• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, November 29, 2017

Kusafisha microwave

4:12 AM // by Kalma // No comments

Kusafisha microwave

Mnato wa chakula kwenye microwave unaonekana vibaya,harufu sio nzuri,na hupunguza thamani ya microwave jikoni.Kwa bahati,microwave ni rahisi kusafisha ukijua.

Vinegar

        Glass inayofaa kwa microwave au bakuli yenye nusu maji changanya na 1 kijiko cha kula cha white vinegar.Tia ndani ya microwave.
Washa kwa dakika 5.Utahitaji dakika chache kwa microwave zenye nguvu zaidi,wakati ukisubiria hapo hapo kwa mara ya kwanza.Njia hii itayeyusha ukuta wa microwave na kugandua vilivyogandia.
Toa kama ni glass au bakuli,tumia kitambaa safi kwa kufutia au paper towel.Ondoa sahani ile ya kioo osha kama chombo kawaida,tumia dishwasher kama una muda.

Ndimu au Limao


   Kata ndimu au limao nusu.Tia maji nusu kijiko cha kula kwenye bakuli na vipande vya ndimu.Washa kwa dakika moja au ndimu imekua ya moto na uchafu umeganduka.Tumia kitambaa safi kufutia.Osha sahani kama kawaida.
Kwasababu ndimu imechemka husafisha vizuri kiasili kwa kibebeo (dustbin)cha taka za jikoni zikate vipande vidogo dogo zaidi na osha na maji mengi.  

Sabuni ya vyombo


Chukua bakuli tia maji ya moto ,tia sabuni ya vyombo kwa kiasi unachohitaji.Washa microwave kwa dakika moja mpaka uchafu uyeyuke.Tumia kitambaa au sponji safi kwa kufuta.Unaweza tumia baking soda ina harufu nzuri.

    Window Cleaner


  Changanya maji na window cleaner kwa maji ya uvuguvugu.Mchanganyiko huu utasafisha ndani na nje ya microwave.
    Futa ndani  kwa kuloweka sponji au kitambaa ndani ya mchanganyiko huo,toa sahani ya microwave safisha ndani na nje hadi uchafu uishe.Hakikisha microwave haijawashwa pindi usafishapo.

Loweka madoa kwa window cleaner kwa dakika 5 kabla ya kusugua.Suuza kitambaa au sponji kwa maji safi na ufute na window cleaner, kwa sababu ni dawa na sio nzuri kwa chakula.Rudia mpaka uhakikishe imeisha na microwave safi. 
      

       Kama baadhi ya madoa hayajatoka tumia kitambaa lowanisha na Olive Oil safisha tena.
Kuwa muangalifu na dawa au sabuni aina nyingine utumiazo kusafishia microwave.Kwa mfano,usitumie dodoki lililolowekwa ndani ya microwave inaweza kushika nyaya zilizolegea ikasababisha hatari. Kutumia dawa zisizo salama ni hatari .Pendelea vitu vya asili kama vinegar,ndimu n.k

Acha microwave ikauke.Hakikisha harufu nzuri ya microwave.Kama bado ina harufu ya window cleaner chukua kitambaa safi kisuuze na maji safi futia tena kwa mara nyingine.

Safisha nje ya microwave.Window cleaner ni salama kutumia kwenye milango ya microwave,vitasa,viwashio,na pembe zake.Futa vizuri mpaka vitakate. 

0 comments:

Post a Comment