• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, October 12, 2021

Kupunguza uzito – Haraka na Nzuri

6:32 AM // by Kalma // No comments

Kupunguza uzito  – Haraka na Nzuri
Unasumbuliwa na uzito? Umechoka kuhangaika?Njia hizi za asili za kupunguza huo uzito kwa haraka bila ya kuhangaika.Kuwa na umbo lenye Afya .”
Uko tayari kupungua uzito bila ya kuhangaika?unaweza ukaifanya hiyo kwa mabadiliko ya kiafya kwa mlo na jinsi ya kuishi kila siku katika maisha yako.Unahitajia,kuwa muangalifu wa kuhesabu calories ambayo ni rahisi na itapelekea kujua kiasi gani unakula pindi usipohesabu ,na baada ya muda utajikuta umejijengea mfumo ambao unakua ni tabia yako ya maisha yako huwa tena ni mazoea….!!!Japokuwa kupunguza kwako uzito utakuwa  kwa kiasi kikubwa mno kwa kujumlisha na mazoezi,na unaweza usifanye pia.Tuangalie njia za asili hizi:
Njia za kupungua uzito kwa haraka
MAJIGlass moja ya maji au green tea kabla ya kula au mara mbili kwa siku.Maji yatachukua nafasi kidogo kwenye tumbo lako,husaidia kuhisi umeshiba hata ukila kidogo.kama itashindikana kunywa glass nzima, basi kunywa kidogo kila unapopata tonge la msosi.Kinywaji cha sukari pia ni kizuri badala ya maji.Weka kipande cha ndimu katika kinywaji chako utapata ladha nzuri.TABIA
1.Hesabu calories unayopata ili kupunguza mwili itakua rahisi kwa kupunguza calories ambazo zinapatikana mwilini mwako .Zitambue calories tokea katika milo unayokula mara kwa mara ,halafu utaijumuisha hizo calories mwisho wa siku yako.Adhimia
Dhumuni au nia ni kupungua pound moja kwa  wiki.Hii ni njia salama ya kupunguza uzito,na haihitaji kuilazimishia kupungua kwa haraka.Pound moja ni sawa na calories 3500,kwa maana hiyo unahitaji  kupunguza calorie 500 kila siku kwa wiki.kula chakula ambacho kinachukua muda kumeng’enywa au kusagwa kama vile matunda,mboga mboga,nuts,legumes na jamii ya nafaka.Kula vyakula vya asili vya kuchelewa kuyeyushwa  husaidia kujihisi umeshiba kwa kipindi kirefu,na vile vile itafanya  metabolism kuwa busy  pia.Achana na bites  ndogo.Pindi unapokula epuka kuwa na mlo mwingi mdomoni.Badala yake, tafuna chakula chako kwa mpangilio.Hii itakulazimisha kula taratibu,na utakua umepangilia mlo wako vizuri na itakua rahisi kwako kujua kirahisi pindi utaposhiba
RATIBA1.Kunywa chai au kifungua kinywa ni lazma yaani haina m-badala.Haiepukiki  na usijichanganye,kwa maana hautapunguza uzito kama utaepuka chai ya asubuhi.Hata kisomi inaonyesha kunywa chai ya asubuhi  hutengeneza metabolism  kwa ajili ya kufanya kazi kutwa nzima.2.Kula kwa mpangilio maalum.Ikiwa utaweza,jaribu kula milo yako kwa mida maalum hiyo hiyo kila siku.Kula kwa kufuata  ratiba husaidia mwili wako kujiandaa na kwa utulivu ambao utaruhusu kuyeyusha kiasi cha calories3.Kama tabia yako ya kula haitabiriki au huwa unaruka ruka milo ,mwili wako hua unawekeza calories kwa ajili ya dharura4.Usipendelee kula uangaliapo tv au mbele ya computer.Kwa kufanya hivyo utajikuta akili yako haipo zaidi kwenye kula.
 5.Epuka kula kwa mfadhaiko au stress.Stress au tamaa ya kula huweza kukuongezea uzito kwasababu utakuwa umekula kupitiliza.Kula pindi hauna njaa kali huongeza tani zisizo lazima za calories kwa diet yako ambayo huweza kuondolewa kirahisi na stress
6.Acha kula usiku mkubwa au mnene.Sababu hiyo, mwili wako hautaunguza calories nyingi pindi ulalapo,ni sawa na kula tu na kulala.
          Enjoy and Share !












Monday, October 4, 2021

10 Makosa ya kupanga sebule(living Room)

1:09 AM // by Kalma // No comments

10 Makosa ya kupanga sebule(living Room)

Sebuleni ni mahala ambapo watu watakujua au kukujadili ulivyo kimsingi hutakiwi kufanya makosa unapoiremba yaani designing.
Haya ni makosa ya kawaida ambayo yatachukiza sebule yako,unatakiwa uyaepuke!
Sebule ni moyo wa nyumba ambayo inaleta mvuto wa kwanza.Ni kiwakilishi ambacho sio cha moja kwa moja kinachokuwakilisha tabia na muonekano wa uhalisisa wako. Imezoeleka,pindi tunavyoremba sebuleni ,tunafikiria zaidi kwa vile tunavyovipenda na hamu na hutuangalii kiundani makosa tunayoweza kuyafanya pindi tunapoiremba.

Umuhimu wa kuangalia sebule ni pale marembo yanaendana na hali halisi ya sebule na muonekano wa hicho chumba.Kumkodi mtaaalam wa kazi hizo sio kwa ajili ya matendo,na hata hivyo ni ghali.Ni nyumba yako na wewe mwenyewe unatakiwa uwe m bunifu wa upambaji kutokana na nafasi ya sebule yako.

Hizi njia nzuri za kupamba sebule yako kama utajua makosa ya kawaida katika upambaji,tumia unachokijua katika upambaji na ilete tija.

Hii inaweza kuwa chochote cha muonekano muhimu kwa upambaji wako.Kosa kuu na muhimu sebuleni ni vurugu katika upangaji,ambao huonyesha kabisa kumepangwa bila mpangilio.Haijalishi ni nyumba mpya au imerekebishwa,kuwa makini na makosa haya ya kikawaida sana yanayofanyika katika kupamba sebule zetu.Mabadiliko madogo machache yanaleta muonekano wa mvuto tofauti.

Taa(Lighting)
Kama hazikuwekwa vizuri,itachukiza chumba chako.Hakikisha kuna taa kila upande.Kuwa na taa za juu peke yake nalo ni kosa pia.Tumia mwanga wa LED zilizofichwa kwenye siling ni wazo zuri .

Wrong Carpet 
Kila mara hakikisha carpet unazotumia zinaendana na size na shepu ya chumba .Kuwa makini wakati wa kuchagua rangi pia.
Mpangilio(Positioning) 


Hakikisha ya kuwa furniture zote ziko sehemu sahihi.Kuweka TV sehemu isiyo sahihi ni kosa lilozoeleka sana haswa katika kupamba sebule.

Sofa kukaa ukutani 

Kuweka sofa ukutani ni kosa la uharibifu.Kama unadhani itafanya sebule kuvutia,sio kweli ,unaiharibu sebule yako 
Rangi za giza ukutani(Dark Wall Colour)


Kupakaa rangi za giza yaani dark hufanya chumba kuonekana kidogo na mrundikano.Kama unapenda rangi za kukolea sana,tumia ukuta wa eneo moja kung’arisha,na tumia rangi za mwangaza kwa pande nyingine za ukuta.
Mpango wa kizamani
Japokuwa wanasema "old is gold",haibebi ukweli katika fashion za kizamani kwenye furniture.Kwahiyo,weka furniture zinazoendana na wakati za kisasa kupendezesha sebule yako.

Kupuuza sehemu muhimu katika chumba
Baada ya yote,sebule ni sehemu ya kualika wageni na ni sehemu ya kupumzika wewe mwenyewe baada ya mchoko na mihangaiko.Usipafanye ni sehemu ya kukaa kula,kunywa,kulala,kufanyia kazi,mazoezi,au kuweka meza yako ya ofisini.
Mapambo madogo dogo

 Kuzidisha sana mapambo sebuleni sio ndio kutavutia hii sio kweli.Kuipamba sebule kwa mapambo ya kisanii yaani art gallery nayo ni makosa yaliyozoeleka kwa watu wengi.Weka furniture chache na zipange sehemu nzuri ziendeane na chumba.
Pazia
Urefu wa pazia dirishani ni fashion ya kizamani (Window-length curtains).Tumia urefu wa pazia tokea sakafuni na magongo ya pazia nzuri halafu yawe marefu. 
Hii huleta muonekano mzuri sebuleni.


Share! Comments! Like ! 
Be hygienic and Smart !