• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Friday, October 25, 2013

KUONDOA MADOA,(ACNE)MWILINI.

5:02 AM // by Kalma // 1 comment

Uko tayari na hiyo siku yenyewe,ushajipanga mwenyewe tarehe tayari,job interview,wedding day,ukijiangalia usoni una pimples,madoa au mabaka .Si majanga hayo?  Doa au kovu madoa hutokea kwa wakubwa 95%.Hakuna tofauti kati ya Spot na acne,kwa kiswahili ipo ila humo humo.

Doa ni mvunjiko wa ngozi,wakati acne huenea mwili mzima.Huweza tokea usoni,kifuani,mgongoni,begani na Buttocks.

        Doa ni kuziba kwa tezi karibu na uso wa ngozi uitwao Sebaceous gland.Hizi tezi huzibwa na Sebum ambazo ni mafuta yaliyozidi yakichanganyika na cells mfu za kwenye ngozi wakati wa kufunguka kwa tezi. Matokeo yake ndio Chunusi.


     Na kama sehemu iliyoziba kuna Bacteria wanaishi katika uso wa ngozi na wanasababisha wekundu,kuvimba hutokana na level ya hormones na hutoa white pus,kutokea kwa whiteheads.

 Doa pia huweza sababishwa na kubadilika kwa hormones kipindi cha Balehe au kuvunja ungo,ujauzito,na mijengeko imara iliosababishwa na Stress tokea mfumuko wa hormones.
     Na haswa mihangaiko ya shughuli za siku kubwa kama harusi,interview n.k.
    Ukishakuwa na madoa sehemu ya mwili ni budi kuyatibu.

Tuwe pamoja tukishuhudia hizi tiba;

Anza kwa Dermatologist,mtaalam wa ngozi kukupatia sababu ya hizo doa, na atakupa ufumbuzi tu ye si mtaalam banaa.

Kuna Antibiotics na dawa yenye Benzoyl Peroxide,inakausha na hutibu sehemu iliyoharibika kwenye ngozi.

         Kujitibu kwa vitu vya asili ni rahisi na gharama ndogo.ukizingatia vitu vya asili vinakufanya uwe mrembo na mwenye afya nzuri .

          Majani ya chai ya mafuta 

Ni antibacterial na anti-inflamatory,kwa kupakaa kwenye doa .Changanya na maji kwanza.

          Rose waterIna anti-inflamatory na aroma za kwenye rose huacha spirits na huondoa haraka stress na tension.

Kama unasumbuliwa na doa mdomoni na kidevuni ni vizuri kumuona mtaalam kwa ushauri.Na kama ni mwanamke kutakuwa kuna walakini hapoo,na huenda ikawa Polycystic Ovary Syndrome.
         Osha uso kwa kumwagia maji mbele ya uso.yaani jimwagie tumia shawa kama kuflash hivi.Hii husaidia kusuuza uchafu.
       KUJIFUKIZA

Chemsha maji weka kwenye bakuli na jifunike na taulo ukiwa umeweka uso karibu na bakuli. Kama mini sauna,kwa dakika  10 kisha osha uso kwa maji baridi,kufunga vinywelea kulinda na bacteria.

           Exfoliate

Clearis,Freederm,na tumia kusafishia asubuhi na jioni.Cream-Sudocrem,nayo husaidia pakaa usiku kucha,zipo madukani. Maganda ya ndizi weka kwenye doa kwa dk 10-15.Ndizi mbivu ilioiva.Kunywa maji kwa wingi huondoa uchafu.Badili Snacks kwa matunda.Tumia dawa kama iko mbaya T-ZONE SPOT ZAPPING STICK pakaa usoni au mwilini kwenye madoa .
           Punguza make-up.

Tumia product zenye Azelaic Acid ina antibacterial  hupunguza wekundu,hata mwenye rangi nyeusi wekundu upo sema hauonekani, na kuungua,na hupatikana kiasili tokea ngano na shayiri (barley).
           Baking sodaChanganya na maji na gandisha kwenye madoa usiku kucha osha asubuhi .

Aspirin tablets Changanya na maji ongezea Zit kupunguza kuvimba na wekundu.

Tumia dawa ya meno

kukausha chunusi,madoa .

Olive Oil 

Pakaa usoni na hata kwingine kwenye madoa kwa dakika 15 osha au oga kwa maji ya uvuguvugu.

Saga tango na OatmealTango husafisha madoa meusi,na Oatmeal hulainisha ngozi pakaa kwa dakika 15-20.

Pakaa asali.Toa kiini cha yai piga ute wa mayai mawili pakaa mpaka ikauke ,igande kabisa tumia maji ya vuguvugu.

Tumia Lavender,rosemary,thyme,sandalwood mafuta yake.

Usikamue chunusi au doa mwilini na haswa ikiwa hakina kichwa huweza kuongeza bacteria ndani ya ngozi.
      Ulakini wa usafi wa mkono pia sio vizuri kukamua,na ikibidi tumia tissue kuepusha kujiumiza na kucha.weka majani ya chai ya mafuta pale ulipokamua kama antiseptic cream kwa usafi zaidi.
   
Barafu nzuri kwa palipovimba ila inaweza sabaisha kuungua.
Usitumie steamer kwa usiku tatu mfululizo hufanya ngozi iwe kavu.

Kwa mabadiliko yoyote baada ya tiba yoyote yasiyo ya kawaida! haraka ondoa au acha kutumia na osha kwa maji baridi au moto yote poa tu.

Mask ya uso fanya mara 2-3 kwa wiki kwa dakika 15-20 hukausha ngozi kwa ngozi ya mafuta na husafisha vinywelea.Ngozi ya mafuta huathiriwa zaidi na madoa na chunusi na vitu kama hivyo.

   Tiba hizo tumia sehemu yoyote ya mwili haina madhara.Muone daktari mtaalamu kwa matumizi ya dawa .Hii ni supplements usitumie bila kumuona daktari.

Mama mjamzito hashauriwi kutumia dawa bila ushauri wa daktari.










1 comment:

  1. I really wish nipate dawa ya kuondoa blackspots na inflammations on my face.

    ReplyDelete