• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, October 30, 2013

ASALI (chakula cha afya duniani).

1:38 AM // by Kalma // No comments

ASALINi ya ajabu yenye rangi ya dhahabu.Hupatikana ndani ya mwaka mzima kila siku.

 Ni chakula kitamu cha nyuki hutumia nectar kutokea kwenye maua.Aina ya Apis ndo hujulikana zaidi.Hukusanywa na wafuga nyuki,na hutumika sana kwa binaadamu.

 Asali inayotengenezwa na wadudu wengine hiyo ina matumizi tofauti. 

Nyuki wanatengeneza asali kwa njia ya uchavushaji(regurgitation)na uvukizi(evaporation).wanaihifadhi katika mizinga ya nyuki.

Ni tamu hulinganishwa na sukari tena huzidi hata hiyo sukari yenyewe.Bacteria wengine hawazaliwi kwenye asali sababu ya maji yako 0.6, kuna bacteria Clostridium Botulimum nae ni hatari kwa watoto wachanga.Ina madhara kwa ukuaji wa Intestinal tracts,hupelekea kuumwa sana hata kifo wakati mwingine.

Asali ina historia kwa binaadamu hutumika kwa vyakula na vinywaji,kuongezea ladha na utamu.Huaminika kidini.

Asali ni dawa.Asali ziko tofauti kulingana na grade na chanzo cha  nectar iliopatikania na maua pia.Ina sukari ya asili dehydrated ambayo hukinga na fermentation.

Hutengenezwa na nyuki kama chakula cha kwao wenyewe sana sana kipindi cha baridi kali na kipindi chakula fresh kikipungua maana yake maua na vyanzo vingine vya vyakula vyao hao nyuki,au hakipatikani,nyuki hutumia asali kama chanzo cha nguvu.


Kuna nyuki wanawake ambao ni Queen,kuna nyuki wanaume,na kuna wanaume wa msimu hawa ni kwa ajili ya fertilization kwa Queen wapya. Wanawake ndo wachapakazi 20,000-40,000.
 Muonekano wa asali unatofauti hutegemeana na maji yalokuwemo,na aina ya flora ilotumika kutengenezea,hali ya hewa,na portion ya sukari iliokuwemo.
Fresh honey ina liquid,maji, sukari nyingi na maji huyeyuka kutegemea hali ya hewa iliopo.Ina Fructose na Glucose.
Egypt wanatumia asali kwa kuongeza ladha ya cake na biskuti, na vyakula vyao vingi hupendelea kutoelea asali .

        Asali imetajwa kwenye uislam sana katika Qur-an na kuna surah inaitwa An-Nahl(the bee).Na ipo Hadith ya Mtume Muhammad(S.A.W) amesema Asali hutuliza maumivu ya magonjwa.
Na Qur-an inasisitiza asali ni kirutubisho cha chakula chenye afya. Qur-an(16:68-69)Jewish wao asali kama ishara ya mwaka mpya na huliwa zaidi siku hiyo,wanakula kwa kuzamisha apples kwenye asali na kuutakia mwaka kuwa mtamu . Asali hupikiwa,hutumika kuokea,kupakaa kwenye mkate na nyongeza kwenye vinywaji. Kama chai, vilevi kama honey wine,or honey beer.

Asali ina mchanganyiko wa sukari na vingi virutubisho.Ina Carbohydrates,Fructose(38.5%),Glucose(31.0%).Asali hubaki na Carbohydrates  yenye Maltose na Sucrose na madini pia.Achilia utamu wake ina Vitamin na madini ya kutosha.
Ina fanya kazi ya Antioxidants, ikiwemo Chysin,Pinobanksin,Vitamin C,Catalase na Pinocembrin. Hutegemea na mmea ulozalisha asali yenyewe.


   Kuna asali ya maua na ya kutengenezwa,bali zote hutokea kwa maua.
Asali ni kitu pekee chakula cha afya na dawa pia,asali huweza kihifadhiwa kwa muda wa mwaka na hata karne, kwa kutegemeana na humidity iliyopo.

          Hutibu magonjwa
Gastric inayopelekea ulcers.Vidonda na kuungua.Antiseptic na antibacterial.MRSA infections.Kulainisha koo na kutuliza kikohozi.Hutoa rushes .Huondoa na kupunguza allergies.Hupunguza high cholesterol.

Mtoto chini ya mwaka haishauriwi kupewa asali sababu ya Botulism iliopo huweza leta madhara katika mfumo wa  digestion. Asali ina sumu endapo italiwa kabla haijatengenezwa inasababisha Kizunguzungu,uchovu,kutapika na nausea.Pia kwa mbali huweza sababisha presha,shock na mapigo ya moyo yasiyo kawaida sio sana nayo hii kutokea,very rare.Sumu hupatikana sana msitu Tutu kwa vine Happer insect huko Newzealand.Sumu yao inaitwa Tutin ipo kwenye asali. Ni kutokula hii aina ya asali na dalili zake ni kutapika,kuweweseka,kizunguzungu,coma n.k.

   
Nchi inayoongoza kuvuna asali ni China,Uturuki na Ukraine.Tanzania Tabora wanashika namba kwa kuvuna asali wakifuatiwa na wengine Singida,kigoma,n.k.
   
Tips ya kuiandaa asali na kupikia.

Kama asali yako imeganda.chukua chombo tia maji moto na kisha weka asali yako kwa dakika 15 itayeyuka.Usiipashe asali kwenye microwave.Tumia asali ikiwa kama kimiminika .Huwa nzuri ikiwekwa badala ya sukari.Katika kupikia tumia 25F sababu asali mara moja kufanya chakula kibadili rangi kuwa brown na hata kuungua.

      FURAHIA ASALI .

Tumia asali mezani kama sukari kwa chai. Chovyea apple kwenye asali.Weka kwenye maziwa ya mgando kama sukari.Sandwich nzuri inayopendwa na watoto ni ile yenye Peanut butter,ndizi na asali."MILK DRINK" Chemshia maziwa ya soya,asali na dark chocolate ambayo sio tamu,kwa moto mdogo.

Urembo wa asili wa uso na ngozi huwezi ukaiacha asali,hutumika kwa kupakaa usoni na hata kujisugulia mwilini.Chukua pumba laini changanya na asali msugulie bi harusi mtarajiwa kwa muda wa wiki nzima mara moja hata mbili,afanye waxing na apakae hinna.



Tuesday, October 29, 2013

KOME/MAKASHA (mussels or clams)

7:10 AM // by Kalma // No comments

KOME

Kome ni anajulikana kwa jina lingine kasha ni kitoweo kinopatikana kwa maji ya bahari au freshwater maji yaso chumvi.Ni kitoweo kwa matumizi ya familia na makazi ya watu wa pwani zaidi.
       Kome wanagamba wenyewe wako ndani.
Kome ni tofauti na chaza,wao ni wakubwa wakati chaza ni wadogo.
Chaza kwa kizungu ni Oyster na kome ni Mussels au clams.
      Neno "mussels"hutumika kumaanisha chakula kwa familia za mabaharia.
Kome wana gamba la rangi ya blue ilokooza,nyeusi,au brown,wenyewe wana rangi ya silver hivi .
    Freshwater ni kama Ziwa,Mto,vijito,maji ya mifereji.
Kome wanakula plankton na viumbe visivoonekana katika bahari ambao wanazama kwenye maji.
Wanapatikana milimani mwa maji.
        Wako jinsia ya kike na kiume.Fertilization yao hutokea nje ya mwili wao,huwa wana larvae kuanzia wiki tatu hadi sita.
       Kome hawa wanaliwa na binaadamu,samaki kama starfish,ndege wa baharini,na dogwhelk anapatikana baharini pia.
    Kome wa freshwater wanaliwa na Otters,raccons,ducks,na baboons wa Coast South Afrika na geese.
Sana sana hutumika kama chakula.
    Italy huchanganya na samaki wengine kwa chakula na wanapendelea wa kuchemsha na wanatia ndimu.
   Ufaransa wao hupatikana kwa jina la Eclade des moules wanawakausha na haswaa Biscay beach bay.
  Huweza kuliwa mchuzi kwa wali na supu pia
India hutumia kwa mkate kama tunda la mkate na mboga mboga pia.Na hutengeneza kwa nazi kama mchuzi kwa wali na viungo na pilipili.
         Kome anaweza kuchomwa,kukaangwa,berbeque,steam,kwa siagi au mafuta na mboga .
Wanatakiwa wawe hai kabla ya kupikwa.wana sumu ila huisha kwa kupikwa .na huchemshwa sana na kisha kumwagwa maji.
Hufunguka maganda wanavopikwa .Unaweza kuwapasua gamba na kuwatoa ila ni rahisi kujikata na kisu na hutumia muda kuwaandaa,kwahiyo rahisi  kuwachemsha na maganda yatatoka yenyewe.
        Ni chakula chenye thamani japokuwa ni rahisi. Kupatikana kwenye baharini na majini.
   Wanafaida za kiafya za kutosha wanacalories,Protein,Carbohydrates,fiber,fat na sodium.Ni sauce ya selenium na Vitamin B12. Na Zinc na Folate.
    Ni chakula chenye afya kwa mlaji ,na kwa familia pia.
Hufananishwa na nyama nyekundu.Na ni tamu ladha yake.
Chakula chenye afya bora ni chenye mchanganyiko wa virutubisho viloanzia 10-20% katika mlo kwa siku katika mwili wa binadamu. Na kome akiwemo.
       Kome ana fatty acids za kutosha zenye faida ambazo hujenga akili na hupunguza inflamatory conditions.
        Hujenga na kuboost immunities imara tokea kwa Vitamin na madini zinc.
         Huongeza nguvu za kiume ,kama utatumia mbichi kwa yule mwenye tatizo hili,au ya kuchemsha,ya kukaanga haishauriwi kutibu tatizo hili.

                   Jinsi ya kutengeneza mchuzi wa kome.

Baada ya kuwachemsha na kumwaga maji ukawatoa magamba.
      Unachukua mafuta ya kupikia unaweka ndani ya sufuria,kitunguu kimoja cha maji kilichokatwa,viungo vya fish masala,au kitunguu thom kijiko cha chai kimoja na tangawizi kijiko kimoja cha chai,tui zito kikombe kimoja .
Nyanya moja iloosaagwa au kukatwa vipande vidogo,na tomato paste au tomato mkebe kijiko cha chakula kimoja.
       Kaanga vitunguu viwe na rangi ya brown weka nyanya na ufunike kwa dakika kumi kisha tia viungo na tomato paste iache ichemke kwa dakika saba hadi kumi hakikisha vinaiva na kukaangika vizuri kama maji yatapungua utakua unaongeza kidogo dogo.
          Tia kome wako changanya na viungo vichanganyike vizuri kwa kukoroga,kisha tia tui na ulikoroge kwa dakika tano liive.

Nzuri kula kwa wali au kwa kutoelea chapati au mkate.
Ni tamu na nzuri kwa afya ya familia yako.

Monday, October 28, 2013

MATUMIZI YA CHUMVI

1:13 AM // by Kalma // No comments

CHUMVIChumvi ina Sodium Chloride.Ni chemical ambayo ina wingi wa ionic salts.Ni asili hutokea wenye milima au halite.

Ni kwa maisha ya wanyama. Saltiness ni kwa ajili ya ladha kwa binadamu.Romania walikua wakichemsha maji wakapata chumvi enzi hizoo.Ilikuwa ikisafirishwa kibiashara wakitumia boti na kwa bahari za Mediterania kwa barabara za chumvi,kupitia sahara wakiwa wamebeba  Camel caravans.Hutumika kwa sherehe za kidini,viwandani,na kitamaduni.

Afrika ilitumika South Sahara.Na sana sana ilitumika kwa chakula .Wanyama wana tissue zina chumvi kwenye nyama,maziwa,na damu.Matunda na mboga pia vina chumvi ya asili ila kidogo.East Asia wanatumia chumvi ambayo ipo kwenye Soy sauce,fish sauce,na Oyester.Huwa zina sodium  nyingi kwenye hizo sauce.Hutumia sana kwenye kupikia kuliko kuongezea juu ya chakula .Chumvi ina madhara ikizidi mwilini.Chumvi ni kitu kikuu kwenye diet.Huweza sababisha blood pressure,ugonjwa wa moyo na stroke,ikizidi mwilini.

Chumvi ya mezani iko 40% uzito wa Sodium,6g(kijiko kimoja cha chai ina sodium 2300gms.Husaidia nerves na mishipa kufanya kazi vizuri. Ina fanya mzunguko wa maji vizuri mwilini ina balansisha fluid.Mlo mzuri hunogeshwa na chumvi ambayo ina sodium.


Tabia ya western countries ni kutumia chumvi 10g kwa siku,iko juu kipimo chake ukilinganisha na Eastern Europe na Asia.
Ni vizuri kupunguza kula chumvi hata cardiovascular disease husababishwa na chumvi nyingi,kwa watu wazima na watoto,japo athari haionekani hapo hapo.Chumvi hushauriwa kula 200gms ya Sodium kwa sikuChumvi hutumika kwa mimea na wanyama.Matumizi ya viwandani ni 68% na sodium chloride ndo inayotumika sana,kwa kupata Caustic soda na chlorine,hutenganishwa na electrolysis.Hutengenezea Pvc,Plastic,Paper pulps.Hutumika kama Flux kutengenezea Aluminium. Chumvi hutengenezea sabuni ,glycerine.Synthetic rubber,kurushia mfinyanzi,na ceramic materials hutumika chumvi kutengenezea.Wakati wa kuchimba chumvi yale mabaki yanayobakia kwenye mchanga na changarawe,hutumika chumvi kwenye matope kujenga ukuta imara kuepusha shimo kujifunika au kuvunjika.Chumvi hiii hutumika kama mordant kwa vitambaa vilokwisha kwa kutengenezea resini kwa kulainishia maji kwa ngozi pia. Chumvi hutumika kuhifadhia, chakula kama nyama,samaki visiharibike kwa muda mrefu.

Wanaoongoza kwa kuchimba chumvi duniani ni kule Khewra salt mine kipo Pakistani.wana sehemu ya kuhifadhia 19,wakati 11 zipo underground km 400 kwa mls 250. 2002 jumla ya chumvi ilivunwa duiani ilikuwa tani 210 milioni,U.S wakiongoza,wakafuatia. China,Germani,India na canada kwenye kumi bora hizo.

 2003-2008  uzalishaji uliongezeka kwa 12% kwa mwaka na China ilishika namba kwa uzalishaji wa viwandani. Chumvi hutumika kwa dini pia.Angalia hii; Hadithi ya sunan Ibn Majah alimsikia Mtume(s.a.w)akisema "chumvi ni master wa chakula chenu ,mungu ameteremsha tokea mbinguni "Moto,Maji,Chuma,na Chumvi".Wahindi wanatumia kipindi cha harusi,na Brahmanic wao hutupia chumvi kwenye moto kipindi cha kutoka mwezi mpya na hupiga kelele kama kuongeza imani na kufurahia. Chumvi ni dawa kwa jino,kutuliza maumivu ya fizi,kung'atwa kwa mbu,koo,na kidonda,kuungua,na kukandia mwili.Kwa kusukutua na maji moto,waeza kupigia mswaki kwa meno yanayotoa damu,na kuweka kwenye kidonda kukata damu. Chumvi hutumika kwa usafi kutoa kutu,vyombo vya mafuta,kusafishia friji,madoa,kupunguza rangi kwa nguo inayochuja,na kutofautisha rangi isichanganyike kwenye nguo,na kusafishia copper.Chumvi hupunguza matunda na mboga kuleta rangi ya brown kama apple au bilinganya,hata viazi n.k.Chumvi huondoa uchafu mikononi ukiwa umetumia vitunguu na thom,utomvu na kusugulia vyombo vya stainless steel hung'aa. Kuzuia wadudu wasiingie ndani kama utamwaga kwenye eneo kama inzi,mende n.k.Chakula kisicho chumvi huwa hakina ladha nzuri ila ikizidi huwa karaha nayo. Chumvi iliwe kwa kiasi na ladha ya chakula.

     

































Friday, October 25, 2013

KUONDOA MADOA,(ACNE)MWILINI.

5:02 AM // by Kalma // 1 comment

Uko tayari na hiyo siku yenyewe,ushajipanga mwenyewe tarehe tayari,job interview,wedding day,ukijiangalia usoni una pimples,madoa au mabaka .Si majanga hayo?  Doa au kovu madoa hutokea kwa wakubwa 95%.Hakuna tofauti kati ya Spot na acne,kwa kiswahili ipo ila humo humo.

Doa ni mvunjiko wa ngozi,wakati acne huenea mwili mzima.Huweza tokea usoni,kifuani,mgongoni,begani na Buttocks.

        Doa ni kuziba kwa tezi karibu na uso wa ngozi uitwao Sebaceous gland.Hizi tezi huzibwa na Sebum ambazo ni mafuta yaliyozidi yakichanganyika na cells mfu za kwenye ngozi wakati wa kufunguka kwa tezi. Matokeo yake ndio Chunusi.


     Na kama sehemu iliyoziba kuna Bacteria wanaishi katika uso wa ngozi na wanasababisha wekundu,kuvimba hutokana na level ya hormones na hutoa white pus,kutokea kwa whiteheads.

 Doa pia huweza sababishwa na kubadilika kwa hormones kipindi cha Balehe au kuvunja ungo,ujauzito,na mijengeko imara iliosababishwa na Stress tokea mfumuko wa hormones.
     Na haswa mihangaiko ya shughuli za siku kubwa kama harusi,interview n.k.
    Ukishakuwa na madoa sehemu ya mwili ni budi kuyatibu.

Tuwe pamoja tukishuhudia hizi tiba;

Anza kwa Dermatologist,mtaalam wa ngozi kukupatia sababu ya hizo doa, na atakupa ufumbuzi tu ye si mtaalam banaa.

Kuna Antibiotics na dawa yenye Benzoyl Peroxide,inakausha na hutibu sehemu iliyoharibika kwenye ngozi.

         Kujitibu kwa vitu vya asili ni rahisi na gharama ndogo.ukizingatia vitu vya asili vinakufanya uwe mrembo na mwenye afya nzuri .

          Majani ya chai ya mafuta 

Ni antibacterial na anti-inflamatory,kwa kupakaa kwenye doa .Changanya na maji kwanza.

          Rose waterIna anti-inflamatory na aroma za kwenye rose huacha spirits na huondoa haraka stress na tension.

Kama unasumbuliwa na doa mdomoni na kidevuni ni vizuri kumuona mtaalam kwa ushauri.Na kama ni mwanamke kutakuwa kuna walakini hapoo,na huenda ikawa Polycystic Ovary Syndrome.
         Osha uso kwa kumwagia maji mbele ya uso.yaani jimwagie tumia shawa kama kuflash hivi.Hii husaidia kusuuza uchafu.
       KUJIFUKIZA

Chemsha maji weka kwenye bakuli na jifunike na taulo ukiwa umeweka uso karibu na bakuli. Kama mini sauna,kwa dakika  10 kisha osha uso kwa maji baridi,kufunga vinywelea kulinda na bacteria.

           Exfoliate

Clearis,Freederm,na tumia kusafishia asubuhi na jioni.Cream-Sudocrem,nayo husaidia pakaa usiku kucha,zipo madukani. Maganda ya ndizi weka kwenye doa kwa dk 10-15.Ndizi mbivu ilioiva.Kunywa maji kwa wingi huondoa uchafu.Badili Snacks kwa matunda.Tumia dawa kama iko mbaya T-ZONE SPOT ZAPPING STICK pakaa usoni au mwilini kwenye madoa .
           Punguza make-up.

Tumia product zenye Azelaic Acid ina antibacterial  hupunguza wekundu,hata mwenye rangi nyeusi wekundu upo sema hauonekani, na kuungua,na hupatikana kiasili tokea ngano na shayiri (barley).
           Baking sodaChanganya na maji na gandisha kwenye madoa usiku kucha osha asubuhi .

Aspirin tablets Changanya na maji ongezea Zit kupunguza kuvimba na wekundu.

Tumia dawa ya meno

kukausha chunusi,madoa .

Olive Oil 

Pakaa usoni na hata kwingine kwenye madoa kwa dakika 15 osha au oga kwa maji ya uvuguvugu.

Saga tango na OatmealTango husafisha madoa meusi,na Oatmeal hulainisha ngozi pakaa kwa dakika 15-20.

Pakaa asali.Toa kiini cha yai piga ute wa mayai mawili pakaa mpaka ikauke ,igande kabisa tumia maji ya vuguvugu.

Tumia Lavender,rosemary,thyme,sandalwood mafuta yake.

Usikamue chunusi au doa mwilini na haswa ikiwa hakina kichwa huweza kuongeza bacteria ndani ya ngozi.
      Ulakini wa usafi wa mkono pia sio vizuri kukamua,na ikibidi tumia tissue kuepusha kujiumiza na kucha.weka majani ya chai ya mafuta pale ulipokamua kama antiseptic cream kwa usafi zaidi.
   
Barafu nzuri kwa palipovimba ila inaweza sabaisha kuungua.
Usitumie steamer kwa usiku tatu mfululizo hufanya ngozi iwe kavu.

Kwa mabadiliko yoyote baada ya tiba yoyote yasiyo ya kawaida! haraka ondoa au acha kutumia na osha kwa maji baridi au moto yote poa tu.

Mask ya uso fanya mara 2-3 kwa wiki kwa dakika 15-20 hukausha ngozi kwa ngozi ya mafuta na husafisha vinywelea.Ngozi ya mafuta huathiriwa zaidi na madoa na chunusi na vitu kama hivyo.

   Tiba hizo tumia sehemu yoyote ya mwili haina madhara.Muone daktari mtaalamu kwa matumizi ya dawa .Hii ni supplements usitumie bila kumuona daktari.

Mama mjamzito hashauriwi kutumia dawa bila ushauri wa daktari.










Wednesday, October 23, 2013

MATUMIZI YA HENNA(HINA )

10:09 AM // by Kalma // No comments

MATUMIZI YA HENNALawsonia Inermis ni jina lingine la henna. Jina la Henna yenyewe asili yake ni lugha ya kiarabu lenye maana ya Dye.
 Hutumika kwa ngozi, nywele, na kucha.Hutumika kwa Hariri,Pamba,na Leather.Henna ilitumika kama urembo Egypt, North Afrika,na waarabu wa Peninsula na South Asia. Ilitumika sana Pakistani ,India na Afrika.
Siku hizi kuna sherehe ya henna maarufu Bridal henna night, ni kimila flani hivi ila imekua ya kisasa zaidi .Huuzwa ikiwa kama unga wa kijani, huchanganywa na maji ya ndimu, chai kali,na tayari kupakaa.Henna hutumika urembo kwa wanawake,hutumika dawa ya asili,na hutumika kwa tatoo.

Wanaume hupendelea kupakaa kwenye nywele na ndevu hii iko sana kwa wasomali kwenye nywele .

  Na wazee kuondoa ile rangi ya mvi kwenye nywele.

Henna ya kwenye nywele inaweza changanywa na Cassia Obovata kwa kuleta blond color, mafuta na waxes na metal salts ikichanganywa na chemical treatments.

Huchanganywa na maji moto pia.Henna hutumika sana kwa urembo haswaa wa kujipakaa kwa sherehe tofauti tofauti,japo mwanzoni ilionekana kwa bi harusi zaidi na fetility celebrations.

Ilianza kwa Baal na Anath kwa sherehe ya kupokea waume zao.

              India wanaamini Henna aloipaka bi harusi ikichelewa kutoka huashiria ndoa ya furaha na kupendwa na in-laws, na ikiwahi kutoka maana yake ndoa haitakua na furaha.
Ukaona sababu ya kuikoleza henna ikolee sana ili isitoke haraka.


              Saudia Arabia  wao kule bi harusi anapakaliwa henna na ndugu yake wa karibu mwenye ndoa ya furaha la si hivyo atamletea ishara mbaya ya ndoa.

Somalia henna huvaliwa na wanawake mikononi kipindi cha harusi,Eid,Ramadhani n.k.


                Tunisia wanasherehekea  henna kwa siku saba .Siku ya tatu bi harusi anavaa nguo za mila huku akipakaliwa henna mikononi na miguuni. Kwa mwanaume bwana harusi anapakaa pinky finger siku ya sita.


               Tanzania kote hutumika kwa urembo wa bi harusi, nywele,Eid, na kupakaa kwa aliyeolewa kama urembo kwa mume wake na sana sana pande za pwani.kwa wale ambao bado kuolewa hupakaa kidogo tu tena siku maalum, kama sherehe n.k.
   
Henna hutumika kuondoa kuungua kwa ngozi ilosababishwa na jua na athletes foot.
     Henna hutumika kwa tatoo na iko salama sababu hutumika henna ya asili ile ya majani.

Majani ya henna yanatumika kutengenezea henna ambayo ni dawa ya kuzuia kuharisha kunakotokana na parasites(ameoba),cancer ,kupanuka kwa wengu(enlarged spleen),maumivu ya kichwa,homa za manjano,na ngozi.
Siku hizi hutibu tumbo na maradhi ya ulcers.


      Henna hupunguza m-ba kwenye nywele,eczema,mapele,fangasi,na vidonda.
Hutumika kwa kunywa ilo chemshwa na kupakaa ilochemshwa pia.

      Henna ina madhara kutokana na dawa wanazochanganyia siku hizi kama kuvimba na kuungua mfano wa malengelenge.


Kama henna ya tatoo hutumika black henna hii huwekwa PPD ambayo ina kama mfano wa lami ambayo haiko salama kwa ngozi.
Huleta madhara kama vipele kwa ngozi,kuunguza,makovu,blistering,n.k.
   
    Ni vizuri kutumia henna ya asili  yaani ya majani kuepusha hizo rubsha zote.

                JINSI YA KUPAKAA HENNA KICHWANI.
Kupakaa henna sio kama kupakaa rangi nyingine za nywele au kushika pizza sauce na meat balls.Nywele zikiwa refu na kazi huwa ngumu kidogo ila hupendezesha nywele sana.
         Pakaa vaseline sehemu za usoni karibu na nywele.husaidia kutopata doa vya rangi.Unaweza kupakaa henna kwa nywele kavu au zilolowa ila nzuri zaidi kwa nywele kavu.

Vaa taulo shingoni au nguo mbaya mbaya. Vaa gloves kisha kata mistari mapande manne ya nywele.Pakaa henna kuanzia chini yaani kwenye ngozi nakupanda juu.Anzia fungu la nyuma na huwa rahisi .Ziache kwa saa 2-4,ukizidisha muda nayo hukolea zaidiKulala nayo usiku kucha ni nzuri ukiwa umevaa kofia ili usichafue shuka.Osha vizuri kwa shampoo unayotumia. Hakikisha henna imeisha vizuri kwenye nywele.

Ya kuzingatia;Pangusa haraka endapo imedondokea kwa ngozi tumia maji na vaseline .Osha conditioner badala ya shampoo.Henna hukolea zaidi siku za mbele. Hudumu kwa muda wa mwezi na kuendelea.Changanya Indigo baada ya kupakaa henna kwa brown color.Pakaa mafuta muda wa usiku tumia Mastard oil ni mazuri kwa kukolezea rangi ya hennaTumia henna baada ya miezi sita kama ulitumia chemicals kwa nywele zako mfano relaxer,au rangi nyingine.Henna hutumika kama dhahabu kwa wale ambao hawana uwezo wa kuvaa dhahabu mikononi.