KUTIBU FANGASI YA KUCHA
Fangasi ya kucha,hujulikana kama onychomycosis
ni tatizo sugu linalowakumba wanawake hata wanaume pia.Dalili zake
inflammation,kuvimba,maumivu ya hali ya juu,kucha kusinyaa au kuwasha Visababishi vingine ya fangasi ya kucha ni kuvaa synthetic socks,kuwa katika
mazingira ya unyevu nyevu,PH level ya
ngozi kuwa sio kawaida,mfumo wa immune system mdogo,viatu vyenye
majasho,uchafu,na kisukari.
Kama fangasi ya kucha haitachukuliwa
tahadhari mara kwa mara huweza kusababisha kukatika kwa kucha,splitting,na hata
kuimaliza kucha na kutoka kabisa.well,habari nzuri ni kwamba fangasi ya kucha
hutibika bila hata ya kutumia pesa kwa bill za dawa.Kuna njia za kufanya
zinatibu fangasi kwa mwezi au miezi miwili.
Njia kuu 10 za kutibu fangasi ya
kucha.
1.Tea
tree oil
Tea tree oil ina antiseptic kama
zilokuwemo kwenye fungicide ambayo husaidia sana katika kutibu aina hii ya
fangasi.Haya mafuta hutumika kutibu athari katika ngozi pia.Kama unatatizo la
aina hii ya fangasi ,chukua tea tree oil yenyewe tumia pamba pangusia mafuta
hayo katika sehemu ilo athirika acha kwa dakika 10 kisha mswaki kwa kusugulia
kwenye hiyo sehemu yenye fangasi.Kabla ya kupakaa mafuta hayo kwenye
ngozi,yachanganye na olive oil sawa na kiasi cha tea tree oil au tumia thyme
oil.Hutibu fangasi kama sio ya muda mrefu au iliokomaa,au sugu.
2.Baking soda
Baking soda ni rahisi kupatikana
nyumbani hutibu fangasi pia.Chukua kikombe nusu cha baking soda,vikombe vinne
vya maji moto,moja ya nne ¼ ya kikombe cha peroxide na nusu kikombe cha chumvi
ya Epsom.Changanya hizo zote vizuri na
kisha moja ya nne ¼ ya kikombe cha white vinegar katika mchanganyiko
huo.Lowesha sehemu ilioathirika na vinegar kwa dakika chache kisha pakaa ule
mchanganyiko kwenye hiyo sehemu tumia pamba na kisha ifunge hiyo pamba kwenye
hiyo sehemu iloathirika kwa fangasi.Tumia njia hii kila baada ya saa 10 kwa
muda wa wiki nne.
3.Mafuta
ya machungwa
Njia nyingine ni kutumia mafuta ya
machungwa.Aina zote za machungwa ni antifungal nayo huweza kutibu fungasi.Kwa kudondoshea
kitone cha mafuta hayo kila siku katika hapo penye fangasi,juu,chini na
katikati ya kucha na iache kwa saa moja.Pia unaweza ukaichanganya hayo mafuta
ya machungwa sawa na mafuta mengine yoyote ,kama mafuta ya mbegu za zabibu.Kama
mafuta ya machungwa yataleta allergy na kusababisha madhara,ni vizuri
kujaribisha kwenye ngozi kwanza kabla ya kuyatumia kwa kujitibu
4.White vinegar
4.White vinegar
White vinegar ni moja wapo ya tiba
nzuri ya fangasi ya kucha.Changanya kama kijiko kimoja cha vinegar na vijiko
viwili vya maji ya vuguvugu.Kisha lowesha sehemu iloathirika na mchanganyiko
huo kwa dakika kumi hadi kumi na tano kila siku.Kama utahisi ngozi inaungua
zidisha maji kidogo kwa vinegar.Ni muhimu kukausha eneo la fangasi baada ya
kunawa au kuoga,la sivyo fangasi itaenea na kuambukiza kwengine.
5.Kitunguu thoum
5.Kitunguu thoum
Kitunguu thoum kina allicin,ambayo
ina antifungal na hutibu fangasi pia.Kwa kutibu mara ya kwanza tumia mafuta ya
kitunguu thoum changanya sawa na vinegar namaanisha kipimo cha vinegar na
mafuta viwe sawa.kisha pakaa eneo la fangasi na pembeni zake kisha funga tumia
bandage.Ikiwa mafuta ya thoum hayapatikani,tengeneza mwenyewe kwa
kuisaga,chukua vitunguu thoum viwili kisha changanya na vijiko viwili vya kula
vya olive oil.kisha iache kwa saa
24.Hata kula kitunguu thoum kimoja kila siku nayo ni dawa ya fangasi pia.
6.Juisi ya siki ya apple
6.Juisi ya siki ya apple
Juisi ya siki ya apple ina acid ya
asili na huweza kulinda na fangasi ya kucha kuendelea.hapo hapo juisi hii
hupambana na vijidudu na huua bacteria.Chukua juisi ya siki ya apple changanya
sawa kwa sawa na maji kwa kipimo chochote utachotumia.Kisha utaitumia kwa
kuloweshea sehemu ya fangasi kila siku kwa muda wa nusu saa.Kama utafanya hivi
kwa muda wa wiki kadhaa utaona mabadiliko kwa muda mfupi tu.Njia nyingine unga
wa ground rice changanya na vijiko vichache vya juisi ya siki ya apple,pakaa na
husaidia kuondoa ngozi iliokufa na kuiweka ngozi yako kuwa laini.
7.
Listerine Mouth Wash
Listerine mouth wash inaua bacteria
na germs mdomoni huweza kutibu fangasi ya kucha pia.Hii ni kwa sababu mouth
wash hii ina alcohol yenye nguvu nyingi za antiseptic huweza kupambana na
bacteria na fangasi pia.Chukua pamba lowesha hii mouth wash na vinegar na maji
ya ndimu ambayo hayajachanganywa na maji.Kisha unaweza loweka miguu au mguu au ukapakaa
mchanganyiko huo kwa dakika kumi hadi kumi na tano kila siku na kisha tumia kwa
kusugulia pia.Fanya hivyo kila siku mpaka ile kucha ya zamani itaondoka itakuja
mpya na nzuri.
8.
Lavender Oil
Lavender oil ina volatile na antiseptic
properties ambayo ina uwezo wa kupambana na aina yoyote ya infection na
kuilinda ngozi kuharibika pia.Chukua kiasi cha lavender oil na tea tree oil
changanya vizuri kisha fanya kuipasha iwe ya uvuguvugu kidogo.Kisha funga kwa
kutumia pamba katika kidole mara mbili au tatu kwa siku.Na vizuri pia kupakaa
mchanganyiko huo kabla ya kulala.
9.
Oregano Oil
Oregano oil ina antiseptic,
antibacterial, anti-parasitical, antiviral, analgesic na antifungal pia.Huweza
tumika kutibu fangasi ya kucha.Chukua matone mawili ya mafuta ya oregano na
changanya na vijiko viwili vya chai vya olive oil.kisha pakaa kwa fangasi kwa
siku mara moja.Fanya hivyo kwa muda wa wiki tatu.
10.Juisi
ya ndimu
Juisi ya ndimu ina antiseptic na ni
antifungal pia.Citric acid iliyomo kwenye ndimu husaidia kumaliza fangasi za
kucha na kutoambukiza.Chukua juisi fresh ya ndimu na pakaa direct sehemu yenye
fangasi na uache kwa dakika 10 kabla ya kusuuza na maji ya uvuguvugu.Tiba hii
irudiwe kila siku kwa muda wa mwezi mmoja mpaka uone matokeo mazuri.Njia
nyingine changanya juisi ya ndimu sawasawa na olive oil na tumia mchanganyiko
huo kusugulia au massage sehemu yenye fangasi.Olive oil itafanya ngozi yako
kuwa laini na juisi ya ndimu itasaidia kuzuia madhara ya fangasi.
Kwa hizo tiba za asili hapo juu za
kutibu fangasi ya kucha,matokeo yake hutegemeana na juhudi ya kuzitumia hizo
dawa.Itumike kwa muda wa kuanzia mwezi na kuendelea ndipo utapoona matokeo
mazuri.
SHARE AND ENJOY !
SHARE AND ENJOY !
0 comments:
Post a Comment