• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Saturday, April 29, 2017

Jikoni

5:32 AM // by Kalma // No comments

Jikoni  
Vyumba vyote nyumbani kwangu,jikoni kunasafishwa  mara kwa mara na umakini zaidi,ni sehemu ngumu kusafisha kwa sababu ina sehemu nyingi,kwasababu  ndio panapotokea chakula chetu na kinyume chake,kama hapakutakata pataleta madhara kwa afya.
Ni sehemu ambayo vijidudu hatarishi huzalishwa hii ndio hatari kubwa.Nitakua pamoja kwa usafi wa jikoni kwa kutumia madawa asilia tafadhali tuwe pamoja na mimi, dawa,utupie zako comments ! 
Kabati(Cabinets)
Nyumbani kwangu makabati yanashika chakula,alama za vidole,na michoro ya uchafu kadhaa,kiukweli huumiza kusafisha.Nimekua muathirika wa microfiber na maji  kusafishia,lakini suluhisho kubwa natumia t-shirt zilochakaa na taulo.

Counters na meza
Vitambaa ni kufutia mezani na juu ya counters.Hutumika kwa granite na formika na haiachi uchafu wala mabaki ya kitaambaa.Sishauri kutumia dawa maalum za kusafishia granite .Usitumie vinegar,ndimu au limau,au mfano wa asidi huchakaza na husababisha kunywea au kulika au kutoboa mawe.Unaweza kutumia vilevi vilotengenezwa nyumbani sio kiwandani nayo sio kila siku hii ni kwa kusaidia kung’arisha na kuondoa uchafu sugu.
Sakafu(Floor)
Hutegemeana na aina ya sakafu ulokua nayo,aina ya usafishaji utatofautiana pia,lakini aina yoyote ya sakafu inaweza kusafishwa kiasili.kwa laminate, ceramic, etc., mchanganyiko wa kikombe kimoja cha vinegar katika galoni ya  maji kwa kutumia dekio patasafishika vizuri sana.
Marumaru na grout,mwagia baking soda nyunyizia  hydrogen peroxide acha kwa dakika chache kabla ya kusugua na kufuta.Hii ni kwa ajili ya grout kuwa nyeupe.
Napendelea kutumia microfiber sana nafanya mpango kutafuta dekio au microfiber mop mbeleni,lakini kwa sasa nasafisha kwa dekio la mkono.
Dishwashing
Kwa sabuni asilia ya vyombo,natumia citron.Nimejaribu za asili za kutengeneza nyumbani ila sijapata mfano wa citron kwakua ni chaguo zuri kwangu,unaeza ukatumia yoyote nzuri unayoipenda wewe.Mfano Dr. Bronner’s Liquid Castille au Dishwashing Liquid from Tropical Traditions ni za asili pia.
Kusafisha dishwasher yenyewe,unatia bakuli moja au mbili juu ya shelf ya dishwasher upande wa kulia white vinegar.Kisha unawasha kama kawaida kukiwa hakuna vyombo lakini, hii huondoa sabuni zilogandia na hufanya dishwasher kufanya kazi vizuri.Hii ifanyike kwa mwezi mara moja.

Oven
Nasafisha mwenyewe oven kwa kunyunyizia maji ndani na pembeni na kumwagia baking soda kidogo  ½ au ¼ inch,naongeza maji kupata uzito mfano wa uji ,naliacha usiku mzima.Asubuhi ,unakwangua ile baking soda ambayo itakua rangi ya brown kwa uchafu kwa kutumia brush ya wire kusugua uchafu sugu na madoa .Baada ya baking soda yote kuisha napangusa na maji yalochanganywa na vinegar kwa mng’ao na usafi .
Nimegundua njia nyepesi ya kusafisha oven kwa dakika 15 tu!

La kuhifadhia taka
Natumia ndoo zaidi ya taka na hua natafuta zenye kuvutia nzuri.Hapa kuna njia mbili;
Kata kipande cha ndimu au limau,sugulia doo hilo na usuuze na maji ya kuchuruzika kwa sekunde 10.  Kugandisha maganda ya  ndimu na chungwa katika tray za barafu na vinegar au maji tumia kusafishia kwa dakika 10
Koroga ½ kikombe cha baking soda na 1kikombe cha white vinegar acha kwa muda wa 10 dakika kabla ya kusuuza na maji au kufuta na disposal.

Vifaa vya kuoshea
Jinsi ya kuosha inategemea ni aina ya wapi na ipi.Kwa matumizi ya vifaa vya bustani husafishwa na maji kwanza kabla ya kutumia kifaa.Kwa vitu vya store vigumu,hivi hulowekwa kwanza na vinegar kwa dakika 10,husuguliwa kwa mikono tu wakati kifaa cha kuoshea kikilowekwa na baking soda.
Chini ya sink
Panasafishwa na vifaa vya jikoni tu.Chini ya sink,chupa ya white vinegar,hydrogen peroxide,baking soda,na kamia soap,kitambaa aina ya microfiber na brush kwa ajili ya kusugua.Ondoa vitu chini ya sink na usafishe kwa urahisi.

Checklist ya usafi wa jikoni
Leo,tuone jinsi ya kuwa na jiko safi!Ondoa dawa zenye madawa na acha kuzitumia!!jipangie ratiba ya kusafisha jiko lako kila muda mara kwa mara kwa kuwa safi siku zote.

Be Hygienic and Smart !

Saturday, April 15, 2017

Usafi asilia wa chooni

2:23 AM // by Kalma // No comments

Usafi asilia wa chooni
 Dondoo
Kingine zaidi ya jiko ni ,usafi wa chooni huchukua muda mwingi na kazi sio ndogo sababu ina sehemu nyingi tofauti tofauti,ni asili yake,ni sehemu inayotaka sana usafi sababu kunatumika mara kwa mara.
Kama uko kama mimi ,lazma na utapenda kazi ya kusafisha choo.Kwa bahati nzuri mpangilio na madawa asilia yatakurahisishia kufanya haraka na vizuri chooni mwako.
 kioo
 Ni kama dirisha,unaweza kusafisha kwa mchanganyiko wa maji na vinegar katika chupa yako ya kupuliza kwa kutumia kitambaa au karatasi. Njia rahisi tumia microfiber cloth,kilowane na kingine kikavu.Au kimoja kilowane na kingine kikavu bila ya kutumia dawa aina yoyote,kwa kila usafishapo.
Counters, marumaru(tile), mabomba ya kuogea (shower),beseni la kuogea(tub)


Kama unavo hivo apo ,unaweza tumia kitambaa hicho kwa vyote.Pia ni nzuri kama utatumia kwa vibebea sabuni.
Nusu kwa nusu vinegar na maji itasafisha maru maru,counters,uso wa makabati,na vibebea sabuni
Mchanganyiko wa baking soda na maji utasafisha uchafu uloganda kwa shower na beseni la kuogea.(tumia vinegar bila maji kwa kutu na uchafu maradufu)
Kwa grout mwaga baking soda na nyunyizia hydrogen peroxide tumia mswaki kusugulia.

 Kwa kutu au uchafu mkubwa zaidi kwa tiles na tub,hizi dawa asilia husafisha vizuri sana lakini haishauriwi kutumia mara kwa mara
 Kwa maru maru za ukutani,milango ilopakaliwa rangi,madoa milangoni,nje ya choo,n.k,hizi dawa za asili husafisha vizuri zaidi.
 vyooMara moja kwa wiki,mwagia baking soda ndani ya choo igande,kisha tia kikombe kimoja cha white vinegar ndani ya maji humo kwa choo.Tumia brush nzuri ya kusugulia choo utaona madoa,kutu na harufu imekwisha kabisa.
Hii pia inatumika chini hata nje ya choo kuondoa harufu mbaya chooni. Nimegundua harufu ya mikojo ni mbaya sana(haswa kwa watoto wanaojifunza kutumia poti) na inajificha katika mikato ya choo cha kukaa hata kile cha aina nyingine ,juu ya mfuniko wa kufunikia choo na pembe za mikato.Nyumbani kwangu usafi huu hufanya kila baada ya wiki mbili .
 Namalizia kuosha choo kwa kupulizia manukato na kufuta chini kwa hydrogen peroxide.
 Manukato( Air Freshening)
 Kuna aina nyingi ya manukato sio nzuri kwa afya na haswaa kwa watoto huweza kuleta madhara,mfano kama Febreeze and Lysol spray zina dawa kali.Kunukiza chooni bila ya sumu hemu jaribu hizi za asili.
 Hizi mbili ziko njiani zitafanya nyumba yako na choo chako kunukia kiasili zaidi,hupunguza gharama za dawa na hulinda afya ya familia yako siku zote.

 Tuambie jinsi gani unasafisha choo chako? tupia maoni yako sasa!

Thursday, April 13, 2017

Kusafisha dirisha la aluminium

6:30 AM // by Kalma // 1 comment

Kusafisha dirisha la aluminium
Kama nyumba yako ina vioo vya aluminium hua ni sababu ya kubeba vumbi na hewa chafu kama havisafishwi ipasavyo.Kwa bahati nzuri,kwa vifaa vichache,vinaweza takata na kunga’aa kwa muda mfupi.
Futa vumbi kwenye fremu ya madirisha
Kabla kusafisha fremu za dirisha,unachotakiwa kufuta vumbi eneo zote kwenye reli za dirisha ,nyavu na vioo vya dirisha zenyewe.Tumia kitambaa cha vumbi,au fagio dogo la manyoa la kuondoa vumbi.Tumia kifa kinachoendana na aina ya dirisha lako,fagia au futa vizuri hadi vumbi lote liishe.
Changanya dawa ya kusafishia  
Ushafuta vumbi na zimeisha,sasa changanya dawa na maji ndani ya chupa ya kupulizia,1/4 ya kikombe ya window cleaner au sabuni ya kusafishia ya maji na kikombe cha maji ya uvuguvugu.Changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutikisa chupa hadi ichanganyike vizuri .Mwishowe,chukua chupa tia maji ya vuguvugu.Huu mchanganyiko utatumika kusuuzia mwishoni ule mchanganyiko wa sabuni.

Tumia mchanganyiko wa sabuni
Ule mchanganyiko wa sabuni na maji ,pulizia kwa madirisha yako machafu iache kwa 1-3 dakika.Kisha,tumia kitambaa cha vumbi kufutia uchafu.Hakikisha dirisha limetakata,suuza na maji ya uvuguvugu na ufute na kitambaa safi kikavu kwa kukaushia.
Tip
Tumia gazeti au karatasi safi kwa mng’ao wa kioo cha dirisha.

Wednesday, April 12, 2017

Kupanga dressing table

5:27 AM // by Kalma // No comments

Kupanga dressing table
Dressing table inavurugika sana kwa sababu ni mahala pakuhifadhia vitu vidogo dogo vingi,kama vipodozi,dawa,vipambio,urembo wa dhahabu,silver n.k.Hata hivyo,dressing table bado inatakiwa iwe safi mara zote na imepangika vizuri ili iwe rahisi kupata vitu pindi utumiapo
 Tips:
Toa au tupa vipodozi vyote visivyotumika.
Hii husababisha dressing table kuwa imejaa na vurugu.Unafikiri kuwa manukato au perfumes,lotions,na vichupa mbali mbali huonekana vizuri .Achilia mbali mawazo hayo,usifikiri hivyo.Unatakiwa utupe vyote visivyotumika kuleta muonekano mzuri na wa kuvutia kwa dressing table yako.Na vile vile utapata nafasi ya kutosha kwa ajili ya vingine muhimu na vipya.
 
Panga kulingana na aina
Jingine,panga vitu kwa makundi kwenye dressing table.Tofautisha mapambo,dawa,mkoba wa huduma ya kwanza,na urembo.Weka powder ya usoni,foundation, lipstick, mascara, eyebrow pencil,na vipambio vingine kundi lake kwasababu hutumika wakati.Kwa hiyo,unatakiwa uwe na mkebe wa kubebea vipodozi kuhifadhi humo.Hata dhahabu,silver na mapambo ya vito na mengineyo yakae kwenye mkebe wake.Hapo utaweka lotion, night cream, sunblock,na vingine vinavyofanana na hivi.Kingine,utazipanga perfume kwa usafi mzuri.Kama una aina ya manukato tofauti tofauti kwa mfano ya usiku na mchana nayo utayawekea kwa makundi yake halikadhalika udi n.k.





Kumbukumbu za upangaji
Kitu gani unatumia sana kwa dressing table yako?Utasema ni vya kujipambia,mashanuo na vitana,lotions, perfumes,na jeweleries. Hta dawa hutumika pale unaposikia maumivu.Hifadhi kwenye droo vile visivyotumika mara kwa mara na weka sehemu ya karibu vile vinavyotumika kila mara ili kuvipata kwa urahisi.




Pendelea kupanga dressing table mara tu inapovurugika .

Tutumie dressing table yako tushare pamoja!

Wednesday, April 5, 2017

Faida 5 za pazia chumbani

4:37 AM // by Kalma // No comments

MAPAZIA 

Pazia chumbani kwako huongeza mvuto kwa apartment.Unaweza kushangazwa labda ni upotevu wa muda na hela kuweka pazia chumbani kwako,usiache kuangalia faida zinazopatikana,usikose nafasi adhiim ya kuwa na pazia chumbani kwako kwa mvuto na muonekano wa kupendeza.
Hizi ni faida za pazia chumbani:
1. LINEN HUDHIBITI JOTO

Pazia aina ya linen hufaa kwa chumba chochote nyumbani kwako,lakini zaidi ni chumbani cha kulala(bedroom).Pazai ya Linen ni laini yaani soft,yenye muonekano wa kifahari.Ni nzito na hufanya kazi ngumu kuliko muonekano wake.Huleta baridi kipindi cha joto na joto kipindi cha baridi.Kama ni mpenzi wa aina nyingine basi Linen liwe chaguo lako.Haina madhara ya aina yoyote.
2. FARAGHA
Kama una majirani wenye tabia ya kuchungulia ndani ya nyumba yako ,pazia huzia hilo.Hakikisha pazia za chumbani kwako sio nyepesi hazionyeshi.Kununua pazia  kubwa zaidi ya dirisha lako,kuepusha kuonekana kupitia pembe za dirisha.
3. VUMBI
Huzuia vumbi kuingia chumbani .Pazia huchukua vumbi kutokea sehemu karibu na eneo lenye vumbi .Hii itazuia vumbi kupenya na kusambaa ndani.Kumbuka kufua na kukung’uta pazia mara kwa mara,zina tabia ya kushika vumbi sana.
4.KUDHIBITI MWANGA
Kuwa na pazia chumbani hudhibiti mwanga.Kwa mchana ukiacha wazi pazia itaingiza mwanga halisi wa jua,haina haja ya kutumia taa.Kama huitaji mwanga,utazifunga.Hii ina tija pindi utumiapo compyuta au ukiangalia sinema.
Kama huoni vizuri screen kwasababu jua linaangazia sana usoni,fungua pazia vizuri zitaleta giza.Kwa upande mwingine,chagua pazia zenye rangi tulivu huleta mwangaza usiku,hata kwa taa yenye mwanga hafifu.Njia nyingine,pazia husaidia kupunguza matumizi ya umeme. 
5.DESTURI YA PAZIA
Pazia ina desturi nyingi.Hupatikana kwa muonekano wa rangi na mapambo tofauti  mbalimbali.Kama una mandhari fulani ya chumba chako ,unachagua kulingana na hilo.Kwa mfano,unanunua pazia zenye kuendana na rangi ya chumba chako.
Kuwa na pazia chumbani ni faida kubwa kimazingira na muonekano wa uzuri.Pazia hua hazilingani kwa kila mmoja ni tofauti kutokana na mapendekezo ya kila mtu.Kuna aina nyingi tofauti za pazia la msingi ni chaguo la moyo wako.

Unapenda pazia za chumbani kwako?tuambie ni za aina gani,rangi je?

Share and Enjoy !

Kusafisha Oven haijawahi kusafishwa(na ukafanikiwa)

4:07 AM // by Kalma // No comments

Kusafisha Oven haijawahi kusafishwa(na ukafanikiwa)

Hii iko serious hivi muda huu 10:30 usiku oven lako limerowekwa na baking soda,racks za oven zimelowekwa kwa bathtub,birika la chai (buli) linatokota maji moto kwa kusafishia juu ya oven,na mumeo kapiga magoti hahaha…nimecheka apo!anasafisha sakafu kwa sponji kwa sababu unagundua muda umeenda na huna dekio au tambara la usafi (mop).(kiukweli ningemwambia aache!)

Tunaita  usafi wa kina(deep cleaning),
Sakamia ikianza hii,hairudi nyuma.
Tukifanya usafi tunapendelea njia za kisasa zaidi kuboresha kazi yetu.Sakamia hatu
tumii madawa makali sana,tumejifunza ni Baking soda kwa kusafishia oven.
Koroga uji wa baking soda na maji pakaa kwenye oven yako.Iache kwa usiku mzima.Unasafisha uji ulioganda kwa kupangusa na maji.Halafu,pulizia vinegar kumalizia uchafu wa baking soda. Futa vizuri.
Muhimu: 
Ufunguo muhimu wa kuitumia baking soda,pindi unaposafisha oven,unapaswa kuipa muda ili ifanye kazi.Kusubiri kwa saa 12 au usiku mzima ndio tiketi yake.
Asubuhi yake unasugua ndani tumia sponji,halafu futa kwa kitambaa safi laini.Muda huo unapulizia vinegar kwa kitambaa unachopangusia mpaka uchafu wa baking soda uishe wote.Utaona rangi ya kijivu na brown yote imeondoka ,na sehemu zote zikibaki safi na mng’ao wa kuvutia.
Mlango wa oven
Baada ya kuloweka na baking soda,nakusugua kutoa uchafu,hapa unaangalia kama oven yako inatoka kioo utatoa utasafisha  hakikisha pameng’aa.
Racks:
Zinafurahia kulowekwa kwa beseni la kuogea(bath tub)!sio lazima beseni najua utaniuliza la kwangu lipo chumbani inakuaje?unaloweka kwa sabuni ya kuoshea vyombo.
Muhimu:
 kama umeamua kusafishia kwenye beseni hakikisha unaweka kitambaa wakati unaziloweka la sivyo zitachubua bathtub.
Tumia sabuni kwa kuzisugua vizuri hadi ziwe kama mpya.
Juu ya jiko (Stovetop):
Tumia maji ya uvuguvugu kuloweka zile chuma za kupikia kukata mafuta.Tia sabuni kali acha kwa 15-20 dakika,kabla ya kusugua.
Unaweza tumia dishwasher(mashine ya kuoshea vyombo)lakini bado haitakatishi sana.Niambie mdau wangu we ni njia gani hutumia zikang’aa?Utendelea kusugua na kufuta kwa kitambaa kisafi laini.
Mwishowe,ni sakafu yaani floor :
Ni safi! Mshukuru aliyekusaidia mumeo,msaidizi n.k amesugua kwa sponji,hao ni wale wakupendao.
Una ratiba gani ya usafi wa kina kwako?
   Sakamia Cleaners
Be hygienic and smart!!