VITU 4, NJIA 3
Utakuwa ni mdau mkuu mmoja wapo wa
hii blog,kwa vyovyote umejifunza mengi kuhusiana na matumizi na faida ya
vyakula tofauti tofauti japo kwa uchache wake.Kipindi hiki badala ya kulist au
kushare kimatumizi au faida ya aina moja ya chakula,nilifikiri iwe tofauti kwa
topic hii kidogo: Vitu 4, njia tatu.
Oats:
Oats:
kwa Maana ya
kuila tu,oats ina fiber nyingi ya
kutosha,protein,na antioxidants.Iko vizuri katika masuala ya afya ya moyo.Kwa
mwili,oats ni ya ajabu sana inaleta moisture kwenye ngozi na nwele,na nzuri kwa
kinga pia.
Maziwa yenye lozi(Almond milk):
Maziwa ya lozi ni hayana dairy,yana antioxidants nyingi,ni mazuri kwa
afya ya moyo.Yana vitamin na madini kama copper,zinc,magnesium,madini ya
chuma,na calcium-na sio tu mazuri kwa ndani hata kwa kuyatumia nje mazuri,sana tu!
Apples:
Hili
tunda pia lina antioxidant ya kutosha!Apples inasaidia kuboost immune system,inaboost
kumbukumbu sana,na huweza kupambana na cancer,hutosheleza hamu ya kula.Apples
ina vitamins A,B,na C,ambayo huipa ngozi yako muonekano mzuri fresh na wa
kuvutia.
Asali:
Asali ni yenye utamu wa asili
pamoja nayo ni anti-bacterial na antifungal pia.Husaidia kwa kutuliza maumivu
ya kifua na tumbo ,pia ni kilinzi cha vijidudu vya moyo na cancer.Asali ni
nzuri kwa nywele na ngozi ikitumiwa kwa nje,huleta joto na hujenga afya nzuri.
1. Tumia vikiwa vya moto
Vinne hivyo ukitumia kwa kifungua
kinywa huwa ni vitamu sana.Chemsha oats na maziwa yenye lozi,kisha tia lozi
zilokatwa katwa,nyunyizia asali juu,chora mchoro wowote kutumia asali juu ya
hayo maziwa.Ni ladha tamu,rahisi,afya na ya moto.Enjoy it!
2. Tumia vya baridi
2. Tumia vya baridi
Hiki ni kipya ila ni kitamu jaribu
utaipenda nakuhakikishia,hautajutia hayo maamuzi yako!Weka hivyo vyakula vinne vya
ukweli,yaani oats,apple,asali na maziwa ya lozi, katika blender na barafu kama
utapata,zisage mpaka ziwe laini.Nyunyizia au mwagia mdalasini unaweza kuwa unga
au ulotwangwa vipande vidogo dogo kama unapenda,kisha furahia ! This is such a
treat to the taste buds. Utapata wakati mgumu kuamini kwamba ni mlo wenye afya
tele.
3. Pakaa usoni.
Kama zilivyotajwa hapo juu,hivyo vinne
ni vya ajabu sana na vina faida lukuki sana tuu pindi utapotumia kwa nje,na
hufanya kazi vizuri.Changanya vyote kwenye blender(bila ya barafu,isiwe ya
moto),tumia kupakaa usoni,kwa dakika 10 halafu osha uso.Utona uso wako uko
mlaini,msafi,na ngozi nyororo.
Unaweza tumia nafaka nzima pia
kutengeneza kwa ajili ya kusafishia uso.Itumie kama singo mwilini.Kwa wale
mnaotarajia kufunga ndoa singo ndo
hiyoooo! Kazi kwako.