• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, February 4, 2014

KUONDOA WEUSI CHINI YA MACHO.

10:31 AM // by Kalma // No comments


 Kulala na kupumzika ni muhimu kwa kuwa na afya nzuri na muonekano bomba.Kuanzia kwenye kuboresha akili,kuongeza ufanyaji kazi mzuri wa moyo,kuongeza ubunifu katika ufanyaji wako wa kazi,faida zake huwa hazina mwisho.Lakini sio rahisi kuupata usingizi wa kutosha kwa kila usiku-na wakati mwingine huonesha usoni chini ya macho huitwa(miwani)na puffy eyes.Japo kuwa tiba yake ni kutibu chanzo cha hilo tatizo ambao ni usingizi na kupumzika vya kutosha.Hizi njia za asili chache,hufix macho ya usingizi….kwa usiku pindi haukupatikana usingizi kama ulivyotakiwa katika mipango.
Viazi.
 Viazi vina asili ya enzymes wanaong’arisha ngozi huitwa catecholase, ambao husaidia kufifiza weusi chini ya macho.Weka kiazi kibichi katika hiyo sehemu ya machoni unaweza kukikata vipande vidogo vyembamba au kwa kusaga kupakaa kama uji.Weka kwa 30 dakika kisha toa,osha uso kwa maji ya kawaida tu ukihisi ulazima.


 Mint leaves
Pakaa majani ya mint kwenye sehemu hiyo ya machoni huleta kuwakwa moto ile kama ukali wa mfano vicks,huongeza msukumo wa damu katika hiyo sehemu na kuondoa weusi.Rahisi ponda majani ya mint kidogo na pakaa machoni hapo kwa dakika 5.Osha uso kwa maji ya kawaida yaani cool water .Unaweza tumia majani ya mint ukachanganya na asali au olive oil kabla hujapakaa kwenye macho .Nayo ni kwa dakika tano . 

Tea bags
Caffeine ndani ya  caffeinated teas,kama chai ya kijani (green tea)kwa muda kukazisha ngozi chini ya macho kuiachia mishipa ya damu kuondoa maji yalozidi, pindi  herbal teas (kama chamomile)huondoa kuungua na m-badiliko wa rangi na kuondoa udhia .Kupaakaa,weka tea bags mbili ilowanishe kwenye chai na  uiache zipoe.Weka kila tea bag moja kwenye macho yako yakiwa yamefungwa kwa kuilaza kwa dakika 15 pindi umekaa mkao wa kujilaza.


Rose water
Rose water ina vitamins kama A na C, ina antiseptic, anti-inflammatory na anti-bacterial pia,na vile vile ni kama balancing effect,ni chaguo zuri la kutumia kwenye ngozi.Unapakaa hayo maji chini ya mcho kwa dakika 10 kwa kulowanisha pamba na kutumia kupakaa.




Matango
Weka vipande vya  matango ya baridi kwenye kila jicho husaidia kuondoa uchovu ,puffy eyes kwa kuyapooza kwake,na husaidia kulainisha ngozi ya machoni mwako.La kuongezea,matango hufanya kazi ya toner na kung’arisha uso,husaidia kuondoa mabadiliko ya rangi katika ngozi.Wengine husema kutumia matango machoni ni tiba ya kizamani lakini hiyo ni wewe kama utaiweka akilini,lakini wengine na mimi nikiwemo ni njia tuliyojiaminisha kuwa nzuri na inasaidia. 
Ni muhimu kunote kwamba weusi chini ya macho husababishwa na upungufu wa usingizi,na sio kama ni lazima hiyo kuwa ndo chanzo. Allergies, matatizo ya pua(nasal congestion), na stress ni sababu za kawaida, nazo pia. Kuligundua tatizo itakupa njia rahisi ya kutibu kwa urahisi na ndani ya muda.



0 comments:

Post a Comment