Mahitaji ya Msingi ya Mapambo ya Kila Chumba Katika Nyumba Yako
Unaweza kuwa na mtindo wa mapambo ya jumla uliochaguliwa kwa nyumba yako yote, lakini kwa mtindo wa jumla, kila chumba kina kusudio na mtindo wake. Jinsi matumizi ya chumba,kinatumiwa na nani, inapaswa kuzingatiwa unapopanga kila chumba na kuchagua vifaa,mapambo, na uzuri na aina ya mapambo hayo.Zingatia mahitaji ya kila chumba na muhusika binafsi, na mapambo kulingana na nafasi ya hicho chumba. Mapambo ya nyumba yanapaswa kuonyesha hisia na ladha yenye maslahi binafsi, lakini lazima pia izingatie kazi maalum ya hivyo vyumba.
Living rooms(sebule ya kupumzika na familia)
Sebule
Sebule zinaweza kutumika kwa kazi nyingi, ni chumba rasmi kinatumika kwa kusalimiana na wageni,ni sehemu hata familia inatumia kusoma kwa Pamoja, ni sehemu ya burudani,kufurahia na kucheka Pamoja,na kucheza pia.Kwa nyumba za kisasa, sebule ni chumba kikubwa kimekuwa karibu na kuhusishwa Pamoja na jiko na dining area.Kubwa la kuzingatia ni kuchagua haswa mahala kwa ajili ya sebule au living room na haswa kuweka eneoau sehemu ya mazungumzo. Chaguo lako na mipangilio ya hiyo sebule yapaswa kiuzingatia akilini mwako.Hapo ndipo unaweza kusonga na mipangilio jinsi ya pa kuweka taa,sehemu ya zulia au rugs,marembo ya sanaa na mengineyo.
Vyumba vya kulala(Bedrooms)
Unatumia theluthi moja ya maisha yako kwenye chumba cha kulala, kwa hivyo unapaswa kuzingatia kwa uangalifu mikakati ya kupafanya mahali pazuri. Anza na kuchagua kitanda na fanicha zingine za chumba cha kulala. Wakati unaweza kuokoa pesa katika maeneo mengine,nunua godoro na mito bora na huo ndio uwekezaji mzuri.Chaguo lako la rangi pia ni muhimu kwenye chumba cha kulala-chagua rangi zisizokolea ikiwa wewe ni mtu wa asubuhi, au rangi zilizokolea kama wewe ni wa kuchelewa. Taa ya chumba cha kulala ni muhimu kwa kuweka mood au hali nzuri, na piaIkiwa huna sehemu kubwa,tafuta ideas ya kupamba chumba kidogo kipendeze.Na vyumba vya kulala vya wageni vina mahitaji yao ya kipekee kwenye kupamba.
Vyumba vya watotoKwa mapambo ya vyumba vya watoto, bado ni mazoea ya kawaida kutumia mandhari ambayo kwa ajili ya wavulana na wasichana, ingawa wazazi wa kileo wameazidisha kutengeneza kufanya vyumba vya watoto kuwa vya kijinsia zaidi.Chumba cha mtoto mchanga kina mahitaji yake ya kupamba, haswa ambapo familia za vijana ambazo bajeti inaweza kuzingatiwa.
Bafu ya kisasaJe! Unataka kubadilisha bafu lako kuwa spa ya kifahari? Angalia ideas za bafu , pamoja kukifanya chumba kihisi ni mapumziko na cha kisasa, na jinsi ya kuchagua makabati, tile, sinki, vioo, taa, na marembo. Katika bafu dogo, changamoto ni kuliremba ili lionekane kubwa.Ikiwa bafuni yako mpya inajumuisha mradi kamili wa kurekebisha, tafuta vidokezo juu ya kufanya liwe zuri na la kisasa. Maamuzi mengine muhimu yatakuwa kuchagua rangi na kuchagua sink zuri na marembo ya kuvutia.
JikoniJikoni kunaweza kuwa ni chumba cha gharama kubwa kurekebisha, kwa hivyo unatakiwa kupanga kwa uangalifu mradi huo wako. Ikiwa urekebishaji kamili haitoshelezi na budget yako,basi tumia njia rahisi kuleta muonekano,ikiwemo usafi wa kina yaani deep cleaning,kurudia rangi,kuweka taa za kisasa,kubadili makabati,kuongeza mapambo,kubadilisha sink,mifereji na mabomba.Mwishowe, chaguo mapambo pekee na rahisi yanayoweza kufanya jiko lionekane jipya kabisa.Na kwa kweli,kwa uchaguzi huu wa mapambo ni sehemu kuu ya uboreshaji wowote wa jikoni ya bajeti ndogo ya mradi huo.
Chumba cha kulia(Dining Rooms)Meza katika chumba cha kula yaani dining room table ni kitu muhimu humo,kwa hivyo chaguo na uwekaji wake ni muhimu katika mapambo. Kuchagua fanicha sahihi inaweza kuwa muhimu sana kwa chumba kidogo cha kula. Vitu vingine muhimu vya kuzingatia ni viti na taa za kuning’inia au chandelier — ambazo zote husaidia kufafanua mtindo wako na kuweka sauti ya chakula. Mwishowe, zingatia kwenye mapazia na vitambaa vya kutandika mezani na marembo mengine.
Foyers
Foyer inapaswa kuwa nafasi ya kukaribishia ambayo huweka muonekano wa eneo la kupumzika, lakini pia kuna mambo mengi ya kuzingatiwa unapobuni na kupamba foyer yako. Sakafu, vifaa vya kuhifadhia, na aina ya marembo ni mambo muhimu katika kubuni foyer.
Ofisi ya NyumbaniUtakuwa na mahitaji tofauti ikiwa utaona wateja katika ofisi yako ya nyumbani na kutumia nafasi hiyo kwa sababu za kitaalam. Lakini hata ikiwa ni mahali tu kwako kwa ajili ya ,kufanya biashara ya na familia, kuna vidokezo maalum vya kupanga na kupamba ofisi ya nyumbani. Pale ambapo bajeti inazingatiwa, tafuta chaguzi za kuokoa pesa.
SHARE AND ENJOY !