• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, November 28, 2013

KUMUOGESHA MTOTO MCHANGA.

9:19 AM // by Kalma // No comments

KUMUOGESHA MTOTO
Watu wengi huogopa kuogesha watoto wachanga,ila ni jambo zuri kama utatoa uoga,ni kweli ina maajabu hivi ,na kama ndio mara yako ya kwanza pia huwa ni ngumu kidogo.
Mazoea ya mila yetu huwa kuna msaidizi pindi mama anapojifungua  na ndo hufanya kazi hizi, ila inaonekana kuanza kuwa ngumu sababu ya ubusy na pirika za maisha kupata mtu wa kuja kukaa na wewe kwa muda.

Isieleweke vibaya,  tabia au mila ya baadhi ya  wanawake wengine  kurudi nyumbani kwao, siishauri sana kwa kipindi cha kujifungua,kwani hupoteza nafasi kubwa ya mume kujua tabu anayopata mke pindi mtoto anapokua mchanga,ni kipindi kizuri cha nyote kufeel hiyo hali na ikibidi mume kutekeleza majukumu mengine.
Na kama italazimika hivyo ni sawa ila kukaa kwako na mume wako na mtoto mchanga ni nzuri zaidi,kwani huongeza mapenzi , kuhurumiana,na kupunguza gharama za kuendesha sehemu mbili kwa muda mmoja..
Kumuogesha mtoto ni kujenga mapenzi baina yenu.Watoto wengi huenjoy kuwekwa kwenyemajimoto,ila wengine huitaji muda kuzoea kwa ngozi yao mpya.

Tumia maji moto,kilo bora zaidi kwako wewe na mtoto mwenyewe.
Fanya haya pindi unapotaka kumuogesha mtoto mchanga :
  • Safisha vitu vyake vya kuogea kama sinki,au beseni ,siku hizi kuna yale special kama bafu hivi,lolote lile au kile, la msingi ulisafishe kwanza.  
  • Tayarisha sabuni,maji moto ya uvguvugu,mafuta,lotion,taulo,nguo za kuvaa kama vest,diaper,nguo yenyewe,socksi,kofia,gloves kwa maeneo ya baridi,nepi,pini ya nepi,baby shoo au blanketi la kumfunikia,n.k.   
  •  
     



  • Osha mikono yako vizuri.
  • Hakikisha chumba hakina baridi,funga madirisha na milango au shusha pazia hutegemeana na hali ya hewa ya sehemu husika.
  • Tia maji ya uvuguvugu kwenye sehemu ya kumuogeshea kama sinki,beseni n.k, kipimo yafunike mabega ya mtoto ukimweka,13cm(5in).
  • Weka maji ya kumsuuzia kwenye chombo kingine pembeni.
  • Mvue nguo zote na umsafishe kama amepuu au kukojoa,umfunge kwenye taulo safi hadi sehemu ya kumuogeshea.
  • Muweke ndani ya beseni ukiwa umemshikilia kichwani na mkono wa kushoto umeegemeza shingoni kwake,asiwe amekaa, awe amelala ila shingo na kichwa viko juu ,ukiwa umemshikilia kwa nyuma,yaani mgongoni.
  • Mwagie maji yakinge kwa mkono wako wa kulia, ni mtoto mdogo yasiwe mengi ,anzia kichwani upande wa uso ukiwa kama unampangusa.
  • Kisha mpakae sabuni kuanzia mabegani ,kushuka mikononi na mpaka miguuni.Inashauriwa kumuogesha mtoto mchanga bila sabuni kuepusha allergy,na sabuni iwe isio na harufu na sio ya urembo,tumia sabuni za watoto.
  • Msuuze kwa maji safi yaso na sabuni yalo pembeni kwenye chombo mpaka sabuni ziishe ,nayo yawe ya uvuguvugu.
  • Kisha msafishe uso yaani mpanguse macho,na kona za pua kama unamkandakanda hivi  na maji kidogo.
  • Mfute kwa taulo safi na kavu,mfunike kwa dakikia 10 kupunguza baridi,kumletea joto mwilini,tumia blanketi.
  • Mpakae mafuta au lotion ukianzia maeneo ya mgongoni huku ukimkandakanda,na sehemu nyingine.
  • Mvalishe nguo safi na mkunjie blanketi.
  • Mkiss kwenye paji la uso wake.
  • Watoto wengi huchukua muda mfupi wakioga ni kulala.
Naamini  we mama pia utakua tayari umeoga na umekula vizuri ,huo utakua muda wako mzuri wa kumnyonyesha mtoto alale vizuri.
TIPS:
  • Usimuache mtoto mwenyewe kwenye maji hata kwa chembe dakika.
  • Pendelea kumkanda viungo mtoto baada ya kuoga.
  • Huweza tumia moto kumkandia kusaidia kupunguza gesi tumboni(colic).weka moto kidogo kwenye chetezo weka mikono yako juu ya ule moto ,itakua yamoto mkande au mmasage mgongoni  na mwili mzima kwa kumnyoosha viungo pia.
  • Baada ya kutoka jua la asubuhi ni muda mzuri wa kumuogesha,huwa hakuna baridi sana.
  • Pendelea kumfanyia zoezi kwa kumkanda,ukiwa umem-beba kupunguza gesi na kumuondolea uoga mtoto.
  • Piga pasi nguo za mtoto kabla ya kuvaa husaidia kuua vijidudu.
  • Nguo za mtoto zisichanganywe na nguo za wengine.
  • Hakikisha nguo za mtoto hazilali kambani nje,anua tu pindi zikaukapo.Husaidia kupunguza wadudu. 

Tuesday, November 26, 2013

KUONDOA CHUNUSI.

9:27 AM // by Kalma // 2 comments

CHUNUSI
Chunusi au Pimples ni aina ya doa au madoa yanayosababishwa na mafuta ya ziada yaliyokuwa trapped katika vinywelea.Nyingine ni Postules au Papules.Chunusi huweza tokea usoni,mabegani kifuani na hata mgongoni.
Chunusi  hutibika  kwa aina ya dawa za kuondoa makovu ambazo zimependekezwa na wataalamu,na hata kwa kununua za maduka ya dawa au urembo,kwa mtazamo wa kujitibu.

SABABISHI:
Ndani ya vinywelea kuna Sebaceous gland,ambayo inazalisha “Sebum”.Pindi layer ya nje ya ngozi inapoziba,seli ya ngozi zilokufa au kuisha, nyuma kushoto hufanya kuganda kama gundi na huganda na sebum.
Hii husababisha vinywelea kujifunga,na sana sana pindi pale ngozi inaposinyaa kama ya “kwapani”.Sebaceous glands huzalisha Sebum nyingi ambazo hujenga nyuma juu ya pale palipoziba,na hii  njia ya Sebum kuna kuwa na bacteria wakiwemo kama Propionibacterium acnes,husababisha madhara na kuungua ambayo huitwa chunusi.

TIBA ;
MADAWA YANAYOAGIZWA
Kuna cream kwa ajili ya kutibu chunusi.
Dawa ya kawaida inayotibu na inayojulikana kwa chunusi ni Benzoyl Peroxide na Salicylic Acid na antibacterial kama Triclosan,zote hizo ni aina ya dawa hupatikana kwa mfumo wa cream na gel na hutumika kwa kupakaa.Husaidia kutoa chunusi kwenye ngozi kwa haraka na hulainisha ngozi pia.Huondoa bacteria kwa haraka.Kabla ya kupakaa unatakiwa uoshe uso au sehemu husika kwa maji ya uvuguvugu na ukisha ukaushe na taulo safi.
Cleanser huweza tumika kuoshea kwa nia ya kupakaa dawa.
Rosecea hii sio kwa ajili ya madhara yatokanayo na bacteria.Madhara yalosababishwa na bacteria hutumika Tretinoin.

Kusafisha uso kuwa safi na kupakaa  cream yatosha kuwa tiba nzuri ya chunusi japo sio ya kudumu.
Aina ya kawaida na nzuri zaidi ni Benzoyl Peroxide,ina hatari ya ngozi kidogo huweza sababisha allergy.
Kwa sasa Nicotinamide hupakaliwa kwa kipindi imeonyesha kutibu zaidi kwa chunusi kuliko antibiotics kama Clindamycin.
Nicotinamide (VitaminB3)sio antibiotics na haina madhara pia.Ina faida ya kupunguza Hyperpigmentation ambayo  ni kisababishi cha chunusi.

DAWA(PRESCRIPTION  MEDICATION).
Dawa nyingine hulazimika kuandikiwa na watalam kwa tiba ya chunusi.Nayo ni Isotretinoin ambayo ni Retinoid.
Historia yake ni antibiotics kama Tetracyclin na Erthromycin zimetajwa.Nazo zilikuwa zinatibu zaidi kushinda Benzoyl Peroxide,Bacteria walikuwa sugu na ikashindwa kupambana nao .Na antibiotics zinaonekana zina madhara zaidi kuliko cream  mfano wa kuumiza tumbo,huweza kubadili rangi ya meno,zile antibiotics ziloelezwa na Dermatologist na wakashauri ni Doxycycline na Minocycline.Kwa ajili ya kuondoa  chunusi kwa mara moja.
Walishauri pia Accutane ambayo ilikuwa nzuri kwa kutibu chunusi nayo. Hii Accutane huweza sababisha madhara kama kutapika,kuharisha na matatizo ya uzazi kwa wanawake.

TIBA YA USAFI(HYGIENE).
Tumia njia hii mara kwa mara ;osha ngozi ilioathirika na chunusi,tumia natural cleanser,husaidia kupunguza seli za ngozi zilokufa na muingiliano wa bacteria ambazo ni sababu ya chunusi.
Japokuwa sio kama ndo inaweza kuondoa kabisa chunusi ila hupunguza kasi ya chunusi kuendelea na kuenea na hata kuzuia pia.
Chunusi ni ngumu kutoka na huchukua muda mrefu.Madawa yametengenezewa na madawa ambayo sio nzuuri kwa ngozi.Tumia njia hizi za asili zifuatazo;

CHUMVI(SEA SALT).
  • ·         Chumvi ina detoxifying qualities hufanya kazi nzuri ya kukausha na kuondoa chunusi na madoa pia.
  • ·         Chukua vijiko (3)vya chai vya chumvi weka ndani ya bakuli.
  • ·         1/2kikombe cha maji ya moto yalochemka sana,tia ndani ya bakuli uloweka chumvi.
  • ·         Changanya na koroga pamoja tumia kijiti cha cotton buds .
  • ·         Chukua upande wa kijiti hiko kina pamba kitakua kimelowa na maji yale .
  • ·         Kisha weka kwenye chunusi au doa na shilkilia  kwa dakika 10-20.
  • ·         Unaweza fanya mara mbili kwa siku mpaka chunusi zikauke.
  • ·         Unaweza tumia kitambaa kuwekea kwenye chunusi zilojikusanya sehemu moja nyingi.

BAKING SODA.
  • ·         Osha uso tumia cleanser au sabuni ya uso.
  • ·         Vijiko vya chai (8)vya baking soda weka kwenye chombo.
  • ·         Tia maji kwenye  chombo uloweka baking soda.
  • ·         Koroga vizuri,iwe laini na uji uji yani isiwe nyepesi wala nzito sana iwe creamy.
  • ·         Pakaa mchanganyiko huo katika chunusi .
  • ·         Subiri kwa dakika 15 mpaka ikauke.
  • ·         Osha na maji ya uvuguvugu.
  • ·         Fanya hivi kwa wiki mara mbili(2)mpaka chunusi zipotee au kukauka.
  • ·         Ikiwa uso utakuwa mkavu sana fanya mara moja(1)kwa wiki.ngozi ikianza kukauka zaidi  ni bora upate ushauri wa daktari. 
  •          Kumbuka kukauka kwa ngozi ni kawaida sababu chunusi husababishwa na mafuta yalozidi kwenye ngozi.

NJIA NYINGINE YA KUONDOA CHUNUSI NYUMBANI KWAKO.

Barafu(ice)
1.       Husaidia katika mzunguko wa damu katika sehemu iloathirika,huondoa uchafu na mafuta yalolundikana kwenye ngozi.
2.       Weka barafu kwenye kitambaa kisha weka sehemu ilo chunusi kwa dakika chache hivi kama unakanda.

Ndimu
1.       Ina Vitamin C,husaidia kukausha chunusi.
2.       Loweka kitambaa kwenye maji ya ndimu ilokamuliwa,kisha pakaa,fanya hivyo kabla ya kulala waeza osha asubuhi au kuosha baada ya nusu saa.Hakikisha unatumia ndimu ilo fresh ndio nzuri zaidi.


Asali
1.       Hii ina antibiotics na huzuia madhara ya bacteria,pakaa asali acha kwa nusu saa kisha osha na maji ya uvuguvugu .
2.       Fanya hivi mara mbili kwa siku.

Dawa ya meno
1.       Wakati unapiga mswaki asubuhi na jioni pakaa dawa hii pia kisha osha uso kwa maji ya uvuguvugu,na unaweza kulala nayo ukaosha asubuhi .
Steam
1.       Weka maji kwenye bakuli maji ya uvuguvugu kisha jifunuke na taulo kichwani ukiwa umeinamisha uso kwenye bakuli hili la maji kwa dakika 10-20.
Kitunguu thoum(garlic)
1.       Hii ni antifungal,antiviral,antiseptic,na ina sulfur pia.visage sugulia kwenye chunusi acha kwa dakika 5 kisha osha uso na maji ya uvguvugu .Hata kula inasaidia kupurify damu,ila usile sana ina madhara tumboni.

Peppermint
1.       Maji ya majani yake ukiweza yapata ,yasugulie au pakaa maji hayo kwa dakika (10).Osha uso kwa maji baridi.Hii ina antibacterial na antiviral.


Tango
1.       Ni antioxidant,ina Potassium,Vitamin A,C,n E.Loweka vipande vya tango kwenye maji kwa saa moja (1hr)virutubisho  kama VitaminA, Potassium na Chlorophyll vitaingia kwenye maji.Chuja maji na kunywa maji yake,au tumia kuoshea uso.

2.       Unaweza tumia kama mask.
3.       Saga tango moja kisha pakaa usoni kwa dakika(15)ikauke.kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.

Papai
1.       Ni antioxidant,Vitamin A,hulainisha ngozi tumia kwa kupakaa kwenye chunusi.






JINSI YA KUSAFISHA LAPTOP.

7:08 AM // by Kalma // 1 comment

JINSI YA KUSAFISHA LAPTOP
Hivi lini ilikuwa mwisho wa kusafisha laptop yako? je keys za laptop yako zimeanza kugoma?laptop yako mpya imeanza kuonekana kama ya zamani?
Kwa kukaa tu kwenye desk laptop yako huwa chafu,sikwambii zinazozunguka katika siti za magari.Vumbi hujikusanya ndani ya laptop na sana sana kwenye feni.Huilazimisha feni kuzunguka zaidi ambayo hatari yake ni kuiruhusu kupata moto husababisha hata kufa .
Ni vizuri kuishi maisha ya raha na yenye afya na yakipendezeshwa na laptop yako safiii…
Fuatilia njia hizi huenda ikatatua huo uchafu wa laptop yako.
Tafuta dawa ya kusafishia-kwenye screen au kioo inabidi utumie “screen cleaner”.Kwa sehemu 
nyingine  chukua  bakuli tia sabuni kiasi,na Isopropyl alcohol.


Changanya mchanganyiko huo.
Kisha tumia
Chupa zile za kupulizia dawa ambazo zina mfuniko wa kupulizia.
Zima compyuta yako na toa betri-usisafishe wakati unatumia.
Toa mouse,disc,cd’s,Usb,waya na chochote kilichochomekwa.
Chukua ile dawa pulizia,kuondoa uchafu.

Kama uchafu uko mwingi unaweza chukua kisu ukatoa keys kwa uangalifu,waeza haribu connector, au kuumia wewe mwenye .
Weka bakuli la maji na sabuni kidogo,tia vile vikasha vya keys ndani ya maji hayo kwa muda kubanduka yale mauchafu yalogandia.Ukisugua tumia mkono au mswaki au brush ndogo ,tumia mswaki ambao hautumiki.
Tia bakuli nyingine maji ya uvguvugu na nusu kipimo cha Isopropyl alcohol.loweka kitambaa kidogo kwenye huo mchanganyiko ,kamua maji yasichuruzikie kwenye laptop.tumia kufutia ndani ya keyboards na uso wa laptop sio screen,ieleweke hapoo.

Safisha katika mikunjo ya laptop tumia ule mchanganyiko wa kupulizia mpaka isafishike vizuri.
Iache laptop kwenye hewa ipate kukauka.Usifunge mfuniko wa laptop. Kama ulitoa keys tokea keyboards anza kuzifuta kwa  kitambaa kikavu.


Anza kurudishia keys kwenye keyboards ukiwa una uhakika mashine yako imekauka vizuri.
Tumia dawa maalum kupangusia screen.Pulizia kisha futa na kitambaa kikavu.Hii iwe hatua ya mwisho katika usafi wako sababu isipate uchafu tena,pindi usafishapo sehemu nyingine.
Usitumie sabuni za kawaida huweza haribu screen yako au kupunguza performance yake,na hata uzuri wa mng’ao wa screen yako.
TIPS
Weka chakula mbali na laptop yako.Osha mikono kabla ya kutumia laptop yako .Kama utatoa keys,hakikisha unajua kurudishia,Tumia keyboard nyingine kugelezea kurudishia keys au print copy yake ili upate picha kamili ya keyboard ya laptop yako.Fanya hivyo kila unapotaka safisha laptop yako.

Pata kinywaji ukipendacho baada ya usafi huo na furahia usafi huo kwani umekusaidia kupunguza stress na umeinjoy piaUsiache kutembelea blog yetu ndani ya mtandao kujifunza mengi na mazuri zaidi.

Sunday, November 17, 2013

LUNCH AT MANAL .

10:32 AM // by Kalma // 1 comment

Hayawi hayawi hatimaye yamekua.Aso na mwana aeleke jiwe!.
    Ndani ya Manal mida ya mchana hivi,wasiwasi mkubwa wa wingu lilotanda mawinguni kuashiria haina muda mrefu kunyesha .Bado haikuwa kikwazo kwa wana Manal kushindwa kulifikia hili,la kufanikisha sherehe ya kula pamoja ya kumpongeza mteja wao alotunikiwa shahada yake siku hiyo ya tarehe 16/11/2013.
 Mnamo saa nne majira ya asubuhi baada ya kukata tamaa na ubusy wa kila mpishi kuwa na oda kumshinda mwenziwe na sehemu zote kuonekana kulishakodiwa rasmi kwa ajili ya kusherehekea baada ya matukio ya graduation.
  Mteja wetu huyu juu na kuchelewa kwake kutoa oda ya nafasi hapa manal,Manal haikumkatisha tamaa ndani ya saa moja ilitimiza hayo utayojionea mwenyewe bila chenga.

   Wageni kuchukua nafasi zao hapa Manal .Huku maandalizi ya chakula yakiendelea.





















 wageni na jamaa wakiendelea kujisevia chakula.










 juisi ya mchanganyiko wa choyaa hiyooo....















 wasiliana nasi kwa sherehe yeyote,karibu sana Manal na tutakufikia ulipo.