10 FAIDA ZA KUSOMA KILA SIKU
Lini ilikua mwisho kusoma kitabu,au gazeti,au maandiko yoyote?Je una tabia ya kusoma kila siku kwenye mitandao ya kijamii yaani Tweets,Facebook,au maelekezo katika vitu unavyotumia?Kama ni mmoja wapo ambaye husomi kila mara,kwa hali hiyo unakosa mambo mengi: kusoma kuna faida nyingi sana , na nyingine hizi zifuatazo hapo chini.
1. Kuistua akili
Wasomi wengi wameonyesha kwamba mara
zote akili ikiwa inafanya kazi ina uwezekano mkubwa wa kulinda na ugonjwa wa Alzheimer na shida ya akili kitaalamu unaitwa Dementia, kufanya ubongo wako kua hai na huulinda usipunguze nguvu.Na hufanya kazi kama
misuli mingine mwilini,akili inahitaji mazoezi ili iwe yenye nguvu na yenye
afya.Ni sawa na kucheza michezo mingi kama mchezo wa bao unaochezwa kuanzia watu wawili, ni mchezo ambao husaidia kuifanya akili kuwa yenye nguvu.
2. Huondoa msongo wa mawazo
Haijalishi una msongo wa mawazo wa kiasi gani inaweza kuwa kazini,katika mahusiano yako binafsi,au katika mambo ya maisha yako ya kila
siku,la kufanya ni kutupilia mbali ikiwa utazubaa kwenye hadithi nzuri.Kitabuni au
riwaya iloandikwa vizuri itakusafirisha kukupeleka kwingine kabisa,wakati hicho
unachokisoma kitakufanya uwe katika hali iliomo humo kwa muda huo,huondoa
wasiwasi na uoga na kitabu kitakupumzisha .
3.
Maarifa
Kila unachokisoma kinaleta habari
mpya kichwani mwako,na huwezi jua kipi kitakuja mkononi mwako.Kuwa na maarifa
mengi ,ndio kuwa na uwezo wa kupambana na changamoto zinazokukabili.
Kwa kuongezea zaidi,hiki ni chakula cha
kukifikiria: ushawahi kukutana na hali ngumu,kumbuka yote hayo yanaweza
yakapotea –kama hela ,kazi,nguvu,afya,lakini tisa kumi maarifa uliyokuwa nayo hayawezi
potea na hubaki milele.
4.
Upanuzi wa misamiati
Hii huendana na hiyo nukta ya hapo juu: unaposoma sana,ndivyo unajua misamiati mingi,na huwa ni maneno unayaotumia
kila siku.Kujua misamiati mingi na kuongea kwa ufasaha ni msaada mkubwa katika
taaluma yoyote,na tambua kwamba unaweza kuzungumza vizuri na ujasiri wote wa
hali ya juu na itaongeza kujiamini na thamani yako kupanda pia.Itaongeza thamani ya kazi
yako,kama wale wasomi wazuri,huongea vizuri,na wana maarifa ya kutosha katika mada tofauti tofauti huwa wanapata kukua na kujijenga haraka zaidi kuliko wale wenye
misamiati kidogo na ujuzi wao udogo wa fasihi,utambuzi wa kisayansi,na matukio
ya utandawazi.
Kusoma vitabu ni muhimu pia kwa
kujua au kujifunza lugha mpya,kama kujua maneno yalokuwamo kwenye kurasa. Ambayo
huongeza ujuzi wa kuyaongea na kuandika kwa ufasaha.
5.
Huongeza kumbukumbu
Pindi unaposoma vitabu,unatakiwa
kukumbuka wahusika,asili zao,matamanio yao,historia zao,na pia vitu
tofauti tofauti vyenye mahusiano na wahusika kwa kila habari.Kwa mfumo wa
kumbukumbu,lakini akili ni kipande cha maajabu ambacho huweza kukumbuka vitu na
kukumbuka vitu hivyo vyote na hat mwisho wake vilipoishia. Ni jambo la ajabu ya kutosha,kila
kumbukumbu mpya inayoingia katika akili hutengeneza ujuzi,na huzidishaukomavu wa akili,ambayo husaidiwa na mfumo wa muda mfupi wa kumbukumbu na
kukomaza kukumbuka hizo hisia.Unaionaje hiyo? Imetulia!
6.
Uwezo wa uchambuzi sahihi
Hivi ushawahi kusoma vitabu vyenye
hadithi za kusadikika,na ukapata suluhisho wewe mwenyewe kabla ya kumaliza
kusoma? kama hivyo ndivyo,ulikuwa na uwezo wa kuchambua na kudadavua mawazo
ukayafanyia kazi kwa kuandikamaelezo yote uliyoyapata na kutengeneza matumaini mapya.
Huo ni sawa na uwezo wa kuchambua
ambao mikono yako imemiliki inapokuja haja ya uchambuzi. Kwanza kujua
ulokiandika kipo sawa,kama wahusika walihusika vizuri, hadithi ilitiririka vizuri n.k. Ulishawahi pata nafasi ya kusimuliana kitabu na wengine,utakua na
uwezo wa kuyachambua maoni yako kwa vizuri,kama uliutumia muda wako vizuri kufuatilia
kila ulichokisoma.
7.Huongeza
umakini wa uono wa maoni
Katika uchizi wa dunia ya mtandao,umakini
unapatikana katika milioni ya muelekeo tofauti tofauti kwa wakati mmoja kama
tunavyovifanyia kazi nyingi kwa kila siku. Kwa kila dakika tano ya maisha,wastani
wa kila mtu hugawanya muda wake katika kafanya kazi,kuangalia barua pepe,kupiga soga yaani kuchat na watu zaidi ya mmoja,(kupitia gchat, skype, whatsaap n.k),macho yote kwenye twitter, kuangalia
smartphone, na muingiliano baina na kati ya wafanyakazi wenzake. Hii aina ya
tabia husababisha kuongezeka kiwango cha msongo wa mawazo,ambayo hupunguza uzalishaji wetu.
Pindi unaposoma kitabu,akili yako
yote inakomaa na hadithi-na vingine vilobakia hupotea au unavipuuza na
utajidhatiti zaidi kujishughulisha na undani wa maelezo unayoyapata kutokea kwenye
hadithi. Jaribu kusoma kwa 15-20 dakika kabla ya kazi(i.e asubuhi yako,kama unatumia usafiri wa wote),utashangaa kwa ugunduzi, maarifa na akili kuchangamka ambao uutakuwa umeupata
ufikapo kazini.
8.Ujuzi
wa kuandika vizuri
Hii huwa mkono kwa mkono na uelewa
mzuri kwa upana wake wa misamiati: Utaalam wa kuweka wazi,kazi nzuri ya
maandishi huwa ni matokeo ya mwandishi mwenyewe,kama ugunduzi wa maanguko,mtirirriko,na
aina ya uandishi wa baadhi ya waandishi,na utaalamu wa mbinu za uchoraji na
utunzi wa waandishi tena wakufunzi waliopita, huwa ni matokeo kwa waandishi wameajifunza kutokea kwa
kusoma kazi za wengine.
9.
Utulivu
Kwa kuongezea kitabu kitakupa mapumziko au furaha ambayo inapatikana katika kusoma kitabu kizuri,na inawezekana somo
unalolisoma likakupa faraja ,matumaini na utulivu wa amani ya nafsi. Kama kusoma
vitabu vya imani,hushusha shinikizo la damu yaani blood pressure na hukupa upole aamani na utulivu,na pindi
unaposoma vitabu vya sifa ya kutatua matatizo vinavyoonyesha jinsi ya kusaidia watu waliopata tabu katika
hali fulani,navyo huleta maumivu ya kuumia.
10.Huburudisha
bila ya gharama
Japokuwa wengi wetu tunapenda
kununua vitabu na tunasoma na kuwa ndiokumbukumbu zetu za baadae,huweza vikawa
bei iko juu. Na kwa kuwa na budget ndogo, au unakosa kabisa kiasi cha kukuwezesha kupata burudani ya vitabu ,unaweza tembelea maktaba ilokaribu na eneo lako au kupitia kwenye
maduka na ukapata hata vitatu viwili. Maktaba zina vitabu vya kila aina ya somo
uanalofikiria,na utakua unazunguka hifadhi yake utapata hata vipya
pia,hautaepuka kuacha kusoma.
Kama itatokea utaishi eneo ambalo
halina maktaba,au unaeza ukapata kwingine au hata kwa mtu mwingine kwa
urahisi,maktaba nyingi zina vitabu vyake kwenye PDF au ePub kwahiyo unaweza
soma kupitia mifumo hiyo,iPad,au compyuta yako.Pia kuna vyanzo vingi kwa njia
ya mtandaoni ambapo huweza kupata vitabu vya bure, kwahiyo viwinde hivyo vipya na kisha
usome!
Kuna utofauti wa tabia za kusoma kwa
kila mtu duniani,na huenda ikawa ukaonja ladha tamu na nzuri
katika fasihi ya waandishi,utenzi,magazeti ya
mitindo,maandiko ya dini,vitabu vya vijana,jinsi ya kutoa msaada,mambo ya
mitaani,au vitabu vya kimapenzi,hapo kitakuwepo kinachotaka kwenye akili yako na
mawazo yako. Kaa pembeni na kompyuta yako kwa muda,fungua kurasa za vitabu,na
ukonge moyo wako kwa wakati mwingine.
usiache kutembelea blog yetu nayo inaburudisha kuisoma.
0 comments:
Post a Comment