• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, September 23, 2021

Water cooler

11:37 PM // by Kalma // No comments

Water cooler
Safisha water cooler kwa maji safi na crisp

Ili kuyafurahia ladha ya maji kwa chupa zetu,kusafisha water cooler na kuitunza ni jukumu letu kuu.Mara zote kuhakikisha maji ni masafi na kifaa hicho ni kisafi ili kujilinda na mazalio ya bacteria mbalimbali.
Jinsi ya kusafisha

 Ondoa chupa iliyoisha maji kwenye cooler 
  Toa kifuniko kama vipo na kifaa chochote kinachotoka kutegemeana na cooler yako.
    Tia 1 kikombe vinegar na 3 vikombe vya maji moto.Tumia kitambaa safi ,safisha ndani ya sehemu inayokaa chupa ya maji.

  Utamwaga maji hayo kupitia mabomba kwenye cooler.Safisha kwa sabuni ya jikoni ya kuua vijidudu na bacteria.kama bomba zinatoka utaosha kama vyombo kawaida.
 Suuza,tumia maji safi na salama mara mbili kwa kufungua bomba za cooler .
Rudishia vifaa ulivyotoa na weka chupa ya maji safi,na chomeka kwenye umeme
Kama umefatisha mpangilio huo cooler yako itakua safi,na umechukua jukumu la kuitunza vyema kiafya na kunywa maji salama.
Wasiliana na wakala wa cooler kwa usafi na marekebisho zaidi.
Inashauriwa kila baada ya miezi sita uifanyie usafi wa kina wa ndani na nje wa cooler yako.

  

Monday, September 13, 2021

Ufumbuzi wakati wa kuoka

12:25 AM // by Kalma // No comments

Ufumbuzi wakati wa kuoka

Epuka haya matatizo ya kuoka

Na haraka tafuta suluhisho inavyowezekana.

Kuna ajali nyingi ambazo zinaweza kutatuliwa pamoja na whipped cream au smear au frosting pia.

Tumezielezea baadhi ya matatizo ya kuoka ambayo unaweza kuyaepuka na vyovyote iwavyo basi rekebisha.

Cookies zilizoungua chiniCookies zinaweza kuungua kwa dakika tu. Chagua sheet za uhakika za kuokea(nyembamba na nyepesi ni nzuri,)toa macho yote kwa cookies wakati wa kuoka haswa reki ya kati. Kama cookies zako zinakuwa za brown kati,basi weka kati kati whipped cream,ice cream au frosting.Kama zimekua muonekano wa kuungua,kata juu ipendezeshe kwa kuipamba juu au katikati weka layer ya ice cream- nani hapendi cookies na cream?

Cake nzitoCake huwa ni delicate-ukichanganya kwa mdogo mdogo,Changanya Pamoja mahitaji tu  yachanganyike vizuri na cake yako itakuwa nyepesi,na itapumua vizuri kwenye oven.Kuchanganya sana inasababisha kuganda,inaleta uzito usiotakikana.Kama cake yako ni leaden,kata kata vipande na loweka kwa syrups au shira nyepesi,whipped cream au liquer kuifanya kuwa moisten.

Cake iliyonywea/iliyojirudi.Tunajua cake zina harufu nzuri,usifungue mlango mpaka iive kabisa;punguza temperature ya jiko,itasababisha keki kunywea.Badala yake ,tumia oven thermometer na haraka chomeka kijiti au toothpick kati kuangalia kama imewiva kwa ndani mpaka chini.Acha cake yako ipoe vizuri kuepusha mabadiliko ya hali ya hewa.Kwa bahati nzuri,keki iliyonywea au iliyorudi bado itakuletea matokeo ya makofi kwa wageni wako.

Pie ya ukoko iliyoungua Kama pie yako inaonekana kuungua yaani imekua rangi ya brown sana mapema tu,funika na tin foil au pie crust protector.Kwa pie ambayo inatoka jikoni kati imeiva vizuri lakini nchani au pembeni imeungua,yaani hapo kwangua ukoko au palipoungua.Kama uzuri wa ncha unaweza kukwanguliwa, huna haja ya kupambia na ladha za kuficha kuungua.Pie yako bado itaonekana nzuri na ladha nzuri kama kawaida tu!

Runny FrostingMaji mengi inapelekea kuleta hali ya kutepeta.Changanya zaidi na confectioners sukari -au cocoa powder kama ni chocolate-mpaka frosting iwe nzito.Iweke kwa friji kama jikoni kwako kuna joto.Kwa keki za layer,frost layer na uiweke frijini mpaka hapo kabla ya kuifrost kwa upande wa nje.

Cake iliyopasuka juu au pie iliyotengeneza ukoko

Keki iliyopata ufa inamaanisha ukandaji wako wa unga/donge ilikua mgumu sana.Kwa pie: Ongeza maji kiasi kwa unga au donge la pie yako  au futa na brush kwa maji kabla ya kuweka frijini au kuikunja.Kata madonge zaidi kwa maumbo mbalimbali pembeni;itakuwa rahisi kuucover ufa wowote kwa aina yoyote na mapambo.Kwa cake:Changanya maji kidogo kwa unga/donge uliyokuwa mgumu.Cake mara nyingi huwa nzuri ikiwa frosting au whipped cream kwa vyovyote,kwa hiyo,tengenezea au pipe na cement.

Cake au Cookies zilizopasuka Kulundika keki kwenye oven iliyopata moto sana husababisha keki au cookies kuvunjuika au kupasuka.Usiruhusu sufuria zako kushika au kuweka hata kama inch moja upande na karibu sana na jiko.Wakati mikono mizuri inapasua kilichookwa vizuri.Tumia  ujanja!Kata keki iliyopasuka au kata vipande pande alafu iwekee layer ya matunda,au pudding,ice cream au whipped cream na iweke kwenye friji ijiachie.Mwishowe imewezekana,lakini desert tamu na ya uhakika.

Enjoy and Share!.


 

 

Sunday, September 5, 2021

Sababu ya kula tangawizi kila siku

11:56 PM // by Kalma // No comments

 Sababu ya kula tangawizi kila siku

  Tumesikia mara nyingi kwamba Tangawizi ni aina ya chakula bora.Ina fiber za kutosha,Vitamini ndo usiseme ni antibiotics za asili na matumizi mengi ambayo mwili wetu unaweza kutumia na ukapata faida.Lakini si kila mtu anapenda ladha ya tangawizi,na hatuitumii sana kwenye vyakula vyetu.Tumeweka sababu kumi kwanini utumie miujiza ya mboga hii kila siku.
Anza na chai ya tangawiziTanagawizi ni kiungo chenye ladha kali chenyewe,lakini ni nzuri kwenye chai.Ni nzuri kwa kuongeza nguvu asubuhi,na hupambana na flu,Ina boost mfumo wa kinga za mwili na ni tamu na yenye afya.

Inapambana na migren

Ushawahi kupata maumivu makali ya kichwa,hakuna dawa yaeza saidia?Huenda ikawa ni migren,lakini tangawizi inaleta nafuu kwa maumivu hayo.

Kupambana na Distention

Kupambana na chango,au baada ya mlo wa mchana au usiku ukaanza kusikia maumivu ya chango la hedhi.Wengi tumejisikia hivyo kawaida sana  lakini tangawizi ni nzuri pia kupunguza hisia za maumivu hayo.

Inapambana na maumivu ya viungo vya mwiliMaumivu ya viungo yaweza kusababisha kuwa mgonjwa kila leo yakiwa serious.Na kweli,daktari wako anatakiwa akushauri kitu,lakini hata hivyo,tangawizi haiwezi kudhuru na ni nzuri kwa maumivu kama haya.

Maumivu ya hedhi?Hayapo tena!]Kuna dawa tele za kupambana na maumivu ya hedhi lakini kama hupendi kumeza dawa kama mimi,unatakiwa kuzingatia kujaribu tangawizi.Itapunguza maumivu na kusaidia kujisikia vizuri.

kukinga na ugonjwa wa kisukari

Kuna aina ya gonjwa la sukari ambayo huweza kumtokea yoyote katika maisha kama hawatakula kiafya na kutofanya mazoezi.Tangawizi huweza kulinda hilo,lakini kiukweli haitoshi kufidia aina ya maisha .

kipindi cha mafua?sio kwako!Tumetaja kuwa kunywa chai ya tangawizi hutengeneza kinga za mwili wako kuwa imara zaidi,lakini kipindi cha mafua,yaweza kuwa kiokoa maisha.Unataka kuachana na ugonjwa huu wa wiki ?Kunywa chai ya tangawizi basi.

Supu Pamoja na tangawiziHatujataja mibadala ya kutosha jinsi ya upishi wa ladha ya tangawizi,lakini hii mifano.Tengeneza supu ya mboga mboga au kuku(inanoga na chochote)halafu sagia tangawizi ndani yake.

Tumia tangawizi kama kiungoKimsingi,unaweza tumia tangawizi kama kiungo.Untengeneza rosti la nyama?Nyunyiza tangawizi ndani yake na huwa ni nzuri zaidi.Tumia kama chachandu pia,Hakikisha hautumii nyingi.Ladha yake ni nzuri na yenye hadhi kubwa mno.

Hulinda moyo wako

Kula tangawizi mara kwa mara kikawaida hulinda vijidudu shambulizi kwenye moyo na hukinga vijidudu kwenye mzunguko wa damu.

Unaweza kuzidisha kuila zaidi kama kuna kesi za maradhi ya moyo ndani ya familia yako kabla.

      Enjoy na Share !