• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, August 6, 2020

Kusafisha vitu vya stainless Steel

7:57 AM // by Kalma // No comments

Kusafisha vitu vya stainless Steel 
Najiuliza vipi vitang’aa vitu vya stainless steel.kwa vipi vibaki kuonekana vipya na mng’ao bila michoro ya vidole na uchafu?Kama nyumba yako ni kama yangu,imezungukwa na aina tofauti ya vitu vya stainless steel.
Nimejaribu kila aina ya brand tofauti masokoni na nikapata jibu kwamba,haufanani usafi wa kila stainless steel, Na sio kila brand husafisha stainless steel.Tofauti ya brand za usafi zinatumika na utofauti wa aina ya stainless steel na zinafanya kazi tofauti kulingana na unachosafisha.Jua kila aina ya stainless steel ina jinsi ya brand yake ya kusafishia.Ndio maana nikatafuta suluhu ya kitu ambacho kitasafisha aina zote za stainless steel.
Njia nzuri ya kusafisha stainless steel 

Unachotakiwa kwanza kitambaa LAINI kwa ajili ya kufutia kifaa chako.Nacho ni kinatambulika kama microfiber cloth – maarufu sana hiki, hiki ni mama wa kufutia nyumbani.Hata ukibisha microfiber ndio uhakika wa usafi na mng’ao kwa vifaa vyako.Na inasafisha kweli!
Katika pita pita yangu,kujaribu na kujaribu,nimekuja na aina hizi tatu ya jinsi ya kusafishia vifaa vya aina hii-aina zote inatumia aina hii ya kitambaa.
Hizi hapaa:
 Maji 
  • White vinegar 
  • stainless steel cleaner 
Njia nyingine ya kujaribu :
club soda

 Olive oil

 Baby oil

  1. club soda –pulizia na pangusa kwa kitambaa
  2. olive or baby oil – pakaa kwenye kitambaa kikavu na pangusia
  3.  window cleaner – kuna watu wanaiamini hii njia-kwa ushauri zaidi tumia non-ammonia window cleaner  
Jinsi ya kusafisha: 
Tumia maji au cleaner kwenye kitambaa na safisha haraka haraka na kusugua mauchafu.Usiruhusu maji au sabuni ikaukie kwa kifaa kabla uchafu haujaisha.Aina hii ya kitambaa ni kwa ajili ya vifaa vya stainless steel.
Pindi unaposafisha nenda moja kwa moja kwenye uchafu husika kwa hicho kifaa.Kwasababu uchafu unaeza ukahamia kwingine upatapo maji.Njia hizi husafisha vizuri sana.Weka karibu kitambaa chako hiki iwe rahisi kwako unapo kihitajia.

HIFADHI KWA DRAW LAKO LA JIKONI AU NING’INIZA PAMOJA NA VITAMBAA VINGINE VYA USAFI ,NJIA NZURI NA RAHISI VIWEKE PAMOJA NA FAGIO NA MADEKIO YA USAFI.

Una njia nyingine ya kusafisha vifaa vya stinless steel?leta dondoo tujumuike pamoja!

0 comments:

Post a Comment