• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, June 10, 2015

Faida ya salad

6:46 AM // by Kalma // No comments

Faida ya salad
Kutumia au kula salad kila siku huleta faida nyingi mwilini. Hata hivyo salad ni afya na lishe rahisi ambayo mtu anatakiwa iwe ni tabia ajizoeshe nayo katika mlo wake.
Ni rahisi kuitengeneza,salad hukuweka karibu kila siku kwa kupata mboga mboga na matunda kama ilivoshauriwa.Unaweza kuongeza mafuta iwapo utakua unakula kila siku matunda na mboga mboga  na bado ukajenga afya yako  kutokea faida za salads.
 Fiber
Faida kuu ya salad ni kupatikana kwa fiber.Kula salad hutengeneza fiber nyingi mwilini,ambayo hupambana na vimbizi au shibe na inapunguza cholesterol.Fiber ipatikanayo kwenye salad husaidia kushiba haraka na kula kidogo.
Hii husaidia kupunguza uzito kwa baadhi  wasiopenda.Sababu salad ni shibe tosha,kula kabla hujala chakula kikuu(main meal)hupunguza kiasi cha calories ambacho ungeongezea tokea mlo wako.Kiasi kidogo cha calories unachokula kutokana na fiber  hupunguza uzito.
M-badala unaofaa
Wasomi wameonyesha  watu wengi  hawali  vyakula vya lishe na afya kama vilivoshauriwa.Wanapendekeza zaidi kula salad na matunda zaidi.Kula salad na matunda kila siku ni m-badala unaofaa  kwa mboga mboga na matunda,ambayo yanasababisha lishe na afya nyingi inayotakiwa mwilini.

Antioxidants
Mara kwa mara ukila salad ya kijani au green salad,unapata  kiasi kikubwa cha juu cha damu  yenye nguvu ya antioxidants.Mboga ina antioxidants muhimu sana kama vitamin C, lycopene, beta carotene na folic acid inalinda na madhara ya miale ya jua. Antioxidants ina sifa  ya kulinda dalili za uzee.
 Mafuta
Kwa kula salad,utakua umeongeza kuipata fat vizuri.Na mafuta hayo hupatikana kwa parachichi,karanga,au olive oil katika salad yako.Husaidia mwili kufyonza phytochemicals vizuri inayotakiwa mwilini.
  
Salads ina hasara kidogo au haina hasara kabisa, ambayo ni maandalizi yake na hutumia muda.

0 comments:

Post a Comment