Kuna mtu alinitumia ujumbe mfupi juzi
kati hapa kwamba, dokta wake kamwambia aache kutafuna chewing gum na kufyonza pipi
hizi,ambayo ilikua ikimsababishia tumbo kujaa gesi.(Nikaiangalia hiyo nikaona
na kutokana na Mayo Clinic,yote ni sawa na ni kisababishi kikubwa kwa watu
wengi tu kwasababu unavuta hewa…kufyonza mrija pia ni sababu ya
gesi).Anyway,aliniuliza kama najua tiba yoyote ya asili ambayo inaweza kuwa
kitunguu au kituungu thoum ili aondoe harufu ya mdomo, tokea apo hivyo ndio
viungo anavyovipenda yeye.(mimi mwenyewe nimeanza kutumia hizi).
Kwahiyo nikafanya uchunguzi
,kujaribisha mawazo mengi mengi tofauti,nikaona nisiwe mchoyo nanyi
muyajue.Nahisi tumbo langu limeshachoka na hizi kahawa nazokunywa!Labda
utafiti mwingine ujao utaangalia jinsi ya kutoa caffeine baada ya kuwa nyingi
tumboni,sijajua athari kuhusu kama vitunguu,tangawizi ,viungo,n.k.
CHAI YA KIJANI(GREEN TEA)
Green tea ni tajiri wa polyphenol,ina antioxidant yenye
nguvu sana ambayo itaondoa plaque kuenea kwenye meno yako. Polyphenols imeonekana
kuzuia bacteria kukua katika mdomo.Kwahiyo kufyonza chai ya kijani husaidia
kuondoa harufu chafu ya vitunguu.Spinach ,chai ya rangi,apples na mushrooms pia
nazo zina polyphenols, unaweza pia kutumia aina hii ya vyakula na kinywaji
baada ya kujiona mdomo unatoa harufu iliosababishwa na mlo wako.Mimi binafsi
napenda chai labda inanisaidia.
MATUNDA NA MBOGA FRESH – Fiber-nyingi hupatikana kwenye matunda na mboga, husaidia
kuondoa harufu mbaya ya mdomoni(na kujisikia umeshiba muda wote,ambayo husaidia
kupunguza uzito).Fiber kwenye vyakula vingi husaidia kutengeneza mate,ambayo
husaidia kusafisha plaque zinazojijenga.Fiber imo kwenye vyakula kama
cerely,apples,na karoti.Enzymes wa asili wanaptikana kwenye apples
,berries,nanasi,na kiwi huondoa sulfur compounds na huondoa harufu mbaya ya
mdomoni.Mboga zenye vitamin C,kama red bell peppers na broccoli husaidia
kutengeneza mazingira ya kuzuia bacteria wa mdomoni,pindi inapoliwa hufanya
kazi hiyo.Hivi vyakula pia husaidia kuondoa mabaki ya vyakula katika meno pia.
MAZIWA– Kufyonza maziwa huondoa harufu mbaya ya mdomo kama utakunywa kabla au wakati wa kula (according to a Journal of Food Science 2010
study). Mafuta katika maziwa huyeyusha sulfur wakati maji kwenye maziwa huwa
kama kisuuza mdomo.Siwezi kula maziwa bila cookies sa sijui hii inafanya kazi
hapa.Kunywa maziwa baada ya kutumia chakula chenye viungo hii haisaidii kuondoa
harufu mbaya.
MKATE –Kukosa carbs katika mlo wako huchangia harufu mbaya ya
mdomo.Kula kipande cha mkate husiadia kuleta harufu nzuri mdomoni.Baada ya kula
kipande cha kitunguu,kipande cha mkate kitasaidia
kuondoa harufu mbaya mdomoni,lakini ladha hubakia kwenye ulimi.Hata hivyo ukila
kipande cha mkate huondoa hiyo harufu na utakua umehifadhi calories kwa
matumizi mengine.
MITI SHAMBA FRESH – Kabla ya mouthwash hazijajulikana,watu walikuwa
wakitafuna miti shamba kuondoa harufu mbaya.Miti shamba ina chlorophyll,ambayo
huondoa harufu na uchafu.Aina ya mitishamba mizuri na fresh ni mkama parsley,mint,binzari,basil,rosemary,thyme,tarragon
na cilantro.Kama chakula chako kitakua na aina yoyote ya miti shamba tafuna kwa
kuondoa harufu.Baada ya chakula pia unaweza tafuna yoyote ambayo unao uwezo wa kuipata na huondoa
harufu mbaya mdomoni.
HARADALI(MUSTARD) – Ok,hii ni ngumu kujaribu lakini pia ijaribishe.Kuna njia
mbili tofauti zipo katika haradali( mustard).Kwanza,chukua kijiko cha chai cha haradali
weka mdomoni,sukutua kisha tema kwa dakika chache.Kisha chukua nusu kijiko cha
chai cha haradali meza itaenda tumboni ambapo itaenda kuua harufu ya vitunguu
thoum na vitunguu mwilini.Njia ya pili ,kuchanganya vijiko vya chai viwili vya
mafuta ya haradali na chumvi.Kisha weka mdomoni huku ukichezea ndani ya mdomo,tema
mate yatayojitokeza na iache haradali kwa dakika 30 .
MAZIWA YA MTINDI –Ounches sita za maziwa ya mtindi husaidia kuondoa harufu
mbaya na uchafu ambayo husababisha hydrogen sulfide na huua wadudu wa mdomoni. Tumia
kwa kunywa maziwa ya mtindi kila siku.
MBEGU & KAHAWA(COFFEE BEANS) –Kutafuna karafuu,au hiliki,shamari(fennel),mbegu za anise,
mara moja huondoa harufu mbaya mdomoni.Kama unahisi unatatizo la aina ya
vyakula kwa sababu ya meno,kuwa makini na hizi pia.Kula kahawa(coffee beans)
ilo kaushwa ni nzuri zaidi na huondoa harufu kwa haraka zaidi.
NDIMU – Kulamba ndimu au kutafuna ganda dogo la ndimu ni nzuri
kwa kuondoa harufu mdomoni pia.Lakini juisi ya ndimu ina acid na huweza kuwa
mbaya kwa meno yako,husababisha meno kupata ganzi.
JUISI YA SIKI YA APPLE – Ni nzuri!Sio tu kwa ajili ya kusukutua ½ kijiko cha chai
cha juisi ya siki ya apple iliochanganywa na kikombe cha maji,husaidia harufu
pia,huondoa harufu ya vitunguu na huwa ni ladha pia ulimini.Kuchanganya na
maji,huondoa ule ukali wake na utausikia mdomo uko vizuri mwepesi.Naifanyia
kazi post zijazo kuhusu juisi ya siki ya apple na matumizi yake.
BAKING SODA – Kutengeneza mouthwash ya baking soda na maji ni tiba ya
asili ya muda mrefu.Tumia hii kwa kusukutua mara moja kwa siku.
MAJI –Pindi unywapo maji baada ya kula
vitunguu au vitunguu thoum unaweza kuhisi haiondoi harufu na uchafu hapo
hapo,kunywa maji mengi kwa mpangilio au utaratibu maalum husaidia mdomo kuwa fresh na harufu nzuri muda wote.Maji
yanasaidia kuondoa bacteria wa kwenye chakula na huzidisha utengenezwaji wa
mate kwa wingi,na pia huwa kama ni kiosha au kisafisha mdomo cha kudumu. Of course kupiga mswaki meno yako,mouthwash,flossing na kusafisha ulimi utaweka mdomo wako kuwa na harufu nzuri na fresh na pia huwa oral hygiene mzuri.
Harufu mbaya ya mdomo inakera
ukiangalia vyakula vyenyewe hivi aina za viungo na uzembe wa usafi unaoweza
sababisha hata ukavu wa mdomo,vijidudu vya kwenye fizi, na vijidudu.Kama
utagundua tatizo hili la harufu mdodmoni inaendelea,muone daktari wa meno kwa
tiba na ushauri zaidi.
0 comments:
Post a Comment