Maumivu ya kichwa sio fun.Wakati
wowote huweza kukutokea,huwezi jua…sidhani kama unaweza kufanya kitu.Kwa upande
wangu mimi ikinitokea huwa natamani kufanya lolote maumivu yapotee na yasirudie
tena ikiwezekana.Kipindi cha kubadili hali ya hewa ,kichwa huwa ni kawaida kila
mtu kuumia au kuumwa,na haswaa kukiwa baridi sana,naziweka hizi tukifanya hivi
tunaweza punguza maumivu ya kichwa,kwa kutumia tiba asili.
Dawa nazo sio nzuri
kwa afya zetu wote.
Kuna aina nyingi na tofauti za
maumivu ya kichwa,na tofauti ya hisia za mwili na tiba zake, najaribu kutoa
aina tofauti ya tiba za asili ambazo huenda ikawepo moja wapo kuwa tiba kwako
wewe na mimi kadhalika.
1. Maji
Dehydration
inajulikana sababu mojawapo kuu ya maumivu ya kichwa.Tunajua kwamba
tunahitajika kunywa maji ya kutosha kwa siku,kiasi cha glasi nane(8),la
kushanagaza ni rahisi kusema kuliko kutekeleza.Kama unahisi maumivu ya kichwa
yanakuanza,la kwanza jiulize umekunywa maji kiasi gani kwa siku hiyo?na kisha
kunywa maji .Kama kinga awali,ni vizuri kunywa maji ya kutosha kila
siku.Utapata faida nyingi nyengine ndani
yake,maji huondoa sumu toka mwilini hupitia kwenye ngozi,hiyo ni faida
mojawapo, zipo nyingi tu.
2. Chai
Kunywa chai kwa wingi-yenye
Tangawizi,kivumbazi(peppermint), au chamomile –husaidia kutuliza maumivu
ya kichwa ya aina zote .Tangawizi ni nzuri kwa migraines huzuia synthesis ya prostaglandin (ambayo husaidia kutuma dalili za
maumivu kwenye ubongo),na kulainisha au kutuliza kujisikia uchovu,ambao uchovu
huendana na migraines
au kipanda uso.
Kivumbazi(peppermint) husaidia kupunguza na kutuliza maumivu
pia-na tokapo kivumbazi(peppermint) nayo huondoa uchovu wa mwili,nayo pia
hutibu kipanda uso. Chomomile hutumika
kutibu na kukinga maumivu ya kichwa,hupumzisha misuli na husaidia
kupunguza stress
(chanzo kikuu cha kuumwa ni kichwa).
3. Essential Oil
Aromatherapy
ilianza tumika karne kama kituliza maumivu .Ni aina moja wapo matata ya
kutuliza maumivu ya kichwa nayo ni lavender(mvinyo), peppermint,(kivumbazi) na eucalyptus.
Matumizi yake,changanya mafuta na maji au mafuta ya nazi na sugua temples,shingo,na
mabegani.Njia nyingine kutumia aromatherapy ni kuongezea tone ya mafuta ya maji
katika maji ya uvuguvugu ya kuogea.Mchanganyiko huo wa maji ya uvuguvugu na
mafuta yenye harufu kama karafuu,mafuta ya nazi, huwa ni kituliza maumivu na
hukufanya ujisikie umeuondoa uchovu na kuondoa maumivu ya kichwa.
4. Acupressure
Acupressure
husaidia kutuliza maumivu kwa kutumia kulainisha mishipa ilojikaza au
kukakamaa na kuondoa endorphins,ni dawa asili ya mwili.
Na sehemu nzuri za acupressure
kwa maumivu ya kichwa ni:
- paji la uso(komwe) — kwenye
kope
- temples
- nyuma shingoni — sehemu ya
katikati
- juu ya kichwa(kichwani) — upande
wa katikati, mstari kwa kuelekea masikioni
- mikono —ukuta kati ya kidole gumba
na kidole shahada
- juu ya mguu — katikati ya kidole
gumba na kidole kinachofuatia
Tumia kidole gumba kupakaa au
kufanya massage
hiyo sehemu kwa mtindo wa
kuzunguka.Endelea kufanya hivyo kwa 1-2dakika,au mpaka utapojisikia kunaanza kuwa
pamoto.
Tahadhari
: Acupressure hii huweza sababisha
kizunguzungu au lightheadedness,chukua tahadhari
kabla haijatokea hivi.
5. Mapumziko
Kupumzika ni sababu yatosha kujisikia vizuri wakati wote-na maumivu ya
kichwa yakiwemo kwenye list.maumivu haya sana husababishwa na stress na wasiwasi,tafuta
namna ya kujipumzisha husaidia kutibu shida hii muda huo huo,na huzuia
kutorudia maumivu ya kichwa kabisa.
6. Apple Cider Vinegar
Tiba hii ni mapendekezo ya mdau
wangu mmoja hivi.(nakushukuru sana!!) japo research ilifanyika na ikaonekana ni tiba ya kichwa.Kuna aina
mbili za kufanya: njia ya ingestion na vaporization(uvukizi). Njia ya ingest,unaweza
changanya vijiko 2 vya kula vya apple cider vinegar katika glasi ya maji na kunywa
yote kwa pamoja.hii inafanya damu kutembea vizuri katika mwili,na vile vile
husaidia kubalansisha kiasi cha PH mwilini.
Njia ya vapor unachukua vijiko 2 vya
kula vya apple
cider vinegar katika sufuria na vikombe 2 vya maji yaliyochujwa kisha chemsha.Ukianza kuona
mvuke sasa zima jiko.
chukua taulo weka kichwani
mwako kisha inamia huo mvuke wa huo mchanganyiko,hema kidogo dogo mpaka utapoona maumivu yanapungua au kuisha
kabisa.
SHARE AND ENJOY !
apple cider vinegar ni juisi ya siki ya apple. Kwa hiyo hayo maneno mekundu ndio unahitaji tafsiri yake
ReplyDeleteNdio Mdau
ReplyDelete