• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, March 18, 2014

VITU 4, NJIA 3

6:58 AM // by Kalma // No comments

VITU 4, NJIA 3
 Utakuwa ni mdau mkuu mmoja wapo wa hii blog,kwa vyovyote umejifunza mengi kuhusiana na matumizi na faida ya vyakula tofauti tofauti japo kwa uchache wake.Kipindi hiki badala ya kulist au kushare kimatumizi au faida ya aina moja ya chakula,nilifikiri iwe tofauti kwa topic hii kidogo:  Vitu 4, njia tatu.

 Oats: 
kwa Maana ya kuila tu,oats  ina fiber nyingi ya kutosha,protein,na antioxidants.Iko vizuri katika masuala ya afya ya moyo.Kwa mwili,oats ni ya ajabu sana inaleta moisture kwenye ngozi na nwele,na nzuri kwa kinga pia.
Maziwa yenye lozi(Almond milk): 
Maziwa ya lozi ni hayana dairy,yana antioxidants nyingi,ni mazuri kwa afya ya moyo.Yana vitamin na madini kama copper,zinc,magnesium,madini ya chuma,na calcium-na sio tu mazuri kwa ndani hata  kwa kuyatumia nje mazuri,sana tu!

 Apples: 
Hili tunda pia lina antioxidant ya kutosha!Apples inasaidia kuboost immune system,inaboost kumbukumbu sana,na huweza kupambana na cancer,hutosheleza hamu ya kula.Apples ina vitamins A,B,na C,ambayo huipa ngozi yako muonekano mzuri fresh na wa kuvutia.
Asali
Asali ni yenye utamu wa asili pamoja nayo ni anti-bacterial na antifungal pia.Husaidia kwa kutuliza maumivu ya kifua na tumbo ,pia ni kilinzi cha vijidudu vya moyo na cancer.Asali ni nzuri kwa nywele na ngozi ikitumiwa kwa nje,huleta joto na hujenga afya nzuri.
Na sasa… hizi njia  3 za kutumia kwa 4 vitamu !
1. Tumia vikiwa vya moto
Vinne hivyo ukitumia kwa kifungua kinywa huwa ni vitamu sana.Chemsha oats na maziwa yenye lozi,kisha tia lozi zilokatwa katwa,nyunyizia asali juu,chora mchoro wowote kutumia asali juu ya hayo maziwa.Ni ladha tamu,rahisi,afya na ya moto.Enjoy it! 
2. Tumia vya baridi
Hiki ni kipya ila ni kitamu jaribu utaipenda nakuhakikishia,hautajutia hayo maamuzi yako!Weka hivyo vyakula vinne vya ukweli,yaani oats,apple,asali na maziwa ya lozi, katika blender na barafu kama utapata,zisage mpaka ziwe laini.Nyunyizia au mwagia mdalasini unaweza kuwa unga au ulotwangwa vipande vidogo dogo kama unapenda,kisha furahia ! This is such a treat to the taste buds. Utapata wakati mgumu kuamini kwamba ni mlo wenye afya tele. 


3. Pakaa usoni.
Kama zilivyotajwa hapo juu,hivyo vinne ni vya ajabu sana na vina faida lukuki sana tuu pindi utapotumia kwa nje,na hufanya kazi vizuri.Changanya vyote kwenye blender(bila ya barafu,isiwe ya moto),tumia kupakaa usoni,kwa dakika 10 halafu osha uso.Utona uso wako uko mlaini,msafi,na ngozi nyororo.
Unaweza tumia nafaka nzima pia kutengeneza kwa ajili ya kusafishia uso.Itumie kama singo mwilini.Kwa wale mnaotarajia kufunga ndoa  singo ndo hiyoooo! Kazi kwako.



0 comments:

Post a Comment