Tips bora za kuhudumia mwili
Kwa kiasi kikubwa sana tunaangalia zaidi urembo wa uso na muonekano,wakati kuna sehemu huwa zina uvivu kuzihudumia katika miili yetu.Japokua make-up na marembo mengine unawezesha muonekano wetu,labda na mpaka mara moja moja kujiangalia zaidi miili yetu,matokeo ya mwishoni hayatupambi muonekano wetu sanaa.Kwahiyo hizi ni Tips chache za kuujali mwili wako katika kujihakikishia muonekano mzuri na wa kuvutia wa mwili zaidi ndani na nje.
Tips za kuujali mwili kwa mwanamke.
1. kuondoa weusi katika kiwiko na magoti:
- Kamua ndimu kupata juisi yake
- Kata vipande vya ndimu
- Sugulia hizo katika weusi /sehemu yenye rangi kwenye kiwiko na magoti
- Acha kwa dakika 20
- Lowesha taulo ndani ya maji ya moto kisha sugulia kwenye hizo sehemu.
2. kulainisha mng’ao wa ngozi:
- Chukua rose water kijiko kimoja cha kula,kijiko kimoja cha glycerine na kijiko kimoja cha kula cha juisi ya lime.
- Changanya pamoja weka kwenye chupa
- Pakaa kila siku kwa muda wa nusu saa kabla ya kuoga au muda wa kulala hufanya ngozi kuwa laini na ya kung’aa.
3. kuondoa chunjua(warts)kuzunguka vidoleni:
- Chukua viazi kizima kikate vipande pande
- Pakaa maji yake kuzungukia hilo eneo la kucha kunako chunjua (hukausha ngozi ilo haribika)
- Tumia kipande cha pamba,sugulia kwa upole
- Osha baada ya dakika kumi
4. kuondoa puffy macho ya uchovu:
- Chukua kipande cha pamba na rose water
- Lowesha pamba kwa maji ya rose kisha weka hapo machoni
- Weka kwa dakika 20
- Lala chali ukiwa umepumzika
- Husaidia kuondoa macho yenye uchovu na kuleta kupumzika
5. kuifanya ngozi laini:
- Vijko 5 vya chai vya olive oil na 50gm paste ya papai
- Changanya pamoja
- Pakaa kwenye sehemu kavu za ngozi
- Fanya hivi mara mbili kila siku kupata ngozi asili na laini
6. mask ya uso kuondoa mikunjo kwenye macho:
- Vijiko vya chai 3 vya maziwa na 3 vya chai vya asali
- Changanya pamoja
- Pasha kidogo huo mchanganyiko
- Pakaa kuzunguka machoni kwa dakika 30
- Osha kwa maji ya uvuguvugu
- Hii ni njia ya asili ya kupunguza na kulinda na mikunjo ya machoni au chini ya macho
7. Conditioner ya asili ya nywele:
- Chukua maziwa yanapendekezwa yawe baridi
- Kabla ya kuoga,pakaa mchanganyiko huo kwenye nywele tumia chanuo kuzichana ,au vidole vyako kuzichambua chambua au spray bottle
- Acha kwa dakika 30
- Osha kwa shampoo unayoitumia
- Maziwa huwa kama conditioner ya asili,hufanya nywele zako kuwa soft na silky
8. kupunguza madoa meusi:
- Chukua kikombe kimoja cha curd na yai moja
- Changanya pamoja
- Pakaa usoni, na sana sehemu yenye doa
- Acha kwa saa moja
- Osha uso na maji
- Husaidia kutakatisha na kupunguza madoa meusi usoni
- Hufanya ngozi ing’ae kiasili
9. kupunguza m-ba:
- Chukua ua la hibiscus na lisage kupata juisi yake
- Pakaa kwenye ngozi ya kichwani ,na zaidi sehemu zenye m-ba
- Acha kwa saa 1-2
- Osha na maji baridi
- Fanya hivi mara mbili kwa wiki kupunguza m-ba
10.kulainisha mikono migumu na nyayo:
- Chukua nusu kikombe cha curd na nusu kijiko cha chai cha vinegar
- Changanya pamoja
- Sugulia mikononi,viganja na nyayo
- Iache kwa dakika 5-10
- Osha kwa maji ya kawaida
0 comments:
Post a Comment