• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, June 10, 2015

Faida ya salad

6:46 AM // by Kalma // No comments

Faida ya salad
Kutumia au kula salad kila siku huleta faida nyingi mwilini. Hata hivyo salad ni afya na lishe rahisi ambayo mtu anatakiwa iwe ni tabia ajizoeshe nayo katika mlo wake.
Ni rahisi kuitengeneza,salad hukuweka karibu kila siku kwa kupata mboga mboga na matunda kama ilivoshauriwa.Unaweza kuongeza mafuta iwapo utakua unakula kila siku matunda na mboga mboga  na bado ukajenga afya yako  kutokea faida za salads.
 Fiber
Faida kuu ya salad ni kupatikana kwa fiber.Kula salad hutengeneza fiber nyingi mwilini,ambayo hupambana na vimbizi au shibe na inapunguza cholesterol.Fiber ipatikanayo kwenye salad husaidia kushiba haraka na kula kidogo.
Hii husaidia kupunguza uzito kwa baadhi  wasiopenda.Sababu salad ni shibe tosha,kula kabla hujala chakula kikuu(main meal)hupunguza kiasi cha calories ambacho ungeongezea tokea mlo wako.Kiasi kidogo cha calories unachokula kutokana na fiber  hupunguza uzito.
M-badala unaofaa
Wasomi wameonyesha  watu wengi  hawali  vyakula vya lishe na afya kama vilivoshauriwa.Wanapendekeza zaidi kula salad na matunda zaidi.Kula salad na matunda kila siku ni m-badala unaofaa  kwa mboga mboga na matunda,ambayo yanasababisha lishe na afya nyingi inayotakiwa mwilini.

Antioxidants
Mara kwa mara ukila salad ya kijani au green salad,unapata  kiasi kikubwa cha juu cha damu  yenye nguvu ya antioxidants.Mboga ina antioxidants muhimu sana kama vitamin C, lycopene, beta carotene na folic acid inalinda na madhara ya miale ya jua. Antioxidants ina sifa  ya kulinda dalili za uzee.
 Mafuta
Kwa kula salad,utakua umeongeza kuipata fat vizuri.Na mafuta hayo hupatikana kwa parachichi,karanga,au olive oil katika salad yako.Husaidia mwili kufyonza phytochemicals vizuri inayotakiwa mwilini.
  
Salads ina hasara kidogo au haina hasara kabisa, ambayo ni maandalizi yake na hutumia muda.

Saturday, June 6, 2015

5 Matunda kwa afya na mng’ao wa ngozi

4:05 AM // by Kalma // No comments

5 Matunda kwa afya na mng’ao wa ngozi
Kupatikana kwa 5 mazuri matunda fresh kwa afya na mng’ao wa ngozi hupendeza na kuvutia kwa kila mmoja wetu.Ni vizuri kuyapata katika kila mlo wako wa kila siku.!”Maisha ya kawaida hutofautiana kwa kuyapata matunda haya kwa kila mlo wako wa kila siku ambayo utang’aza ngozi yako na kuimarisha afya yako.Matunda husaidia kusafisha uchafu wa mwilini,kutengeneza na kurembesha ngozi,hydration ya kiasili,muonekano na mnga’ao wa ngozi,hutengeneza ngozi kuwa na muoekano wa ujana kila siku,na kutengeneza ngozi nyororo na laini. 
Matunda ni salama bila ya madhara yoyote kwa upande wowote wa kiafya ya mwili kwa muda wote.
Hayana sumu na yenye manufaa mengi katika kuboresha lishe na afya nzuri ya mwili na ngozi wa ujumla.
Ndizi
Ndizi ina wingi wa  Vitamini kama A, B na E. Hufanya kazi ya anti-ageing. Chagua tunda hili kwa kusafishia uso(facial)tumia ndizi iliosagwa changanya na asali kwa kung’arisha ngozi.Ni chanzo kikuu cha fibre ,madini,magnesium,na potassium,husaidia kurahisisha mzunguko wa damu mwilini na kujenga vilinda mwili imara.Ni tunda zuri kwa m-badala wa kurudisha afya kama kiburudisho katika mlo wako. 
 Papai
Ina antioxidants na enzyme waitwao Papain, papai hulinda na uchafu kwenye ngozi na huondoa seli mfu zinazotumika kwenye ngozi.Pakaa uso taratibu kwa dakika kadhaa,husafisha na hulainisha ngozi yako.Saga papai changanya na vijiko 2 vya chakula vya asali au maziwa ya mtindi,tumia mchanganyiko huo kama mask.Tumia maji ya uvuguvugu kwa kunawia baada ya dakika 20 kisha pakaa moisturizer utaona tofauti.
 Ndimu
Ndimu ina Vitamin C nyingi na hutumika kama bleach ambayo ni cleanser nzuri  huondoa mikunjo,makovu na madoa doa,na kupauka kwa ngozi.Anza siku yako kwa kunywa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na kijiko cha ndimu na kijiko cha chai cha asali ukiwa hujala kitu.Mchanganyiko huu husaidia kupambana na cellulite na kusafisha ngozi yako kwa ndani zaidi.Kinywaji hiki hupunguza na kuondoa mikunjo kwenye ngozi na husababisha mng’ao asilia.

Chungwa
Machungwa yana Vitamin C,kwahiyo huongeza mng’ao wa ngozi.Huondoa mikunjo na hupunguza kuzeeka kwa ngozi.Kausha maganda ya machungwa yasage kisha yahifadhi kwa container zuri.Tumia kwa kupakaa kama scrub mara moja au mbili kwa wiki kwa kusafishia uso na kung’arisha ngozi. 
Apple
Tunda hili  yana antioxidant, hulinda kuharibika kwa seli na tishu na yanafanya kazi ya kulinda uzee kwa ngozi.Hupunguza mikunjo na kusafisha mistari inayojitokeza kwenye ngozi na kusafisha ngozi pia.Tengeneza juice ya apple changanya na asali pakaa usoni,ikikauka utaosha.Ni mask nzuri yenye kusafisha na kulainisha ngozi na kuifanya ngozi yako ing’ae na kuvutia.