maji ya kawaida  

Natumai utaona faida yake ukizitumia tips hizi.Tujulishe ukijaribu!