Upambaji ndani chumba cha watoto
Kupamba chumba cha watotoni changamoto kubwa kuliko kujenga
nyumba nzima.Kila mtoto yuko tofauti;na kuiga vilivyozoeleka sio chaguo
zuri,inayokuja kupamba chumba cha
watoto.Hata hivyo unaweza kupendelea kufanya kile unachokipenda endapo
una tips mikononi mwako.Ukachukua mawazo na fikra tokea kwa designs
zilizokuwepo.Kupangilia unachokitaka wewe kutokea kwako mwenyewe utapata chumba
kizuri na utofauti wa kipekee.Chumba cha watoto ni sehemu ambayo watoto wako
wanatumia muda wao mwingi wakiwa ndani yaani indoors.Kwahiyo design inatakiwa
iwawezeshe kujisikia vizuri,huru wenye nguvu na kujiamini.Haijalishi mpango au
ideas gani utatumia,kuu ni ubunifu na mpangilio mzuri.
Washirikishe watoto wako kuliendea hilo na wape nafasi huru
kuchagua aina za designs pia.Zingatia umri wa watoto, wako wangapi wanashare
hicho chumba na jinsia ni muhimu.
Hapa,tutazungumzia zaidi njia nzuri ya kupamba chumba cha
watoto.
Rangi
Unapendelea muonekano wa nyeupe au kijivu yaani grey
nyumbani kwako.Lakini,pindi unapodesign chumba cha watoto,la muhimu kulitilia
mkazo ni rangi.Hii ni muhimu kwa upambaji wa chumba cha watoto itafanya eneo
lionekane hai na zuri.
Eneo la hifadhi la
kutosha
Nafasi ya kutosha
Nafasi itiliwe mkazo zaidi kwa muonekano wa kipekee,usisahau
nafasi ya stoo ya kutosha.Watoto
wanavitu vingi vya kuhifadhi,pangilia kuanzia madaftari na michezo
yao.Kwahiyo,hakikisha una nafasi kubwa kwa ajili ya kuhifadhia na kupunguza
msongamano ndani ya chumba.
Aina ya kitanda
Siku hizi,kuna aina nyingi za vitanda maalum kwa ajili ya
vyumba vya watoto tu.Kama unataka kitu tofauti,tengeneza kwa wataalamu.Hii peke
yake itabadili muonekano wa chumba na watoto kwa hakika watapenda kuwa na kitu
tofauti na fashion za kiasili au asilia. Bunk bed pia ni nzuri kuchagua.
Tengeneza picha za sanaa
Tengeneza cha kuvutia cha kisanii kilichopangika vyema
kabisa ni njia nzuri ya muonekano wa kuvutia chumbani kwa watoto.Hii
itawasaidia kujifunza zaidi,na unaweza kuwapa motisha waunde vitu vyao vya
sanaa.Faida kuu ipatikanayo hapa utakua umebadili muonekano kwa gharama ndogo
sana .Mimi napenda chumba kikubwa bila aina za sanaa yoyote.
Wallpapers
Tumia wallpapers chumbani kwa watoto ni kitu kizuri
kitabadili muonekano mzima wa chumba hicho.Na ni m badala rahisi na flexible,ni
rahisi kubadili badili wakati wowote utakavyo.Hii husaidia chumba kuwa
fresh,bila ya kuwabore watoto.Na hii ni moja wapo ya mpango wa kupamba vizuri
chumba cha watoto.
Sehemu ya kuchezea
Eneo la kuchezea ni
muhimu pindi unapopamba chumba cha watoto .Weka mazingira ya eneo la kuchezea
kwa watoto wako.Wakati unafanya hivi,waangalie machoni mwao na uwape kipaumbele
kwa mapendekezo yao na kinachowavutia au hitajio lao.
0 comments:
Post a Comment