Mahitaji ya Msingi ya Mapambo ya Kila Chumba Katika Nyumba Yako
Unaweza kuwa na mtindo wa mapambo ya jumla uliochaguliwa kwa
nyumba yako yote, lakini kwa mtindo wa jumla, kila chumba kina kusudio na
mtindo wake. Jinsi matumizi ya chumba,kinatumiwa na nani, inapaswa kuzingatiwa unapopanga kila
chumba na kuchagua vifaa,mapambo, na uzuri na aina ya mapambo hayo.Zingatia mahitaji ya kila chumba na muhusika binafsi, na mapambo
kulingana na nafasi ya hicho chumba. Mapambo ya nyumba yanapaswa kuonyesha hisia
na ladha yenye maslahi binafsi, lakini lazima pia izingatie kazi maalum ya hivyo vyumba.
Living rooms(sebule ya kupumzika na familia)
Sebule
Sebule zinaweza kutumika kwa kazi nyingi, ni chumba rasmi kinatumika kwa
kusalimiana na wageni,ni sehemu hata familia inatumia kusoma kwa Pamoja, ni
sehemu ya burudani,kufurahia na kucheka Pamoja,na kucheza pia.Kwa nyumba za
kisasa, sebule ni chumba kikubwa kimekuwa karibu na kuhusishwa Pamoja na jiko
na dining area.
Kubwa la kuzingatia ni kuchagua haswa mahala kwa ajili ya
sebule au living room na haswa kuweka eneoau sehemu ya mazungumzo. Chaguo lako
na mipangilio ya hiyo sebule yapaswa kiuzingatia akilini mwako.Hapo ndipo
unaweza kusonga na mipangilio jinsi ya pa kuweka taa,sehemu ya zulia au rugs,marembo
ya sanaa na mengineyo.
Vyumba vya kulala(Bedrooms)
Unatumia theluthi moja ya maisha yako kwenye chumba cha
kulala, kwa hivyo unapaswa kuzingatia kwa uangalifu mikakati ya kupafanya
mahali pazuri. Anza na kuchagua kitanda na fanicha zingine za chumba cha
kulala. Wakati unaweza kuokoa pesa katika maeneo mengine,nunua godoro na mito bora
na huo ndio uwekezaji mzuri.
Chaguo lako la rangi pia ni muhimu kwenye chumba cha
kulala-chagua rangi zisizokolea ikiwa wewe ni mtu wa asubuhi, au rangi zilizokolea
kama wewe ni wa kuchelewa. Taa ya chumba cha kulala ni muhimu kwa kuweka mood
au hali nzuri, na pia
Ikiwa huna sehemu kubwa,tafuta ideas ya kupamba chumba
kidogo kipendeze.Na vyumba vya kulala vya wageni vina mahitaji yao ya kipekee kwenye
kupamba.
Vyumba
vya watotoKwa mapambo ya vyumba vya watoto, bado ni mazoea ya kawaida
kutumia mandhari ambayo kwa ajili ya wavulana na wasichana, ingawa wazazi wa kileo
wameazidisha kutengeneza kufanya vyumba vya watoto kuwa vya kijinsia zaidi.
Chumba cha mtoto mchanga kina mahitaji yake ya kupamba, haswa
ambapo familia za vijana ambazo bajeti inaweza kuzingatiwa.
Bafu ya
kisasaJe! Unataka kubadilisha bafu lako kuwa spa ya kifahari? Angalia
ideas za bafu , pamoja kukifanya chumba kihisi ni mapumziko na cha kisasa, na jinsi ya kuchagua makabati,
tile, sinki, vioo, taa, na marembo. Katika bafu dogo, changamoto ni kuliremba
ili lionekane kubwa.
Ikiwa bafuni yako mpya inajumuisha mradi kamili wa kurekebisha,
tafuta vidokezo juu ya kufanya liwe zuri na la kisasa. Maamuzi mengine muhimu
yatakuwa kuchagua rangi na kuchagua sink zuri na marembo ya kuvutia.
JikoniJikoni kunaweza kuwa ni chumba cha gharama kubwa
kurekebisha, kwa hivyo unatakiwa kupanga kwa uangalifu mradi huo wako. Ikiwa urekebishaji kamili haitoshelezi
na budget yako,basi tumia njia rahisi kuleta muonekano,ikiwemo usafi wa kina
yaani deep cleaning,kurudia rangi,kuweka taa za kisasa,kubadili
makabati,kuongeza mapambo,kubadilisha sink,mifereji na mabomba.
Mwishowe, chaguo mapambo pekee na rahisi yanayoweza kufanya
jiko lionekane jipya kabisa.Na kwa kweli,kwa uchaguzi huu wa mapambo ni sehemu kuu ya uboreshaji wowote wa jikoni ya bajeti ndogo ya mradi huo.
Chumba
cha kulia(Dining Rooms)Meza katika chumba cha kula yaani dining room table ni
kitu muhimu humo,kwa hivyo chaguo na uwekaji wake ni muhimu katika mapambo.
Kuchagua fanicha sahihi inaweza kuwa muhimu sana kwa chumba kidogo cha kula.
Vitu vingine muhimu vya kuzingatia ni viti na taa za kuning’inia au chandelier — ambazo zote husaidia kufafanua
mtindo wako na kuweka sauti ya chakula.
Mwishowe, zingatia kwenye
mapazia na vitambaa vya kutandika mezani na marembo mengine.
Foyers
Foyer inapaswa kuwa nafasi ya kukaribishia ambayo huweka muonekano
wa eneo la kupumzika, lakini pia kuna
mambo mengi ya kuzingatiwa unapobuni na kupamba foyer yako.
Sakafu, vifaa vya
kuhifadhia, na aina ya marembo ni mambo muhimu katika kubuni foyer.
Ofisi ya NyumbaniUtakuwa na mahitaji tofauti ikiwa utaona wateja katika ofisi
yako ya nyumbani na kutumia nafasi hiyo kwa sababu za kitaalam. Lakini hata
ikiwa ni mahali tu kwako kwa ajili ya ,kufanya biashara ya na familia, kuna
vidokezo maalum vya kupanga na kupamba ofisi ya nyumbani. Pale ambapo bajeti
inazingatiwa, tafuta chaguzi za kuokoa pesa.
SHARE AND ENJOY !
0 comments:
Post a Comment