Kusafisha microwave
Mnato wa chakula kwenye microwave unaonekana vibaya,harufu
sio nzuri,na hupunguza thamani ya microwave jikoni.Kwa bahati,microwave ni
rahisi kusafisha ukijua.
Vinegar
Glass inayofaa
kwa microwave au bakuli yenye nusu maji changanya na 1 kijiko cha kula cha
white vinegar.Tia ndani ya microwave.
Washa kwa dakika 5.Utahitaji dakika chache kwa microwave
zenye nguvu zaidi,wakati ukisubiria hapo hapo kwa mara ya kwanza.Njia hii
itayeyusha ukuta wa microwave na kugandua vilivyogandia.
Toa kama ni glass au bakuli,tumia kitambaa safi kwa kufutia
au paper towel.Ondoa sahani ile ya kioo osha kama chombo kawaida,tumia
dishwasher kama una muda.
Ndimu au Limao
Kata ndimu au limao
nusu.Tia maji nusu kijiko cha kula kwenye bakuli na vipande vya ndimu.Washa kwa
dakika moja au ndimu imekua ya moto na uchafu umeganduka.Tumia kitambaa safi
kufutia.Osha sahani kama kawaida.
Kwasababu ndimu imechemka husafisha vizuri kiasili kwa
kibebeo (dustbin)cha taka za jikoni zikate vipande vidogo dogo zaidi na osha na maji
mengi.
Sabuni ya vyombo
Chukua bakuli tia maji ya moto ,tia sabuni ya vyombo kwa
kiasi unachohitaji.Washa microwave kwa dakika moja mpaka uchafu uyeyuke.Tumia
kitambaa au sponji safi kwa kufuta.Unaweza tumia baking soda ina harufu nzuri.
Window Cleaner
Changanya maji na
window cleaner kwa maji ya uvuguvugu.Mchanganyiko huu utasafisha ndani na nje
ya microwave.
Futa ndani kwa kuloweka sponji au kitambaa ndani ya
mchanganyiko huo,toa sahani ya microwave safisha ndani na nje hadi uchafu
uishe.Hakikisha microwave haijawashwa pindi usafishapo.
Loweka madoa kwa window cleaner kwa dakika 5 kabla ya
kusugua.Suuza kitambaa au sponji kwa maji safi na ufute na window cleaner, kwa
sababu ni dawa na sio nzuri kwa chakula.Rudia mpaka uhakikishe imeisha na
microwave safi.
Kama baadhi ya
madoa hayajatoka tumia kitambaa lowanisha na Olive Oil safisha tena.
Kuwa muangalifu na dawa au sabuni aina nyingine utumiazo
kusafishia microwave.Kwa mfano,usitumie dodoki lililolowekwa ndani ya microwave
inaweza kushika nyaya zilizolegea ikasababisha hatari. Kutumia dawa zisizo salama ni
hatari .Pendelea vitu vya asili kama vinegar,ndimu n.k
Acha microwave ikauke.Hakikisha harufu nzuri ya
microwave.Kama bado ina harufu ya window cleaner chukua kitambaa safi kisuuze
na maji safi futia tena kwa mara nyingine.