• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Sunday, May 8, 2022

Ubunifu wa Matumizi ya Tea Bags

10:36 PM // by Kalma // No comments

 Ubunifu wa Matumizi ya Tea BagsUsitupe tea bags iliyotumika tena!

Tumia zaidi iliyotumika na usave hela na kupunguza taka.Kutibu macho na tea bags!Kuzuia  uvimbe wa chini ya macho kwa kutumia tea bags.Tumia kwa spa ujisikie vizuri ,itunze tea bags baada ya matumizi kwa dhumuni la kutumia tena. Furahia aromatherapy na athari zake za kujipumzisha .

Loweka miguu yakoChai ni kiburudisho chenye nguvu,huziba matundu na kuondoa ngozi chafu yenye mafuta.Kamua teabags iliypotumika na utumie mabaki ya mfano wa chai kwa kunawia miguu.

Chai nyeusi au black tea ni nzuri kwa kuondoa harufu mbaya miguuni, ambapo chai ya kijani hutuliza mwili nakuutia nguvu.

Umeungua?

Chai huponesha kuungua kwa jua, au kuchomwa na kiwembe au maumivu ya kuungua madogo madogo yatokanayo na kuunguzwa na sufuria au pasi.Hifadhi tea bags zilizotumika kwenye friji kwa muda wa wiki hadi mbili(njia nzuri na sahihi ya kuhifadhi kuweka kwenye mifuko yenye kufunga yaani air tight silicone bag,yenye unyevu),na utoe michache kwa ajili ya kutibu majeraha madogo kwenye ngozi yako.

Asidi za tannic ipatikanayo kwenye chai huzuia mtiririko wa damu kwenye cappilarries zako,inapambana na maumivu ya kuvimba au malenge lenge. Unaweza tumia tea bags kutibu kuvimba kulikosababishwa na kung’atwa na mdudu na hutibu vizuri  na haraka!

Kwa mapishi matamu ya pasta na grainZidisha utamu na ladha kwa kutumia tea bags pembeni mwa sufuria unayopikia pasta ,quinoa,wali,au aina yoyote ya nafaka.Manjano iliyosagwa ni tamu kwenye wali,Rooibos ni tamu ikichanganywa na oatmeal,na jasmine green tea ikichangnywa na yenye ladha kwenye pasta!

Huzuia kutu kwa sufuriaTannis husaidia oxidation,ambayo unaweza kutumia kuondoa kutu! Tumia kwa kufuta kutu kwenye pots,sufuria,na vifaa mbalimbali jikoni na utensils kwa kutumia tea bags kabla ya kuacha kukauka kwenye shelves.

Huzuia wadudu

Wadudu majumbani kama vile inzi na panya hawapendi harufu ya chai.Acha tea bags chache zikauke baada ya matumizi, weka ndani ya makabati.Aina ya mint ni nzuri kwa hili,na tea bags zilizotumika italeta athari zaidi ya harufu nzuri ndani ya kabati na itaua vijidudu.

Rutubisha mbolea yakoKunyunyizia kilichokuwemo kwenye tea bags iliyotumika kwenye mbolea itaongeza mchakato wa kuozesha zaidi,itasaidia mabaki ya chakula kuoza haraka.Ongeza majani ya chai katika mbolea yako husaidia kuzalisha bacteria ambao watazalisha rutuba sana kwa mimea yako,na hutengeneza mbolea kuwa ni yenye rutuba unapoongezea kwenye bustani yako au mimea nyumbani kwako.

kupambana na mafuta

Ukali wa chai wa hali ya juu pia hufanya kazi nzuri  kwa kuondoa mafuta .Tumia tea bags chache tia kwenye dishwasher pindi uoshapo  sufuria na bakuli zenye mgando wa mafuta,na tumia tea bags kama facial cleanser!


Share and enjoy!










Friday, April 8, 2022

Mahitaji ya Msingi ya Mapambo ya Kila Chumba Katika Nyumba Yako

10:17 PM // by Kalma // No comments

Mahitaji ya Msingi ya Mapambo ya Kila Chumba Katika Nyumba Yako

Unaweza kuwa na mtindo wa mapambo ya jumla uliochaguliwa kwa nyumba yako yote, lakini kwa mtindo wa jumla, kila chumba kina kusudio na mtindo wake. Jinsi matumizi ya chumba,kinatumiwa  na nani, inapaswa kuzingatiwa unapopanga kila chumba na kuchagua vifaa,mapambo, na uzuri na aina ya mapambo hayo.Zingatia mahitaji ya kila chumba na muhusika binafsi, na mapambo kulingana na nafasi ya hicho chumba. Mapambo ya nyumba yanapaswa kuonyesha hisia na ladha yenye maslahi binafsi, lakini lazima pia izingatie kazi maalum  ya hivyo vyumba.

Living rooms(sebule ya kupumzika na familia)

Sebule

Sebule zinaweza kutumika kwa  kazi nyingi, ni chumba rasmi kinatumika kwa kusalimiana na wageni,ni sehemu hata familia inatumia kusoma kwa Pamoja, ni sehemu ya burudani,kufurahia na kucheka Pamoja,na kucheza pia.Kwa nyumba za kisasa, sebule ni chumba kikubwa kimekuwa karibu na kuhusishwa Pamoja na jiko na dining area.Kubwa la kuzingatia ni kuchagua haswa mahala kwa ajili ya sebule au living room na haswa kuweka eneoau sehemu ya mazungumzo. Chaguo lako na mipangilio ya hiyo sebule yapaswa kiuzingatia akilini mwako.Hapo ndipo unaweza kusonga na mipangilio jinsi ya pa kuweka taa,sehemu ya zulia au rugs,marembo ya sanaa na mengineyo.

Vyumba vya kulala(Bedrooms)

Unatumia theluthi moja ya maisha yako kwenye chumba cha kulala, kwa hivyo unapaswa kuzingatia kwa uangalifu mikakati ya kupafanya mahali pazuri. Anza na kuchagua kitanda na fanicha zingine za chumba cha kulala. Wakati unaweza kuokoa pesa katika maeneo mengine,nunua godoro na mito bora na huo ndio  uwekezaji mzuri.Chaguo lako la rangi pia ni muhimu kwenye chumba cha kulala-chagua rangi zisizokolea ikiwa wewe ni mtu wa asubuhi, au rangi zilizokolea kama wewe ni wa kuchelewa. Taa ya chumba cha kulala ni muhimu kwa kuweka mood au hali nzuri, na piaIkiwa huna sehemu kubwa,tafuta ideas ya kupamba chumba kidogo kipendeze.Na vyumba vya kulala vya wageni vina mahitaji yao ya kipekee kwenye  kupamba.

Vyumba vya watotoKwa mapambo ya vyumba vya watoto, bado ni mazoea ya kawaida kutumia mandhari ambayo kwa ajili ya  wavulana na wasichana, ingawa wazazi wa kileo wameazidisha kutengeneza kufanya vyumba vya watoto kuwa vya kijinsia zaidi.Chumba cha mtoto mchanga kina mahitaji yake ya kupamba, haswa ambapo familia za vijana ambazo bajeti inaweza kuzingatiwa.

Bafu ya kisasaJe! Unataka kubadilisha bafu lako kuwa spa ya kifahari? Angalia ideas za bafu , pamoja kukifanya chumba kihisi ni mapumziko  na cha kisasa, na jinsi ya kuchagua makabati, tile, sinki, vioo, taa, na marembo. Katika bafu dogo, changamoto ni kuliremba ili lionekane kubwa.Ikiwa bafuni yako mpya inajumuisha mradi kamili wa kurekebisha, tafuta vidokezo juu ya kufanya liwe zuri na la kisasa. Maamuzi mengine muhimu yatakuwa kuchagua rangi na kuchagua sink zuri na marembo ya kuvutia.

JikoniJikoni kunaweza kuwa ni chumba cha gharama kubwa kurekebisha, kwa hivyo unatakiwa kupanga kwa uangalifu mradi  huo wako. Ikiwa urekebishaji kamili haitoshelezi na budget yako,basi tumia njia rahisi kuleta muonekano,ikiwemo usafi wa kina yaani deep cleaning,kurudia rangi,kuweka taa za kisasa,kubadili makabati,kuongeza mapambo,kubadilisha sink,mifereji na mabomba.Mwishowe, chaguo mapambo pekee na rahisi yanayoweza kufanya jiko lionekane jipya kabisa.Na kwa kweli,kwa  uchaguzi huu wa mapambo ni sehemu kuu ya  uboreshaji wowote wa jikoni ya bajeti  ndogo ya mradi huo.

Chumba cha kulia(Dining Rooms)Meza katika chumba cha kula  yaani dining room table ni kitu muhimu humo,kwa hivyo chaguo na uwekaji wake ni muhimu katika mapambo. Kuchagua fanicha sahihi inaweza kuwa muhimu sana kwa chumba kidogo cha kula. Vitu vingine muhimu vya kuzingatia ni viti na taa za kuning’inia au  chandelier — ambazo zote husaidia kufafanua mtindo wako na kuweka sauti ya chakula. Mwishowe, zingatia kwenye mapazia na vitambaa vya kutandika mezani na marembo mengine.

Foyers

Foyer inapaswa kuwa nafasi ya kukaribishia ambayo huweka muonekano wa  eneo la kupumzika, lakini pia kuna mambo mengi ya kuzingatiwa unapobuni na kupamba foyer yako. Sakafu, vifaa vya kuhifadhia, na aina ya marembo ni mambo muhimu katika kubuni foyer.

 Ofisi ya NyumbaniUtakuwa na mahitaji tofauti ikiwa utaona wateja katika ofisi yako ya nyumbani na kutumia nafasi hiyo kwa sababu za kitaalam. Lakini hata ikiwa ni mahali tu kwako kwa ajili ya ,kufanya biashara ya na familia, kuna vidokezo maalum vya kupanga na kupamba ofisi ya nyumbani. Pale ambapo bajeti inazingatiwa, tafuta chaguzi za kuokoa pesa.


SHARE AND ENJOY !







































 

Monday, March 21, 2022

SABABU YA KUPENDA KALE.

9:19 AM // by Kalma // No comments

KALE, 
Imeonekana kale imekua mtoto anaefahamika sana siku hizi.Miaka ya nyuma kidogo sikuwahi kusikia kale hili,na sasa ni mboga ninayoikimbilia mwanzo nikiingia sokoni.
Chakula tofauti huweza kuwa mtindo kwa kipindi fulani hivi,lakini binafsi sidhani kama kale ni kimoja wapo.Mboga hii ipo kwa muda sanaa.
Kama hujawahi nunua mboga hii ya kijani maishani mwako , nakusisitizia kubwa fanya haraka ununue ukijani huu.Lakini iwe baada ya kujua sababu tano hizi!

Ni chakula cha kuondoa sumu.

Kale ina  fiber na sulfur — zote ni kazi kuu katika ini lako,husaidia kutoa sumu mwilini. 

Vitamin A, vitamin A, vitamin A.

Kale ina zaidi ya 100% ya vitamin A inayotakiwa kila siku — 133% ndio haswaa,ambayo ni zaidi ya mboga nyingi za kijani zilizopo.
Vitamin A hufanya maajabu katika mfumo wa kinga mwilini,mpango mzima wa kuona,na husaidia kupambana na cancer kwa kudhibiti uzalishwaji katika seli zinazoweza sababisha cancer.

 Ni anti-inflammatory.

Vyakula vingi tunavokula,kama cereals,nafaka,vyakula vya kutengeneza,na vingi— vinosababisha inflammation katika mwili. Chronic inflammation huweza sababisha maradhi kama uchovu,kisukari,ugonjwa wa moyo,na cancer, kwahiyo ni muhimu kuepuka vyakula ambavo huweza kuleta madhara hayo.
kale kama anti-inflamatory properties ina  omega-3 fatty acids,ambayo inaaminika kuwa na nafsi kubwa katika kupunguza matatizo hayo.

 Ni rahisi kukua.

Sijawahi jaribisha kuupanda mwenyewe.lakini chanzo changu kinanilazimisha nifanye hivyo.Japo kale huota vizuri sahemu za baridi,pia huweza kukua vizuri hata kwa hali yoyote ya hali ya hewa.kama huna garden nje kwako waeza panda pia kwenye pot,La msingi iwe na 6 inches, ya nafasi katika pot kuruhusu kukua. Kale ni pretty skilled katika kupambana na wadudu(disease)- ni ndoto ya mwanzo ya kuwa na garden!.
 Kale chips ni tamu.

Kama hujawahi jaribu kale chips,tafadhali fanya nyumbani kwako kwa mara ya kwanza.
Ni ya ajabu na rahisi kutengeneza,na tafuta soko zuri utayoipata ikiwa fresh huwa yenye ladha nzuri na tamu,inaweza shinda ya kutengeneza mwenyewe nyumbani,ila kwa kwetu huku sina uhakika kama yapatikana iliotengenezwa.

Chips za kale :

Jinsi ya kuandaa:

 Preheat oven kwa 350 degrees F.katakata vipande vya kale ilo lowekwa vya size tu sio vikubwa sio vidogo,changanya na olive oil,tia chumvi na ya vitunguu thom.weka kwenye sahani ya oven yako kisha oka kwa 15 dakika(mpaka ziwe crispy) na inakua kama pie,nzuri ,tamu ladha yake,na virutubisho kibao.

Hizo ni tano katika nyingi zao katika lishe na afya yako tokea mmea kale.Tupia nyingine tujenge afya zetu na familia kwa ujumla!!



Enjoy and Share !