• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, May 27, 2015

VYAKULA VINAVYOBORESHA KUMBUKUMBU

7:25 AM // by Kalma // No comments

Ni jambo zuri kujua aina ya vyakula vinathamani zipi katika miili yetu.Chakula ni jinsi tunavyokitumia sisi wenyewe ,na bora zaidi kukiangalia faida ya chakula,kama ni chanzo cha nguvu mwilini mwetu.Tukiwa na ufahamu wa faida za chakula itatusaidia kula vyakula vizuri zaidi katika ubora wa afya,kwa kujisikia tuko vizuri,kiafya na kiakili pia.Nilikua naangalia njia za kukuza na kuboresha kumbukumbu,nilichogundua ni kwamba vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha hili.La msingi tule vyakula vyenye kuujenga mwili vizuri.
 Chai(tea)
Faida ya chai huonekana kama ina mwisho-lakini huathiri kumbukumbu chai imehusika.Antioxidants inayopatikana kwenye chai ina  polyphenols –huboresha kumbukumbu,na hufanya kazi ya utambuzi katika akili.Chai ya kijani na nyeusi inazuia kazi ya enzymes wawili (acetylcholinesterase na butyrylcholinesterase), ambao wanashabihiana na ukuaji na maendeleo ya vijidudu vya Alzheimer.Kama unataka kuboresha kumbukumbu tumia sana chai,na ni vizuri ya kutengeneza mwenyewe,unaweza kuweka viungo vya asili unavovipenda na chai yako ikawa tamu ladha yake.




Rosemary
Kisomi zaidi ilionekana hata harufu tu ya rosemaru huboresha kumbukumbu ya muda mrefu na mfupi pia,na hata mahesabu ya kiakili,kutokea na compounds zinazopatikana kwenye harufu yake.Unaweza ukapanda nyumbani kwako ukawa unaipata harufu hiyo au kwenye chakula kwa kutumia mimea inapatikana kwenye olive oil.


 Kiazi sukari(beets)
Vyakula vyenye Nitrate nyingi kimojawapo ni kiazi sukari,huongeza msukumo wa damu,hufanya akili yako kuwa nyepesi na sharp na hulinda na matatizo ya akili.

 Mbegu za alizeti
Karanga na mbegu inasambaza mwilini omega-3 fatty acids,ambayo ni maarufu kwa kuboresha akili.Mbegu kama za alizeti ina chanzo kizuri cha vitamin E, husaidia kulinda seli za mishipa ya akili isiathiriwe.Kula karanga na mbegu hujenga afya na mwili pia.

Vyakula vyote ni vizuri kupata katika mlo wako wa kila siku.Uwezo wa kuboresha akili ni sehemu ndogo ya ujumla ya faida za kiafya mwilini.Tuweke mikakati ya kuangalia chakula tunavyokula na familia zetu kiwe ni njia mojawapo nay a muhimu katika kujenga afya,kutia nguvu,na tuwe wenye furaha katika maisha yetu ya kila siku. 


 cake yenye mbegu za alizeti.
 mbegu za alizeti zilorostiwa.


SHARE !

0 comments:

Post a Comment