10 Makosa ya kupanga sebule(living Room)
Sebuleni ni mahala ambapo watu watakujua au kukujadili
ulivyo kimsingi hutakiwi kufanya makosa unapoiremba yaani designing.
Haya ni makosa ya kawaida ambayo yatachukiza sebule
yako,unatakiwa uyaepuke!
Sebule ni moyo wa nyumba ambayo inaleta mvuto wa
kwanza.Ni kiwakilishi ambacho sio cha moja kwa moja kinachokuwakilisha tabia na
muonekano wa uhalisisa wako. Imezoeleka,pindi tunavyoremba sebuleni ,tunafikiria
zaidi kwa vile tunavyovipenda na hamu na hutuangalii kiundani makosa tunayoweza
kuyafanya pindi tunapoiremba.
Umuhimu wa kuangalia sebule ni pale marembo
yanaendana na hali halisi ya sebule na muonekano wa hicho chumba.Kumkodi
mtaaalam wa kazi hizo sio kwa ajili ya matendo,na hata hivyo ni ghali.Ni nyumba
yako na wewe mwenyewe unatakiwa uwe m bunifu wa upambaji kutokana na nafasi ya
sebule yako.
Hizi njia nzuri za kupamba sebule yako kama utajua makosa ya
kawaida katika upambaji,tumia unachokijua katika upambaji na ilete tija.
Hii inaweza kuwa chochote cha muonekano muhimu kwa upambaji
wako.Kosa kuu na muhimu sebuleni ni vurugu katika upangaji,ambao huonyesha
kabisa kumepangwa bila mpangilio.Haijalishi ni nyumba mpya au
imerekebishwa,kuwa makini na makosa haya ya kikawaida sana yanayofanyika katika
kupamba sebule zetu.Mabadiliko madogo machache yanaleta muonekano wa mvuto
tofauti.
Taa(Lighting)
Kama hazikuwekwa vizuri,itachukiza chumba chako.Hakikisha
kuna taa kila upande.Kuwa na taa za juu peke yake nalo ni kosa pia.Tumia mwanga
wa LED zilizofichwa kwenye siling ni wazo zuri .
Wrong Carpet
Kila mara hakikisha carpet unazotumia zinaendana na size na
shepu ya chumba .Kuwa makini wakati wa kuchagua rangi pia.
Mpangilio(Positioning)
Hakikisha ya kuwa furniture zote ziko sehemu sahihi.Kuweka
TV sehemu isiyo sahihi ni kosa lilozoeleka sana haswa katika kupamba sebule.
Sofa kukaa ukutani
Kuweka sofa ukutani ni kosa la uharibifu.Kama unadhani
itafanya sebule kuvutia,sio kweli ,unaiharibu sebule yako
Rangi za giza ukutani(Dark Wall Colour)
Kupakaa rangi za giza yaani dark hufanya chumba kuonekana
kidogo na mrundikano.Kama unapenda rangi za kukolea sana,tumia ukuta wa eneo
moja kung’arisha,na tumia rangi za mwangaza kwa pande nyingine za ukuta.
Mpango wa kizamani
Japokuwa wanasema "old is gold",haibebi ukweli
katika fashion za kizamani kwenye furniture.Kwahiyo,weka furniture zinazoendana
na wakati za kisasa kupendezesha sebule yako.
Kupuuza sehemu muhimu katika chumba
Baada ya yote,sebule ni sehemu ya kualika wageni na ni
sehemu ya kupumzika wewe mwenyewe baada ya mchoko na mihangaiko.Usipafanye ni
sehemu ya kukaa kula,kunywa,kulala,kufanyia kazi,mazoezi,au kuweka meza yako ya
ofisini.
Mapambo madogo dogo
Kuzidisha sana mapambo sebuleni sio ndio kutavutia hii sio
kweli.Kuipamba sebule kwa mapambo ya kisanii yaani art gallery nayo ni makosa
yaliyozoeleka kwa watu wengi.Weka furniture chache na zipange sehemu nzuri
ziendeane na chumba.
Pazia
Urefu wa pazia dirishani ni fashion ya kizamani
(Window-length curtains).Tumia urefu wa pazia tokea sakafuni na magongo ya
pazia nzuri halafu yawe marefu.
0 comments:
Post a Comment