VIUNGO,
Ni mpenzi wa viungo sana,na jiko langu limerembwa na aina tofauti tofauti pia ya viungo.Zinavutia rangi zake,na vyenye mvuto wa asili harufu yake yenye kuleta hamu ya kula.
Visiwani haswa Zanzibar, Tanga siwezi kuiacha Morrocco hutumia sana viungo,Sio tu kuongeza ladha ya chakula bali pia vina faida nyingi za kiafya na urembo pia.Ni kitu kizuri kujifunza vipi viungo vitatusaidia katika maisha yetu ya kila siku.
Chumvi,pilipili,tangawizi,manjano,(turmeric),pilipili mbuzi(paprika),jira au binzari nyembembe au uzile(cumin),zafarani(saffron) .
Hizo chache hapo juu huenda zikatusaidia katika afya zetu….
Tangawizi
Njano isokooza rangi yake na harufu kali,inasifika kuwa ni kiungo kizuri chenye faida nyingi kiafya.Kama unahisi uchovu,au tumbo limevurugika,tangawizi husaidia kutoa hayo udhia.Kuanzia mmeng’enyo chakula mbaya au uliokuwa slow,kutibu joints pia,tafuna kipande kidogo au weka kwenye kinywaji cha moto italeta nafuu.
Manjano (Turmeric)
Hiki ni kiungo kimojawapo kinatumika sana kipindi cha baridi kali huleta ujoto na harufu yake nzuri.Manjano ni yenye asili ya anti-inflamatory hutumika sana kwenye dawa za ayurvedic.Husaidia kuboost immune system,na pindi usikiapo baridi kali mwilini.Na hutumika kupakaa usoni na ni kujisugulia mwilini,hutoa uchafu,hufanya ngozi kuwa laini na hung’risha rangi ya ngozi kuwa yenye mvuto.huleta rangi kwenye chakula.
Pilipili mbuzi au boga(Paprika)
Hii ina lishe nyingi za kiafya katika mwili wetu,na sana Vitamin A.Kijiko cha chai kimoja cha rangi nyekundu ina zaidi ya 100% ya mahitaji ya kiafya mwilini ya kila siku.Kama vitamin A husaidia kuona,huongeza madini ya chuma ambayo hutia nguvu mifupa.
supu yenye paprika.
Jira (Cumin)
supu yenye paprika.
Jira (Cumin)
Jira ina nguvu sana,huwa ni kama badala ya chumvi.Ina kiasi cha Sodium kidogo,tumia zaidi hii badala ya chumvi husaidia kushusha blood pressure,ni yenye ladha nzuri katika chakula.Jira ni chanzo kizuri cha Vitamin B,ambayo inasaidia kuleta usingizi.Jaribu kula ndizi iliyochanganywa na jira kabla ya kwenda kitandani kama una shida ya kupata usingizi.
Zaafarani(Saffron)
Japokuwa hiki kiungo ni cha gharama ,ni kizuri kwa chenye afya nyingi nyingi.Husaidia digestion na inflammation,unaweza ukatumia zaafarani kwa njia nyingi na kuweka kwenye chakula pia.Tengeneza mask ya maziwa ya zaafarani,chukua zaafarani weka kwenye maziwa mabichi ambayo hayajachemshwa.Kisha iache zaafarani kwa saa mbili kabla ya kuyatumia,maziwa yatakuwa rangi nyekundu.kisha pakaa usoni,iache kwa dakika kumi10 kabla ya kuosha uso.Kiungo hiki husaidia kusafisha uso na ngozi iliokauka na huondoa madoa!
Cake ya strwabery na zaafarani.
Cake ya strwabery na zaafarani.
0 comments:
Post a Comment