• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, May 23, 2023

10 FAIDA ZA KUSOMA KILA SIKU

4:49 AM // by Kalma // No comments

10 FAIDA ZA KUSOMA KILA SIKU

Lini ilikua mwisho kusoma kitabu,au gazeti,au maandiko yoyote?Je una tabia ya kusoma kila siku kwenye mitandao ya kijamii yaani Tweets,Facebook,au maelekezo katika vitu unavyotumia?Kama ni mmoja wapo ambaye husomi kila mara,kwa hali hiyo unakosa mambo mengi: kusoma kuna faida nyingi sana , na nyingine hizi zifuatazo hapo chini.

1. Kuistua akili

Wasomi wengi wameonyesha kwamba mara zote akili ikiwa inafanya kazi ina uwezekano mkubwa wa kulinda na ugonjwa wa Alzheimer na shida ya akili kitaalamu unaitwa Dementia, kufanya ubongo wako kua hai na huulinda usipunguze nguvu.Na hufanya kazi kama misuli mingine mwilini,akili inahitaji mazoezi ili iwe yenye nguvu na yenye afya.Ni sawa na kucheza michezo mingi kama mchezo wa bao unaochezwa kuanzia watu wawili, ni mchezo ambao husaidia kuifanya akili kuwa yenye nguvu.

2. Huondoa msongo wa mawazo 


Haijalishi una msongo wa mawazo wa kiasi gani inaweza kuwa kazini,katika mahusiano yako binafsi,au katika mambo ya maisha yako ya kila siku,la kufanya ni kutupilia mbali ikiwa utazubaa kwenye hadithi nzuri.Kitabuni au riwaya iloandikwa vizuri itakusafirisha kukupeleka kwingine kabisa,wakati hicho unachokisoma kitakufanya uwe katika hali iliomo humo kwa muda huo,huondoa wasiwasi na uoga na kitabu kitakupumzisha .

3. Maarifa 

Kila unachokisoma kinaleta habari mpya kichwani mwako,na huwezi jua kipi kitakuja mkononi mwako.Kuwa na maarifa mengi ,ndio kuwa na uwezo wa kupambana na changamoto zinazokukabili.
Kwa kuongezea zaidi,hiki ni chakula cha kukifikiria: ushawahi kukutana na hali ngumu,kumbuka yote hayo yanaweza yakapotea –kama hela ,kazi,nguvu,afya,lakini tisa kumi maarifa uliyokuwa nayo hayawezi potea na hubaki milele.

4. Upanuzi wa misamiati

Hii huendana na hiyo nukta ya hapo juu: unaposoma sana,ndivyo unajua misamiati mingi,na huwa ni maneno unayaotumia kila siku.Kujua misamiati mingi na kuongea kwa ufasaha ni msaada mkubwa katika taaluma yoyote,na tambua kwamba unaweza kuzungumza vizuri na ujasiri wote wa hali ya juu na itaongeza kujiamini na thamani yako kupanda pia.Itaongeza thamani ya kazi yako,kama wale wasomi wazuri,huongea vizuri,na wana maarifa ya kutosha katika mada tofauti tofauti huwa wanapata kukua na kujijenga haraka zaidi kuliko wale wenye misamiati kidogo na ujuzi wao udogo wa fasihi,utambuzi wa kisayansi,na matukio ya utandawazi.

Kusoma vitabu ni muhimu pia kwa kujua au kujifunza lugha mpya,kama kujua maneno yalokuwamo kwenye kurasa. Ambayo huongeza ujuzi wa kuyaongea na kuandika kwa ufasaha.

5. Huongeza kumbukumbu

Pindi unaposoma vitabu,unatakiwa kukumbuka wahusika,asili zao,matamanio yao,historia zao,na pia vitu tofauti tofauti vyenye mahusiano na wahusika kwa kila habari.Kwa mfumo wa kumbukumbu,lakini akili ni kipande cha maajabu ambacho huweza kukumbuka vitu na kukumbuka vitu hivyo vyote na hat mwisho wake vilipoishia. Ni jambo la ajabu ya kutosha,kila kumbukumbu mpya inayoingia katika akili hutengeneza ujuzi,na huzidishaukomavu wa akili,ambayo husaidiwa na mfumo wa muda mfupi wa kumbukumbu na kukomaza kukumbuka hizo hisia.Unaionaje hiyo? Imetulia!  

6. Uwezo wa uchambuzi sahihi

Hivi ushawahi kusoma vitabu vyenye hadithi za kusadikika,na ukapata suluhisho wewe mwenyewe kabla ya kumaliza kusoma? kama hivyo ndivyo,ulikuwa na uwezo wa kuchambua na kudadavua mawazo ukayafanyia kazi kwa kuandikamaelezo yote uliyoyapata na kutengeneza matumaini mapya.

Huo ni sawa na uwezo wa kuchambua ambao mikono yako imemiliki inapokuja haja ya uchambuzi. Kwanza kujua ulokiandika kipo sawa,kama wahusika walihusika vizuri, hadithi ilitiririka vizuri n.k. Ulishawahi pata nafasi ya kusimuliana kitabu na wengine,utakua na uwezo wa kuyachambua maoni yako kwa vizuri,kama uliutumia muda wako vizuri kufuatilia kila ulichokisoma.

7.Huongeza umakini wa uono wa maoni  

Katika  uchizi wa dunia ya mtandao,umakini unapatikana katika milioni ya muelekeo tofauti tofauti kwa wakati mmoja kama tunavyovifanyia kazi nyingi kwa kila siku. Kwa kila dakika tano ya maisha,wastani wa kila mtu hugawanya muda wake katika kafanya kazi,kuangalia barua pepe,kupiga soga yaani kuchat na watu zaidi ya mmoja,(kupitia gchat, skype, whatsaap n.k),macho yote kwenye twitter, kuangalia smartphone, na muingiliano baina na kati ya wafanyakazi wenzake. Hii aina ya tabia husababisha kuongezeka kiwango cha msongo wa mawazo,ambayo hupunguza uzalishaji wetu.

Pindi unaposoma kitabu,akili yako yote inakomaa na hadithi-na vingine vilobakia hupotea au  unavipuuza na utajidhatiti zaidi kujishughulisha na undani wa maelezo unayoyapata kutokea kwenye hadithi. Jaribu kusoma kwa 15-20 dakika kabla ya kazi(i.e asubuhi yako,kama unatumia usafiri wa wote),utashangaa kwa ugunduzi, maarifa na akili kuchangamka ambao uutakuwa umeupata ufikapo kazini.

8.Ujuzi wa kuandika vizuri  

Hii huwa mkono kwa mkono na uelewa mzuri kwa upana wake wa misamiati: Utaalam wa kuweka wazi,kazi nzuri ya maandishi huwa ni matokeo ya mwandishi mwenyewe,kama ugunduzi wa maanguko,mtirirriko,na aina ya uandishi wa baadhi ya waandishi,na utaalamu wa mbinu za uchoraji na utunzi wa waandishi tena wakufunzi waliopita, huwa ni matokeo kwa waandishi wameajifunza kutokea kwa kusoma kazi za wengine.

9. Utulivu

Kwa kuongezea kitabu kitakupa mapumziko au furaha ambayo inapatikana katika kusoma kitabu kizuri,na inawezekana somo unalolisoma likakupa faraja ,matumaini na utulivu wa amani ya nafsi. Kama kusoma vitabu vya imani,hushusha shinikizo la damu yaani blood pressure na hukupa upole aamani na utulivu,na pindi unaposoma vitabu vya sifa ya kutatua matatizo vinavyoonyesha jinsi ya kusaidia watu waliopata tabu katika hali fulani,navyo huleta maumivu ya kuumia.

10.Huburudisha bila ya gharama

Japokuwa wengi wetu tunapenda kununua vitabu na tunasoma na kuwa ndiokumbukumbu zetu za baadae,huweza vikawa bei iko juu. Na kwa kuwa na budget ndogo, au unakosa kabisa kiasi cha kukuwezesha kupata burudani ya vitabu ,unaweza tembelea maktaba ilokaribu na eneo lako au kupitia kwenye maduka na ukapata hata vitatu viwili. Maktaba zina vitabu vya kila aina ya somo uanalofikiria,na utakua unazunguka hifadhi yake utapata hata vipya pia,hautaepuka kuacha kusoma.

Kama itatokea utaishi eneo ambalo halina maktaba,au unaeza ukapata kwingine au hata kwa mtu mwingine kwa urahisi,maktaba nyingi zina vitabu vyake kwenye PDF au ePub kwahiyo unaweza soma kupitia mifumo hiyo,iPad,au compyuta yako.Pia kuna vyanzo vingi kwa njia ya mtandaoni ambapo huweza kupata vitabu vya bure, kwahiyo viwinde hivyo vipya na kisha usome!


Kuna utofauti wa tabia za kusoma kwa kila mtu duniani,na huenda ikawa ukaonja ladha tamu na nzuri
 katika fasihi ya waandishi,utenzi,magazeti ya mitindo,maandiko ya dini,vitabu vya vijana,jinsi ya kutoa msaada,mambo ya mitaani,au vitabu vya kimapenzi,hapo kitakuwepo kinachotaka kwenye akili yako na mawazo yako. Kaa pembeni na kompyuta yako kwa muda,fungua kurasa za vitabu,na ukonge moyo wako kwa wakati mwingine.  

usiache kutembelea blog yetu nayo inaburudisha kuisoma.






























Thursday, May 11, 2023

7 SABABU YA KUWA NA BUSTANI JIKONI

12:35 AM // by Kalma // No comments

 7 HIZI NI SABABU YA KUWA NA BUSTANI

 JIKONI

Kama ulikua unawaza mawazo ya kukuza viungo vyako mwenyewe,ni vizuri ukafanya hivyo! Chagua sehemu karibu na dirisha au balcony ya jikoni au ndani jikoni na upandishe mimea.Hutajutia! hizi ni sababu kwanini bustani za jikoni zitakushangaza.

1. Unapata viungo fresh pale unapohitaji

Mara nyingine unahitaji majani ya mint au basil,

unachuma tu hapo kwenye mmea wako na utaacha kwenda kununua. La kuongezea huhitajiki kununua fungu zima na kulihifadhi kwa mahitaji ya kutumia jani moja.2. Unajua haswa kile unachoweka kwenye chakula chako

Siku hizi,na hizi dawa zinazowekwa kuzuia wadudu,ni ngumu kujua kama chakula ni salama au laa.Kama unakuza au unazalisha mwenyewe,unajua kuwa ya kwamba na kuwa na uhakika kuwa chakula au mboga hizi ni salama na hazina dawa.3. Inakua kazi rahisi

Mimea haina gharama kubwa haswa pale inapokua imetulia,kikubwa kinachohitajika ni maji kidogo.Baada ya muda utatunza fedha yako ile na haitakuwa tena kwa ajili ya kununua  mboga mboga,na haswa pale unapohitaji vyakula vizuri na vilivyo fresh.

4. Unakua ni mwenye afya

Kama unazalisha na kuitunza  mimea kama tulsi na mint,unaweza kuwa unakula jani moja au majani mawili kila siku,au ukaweka kwenye chai ya asubuhi, au ukanogeshea mapishi yako.

Hivi viungo vina faida ya dawa za kutosha ambazo zimo kwa ajili ya kutibu magonjwakama vile changamoto ya upumuaji,inatunza afya ya meno,hutibu homa,asthma,changamoto ya mapafu,ugonjwa wa moyo na stress yaani msongo wa mawazo.

5. Unapata dozi ya utulivu ya kujituliza tena ya kiasili.

Bustani ni ina kazi ya kutuliza na kupunguza au kuondoa kiasi chamsongo wa mawazo na kusaidia  kuwa mwenye kupumzika.Kuzungukwa na mimea asili unatakiwa kuwa na hali ya muonekano mzuri wa afya ya akili, Pamoja na maandiko ya wasomi mengi kuona maajabu kwa ujumla.

6. Mimea hufukuza wadudu/mbuKama unachagua viungo haswa kwa kutulia,inaweza kufukuza mbu kwa kiwango kikubwa,inazuia na kupunguza kung’atwa na mbu na kinga dhidi ya dengue na malaria.

Mmea mzuri kwa kinga ya mbu ni marigold-weka mmea mmoja katika kila mmea wa viungo.Na rangi zake zitang’arisha nyumba yako pia!

7. Hali ya kushangaza

Unaweza kudharau wazo la kupanda mimea,lakini ukianza kukuza ya kwako mwenyewe,

Utajua haswa tunachomaanisha.Kila mpigo mmoja ,branch au maua yanayokuzwa itakupa hali ya kuridhika na kukupatia furaha wakati wote.