• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, November 21, 2017

Jinsi ya kung’arisha tiles

2:36 AM // by Kalma // No comments

Jinsi ya kung’arisha tiles

Achana na kufagia na kudeki kila siku vipi unaweza kung’arisha tiles zilizofubaa,tiles zisizo ng’aa tena?Usikate tamaa,kuna njia ya kurudisha mng’ao kwa tiles zako tena.Njia hizi tumejaribu na zikafaa na kuleta mng’ao kwa tiles.
Vinegar na maji ya uvuguvugu
Tuanze na hii lakini inafanya kazi vizuri sana.Hii njia ni common imezoeleka sana hata pindi usafishapo kila mara.Vinegar hung’arisha vizuri na huondoa madoa mpaka tiles za ukutani sehemu ya kupikia.Kumbuka usitumie vinegar kwenye sakafu ya mbao ni asidi ambayo itaharibu hilo eneo.Suuza eneo hilo kwa maji ya baridi baada ya kusugua tumia vinegar.

Furniture Polish
Hii ni nyepesi lakini nzuri nayo kung’arishia tiles zako.Unachotakiwa kupulizia kwenye kitambaa cha kusafishia au kitambaa cha tea towel kwa mipulizo kumi(10) ya furniture polish.Weka kitambaa kwa sakafu yako na utumie mgongo wa brush kupolish kwenye tiles zako.Angalia vizuri uliposugua patakua panateleza kwa saa chache mpaka patakavyokuka.
Mswaki na dawa ya meno



Naamini watu wengi wanawaza jinsi ya tiles zao kung’ara.Njia moja tuliyoigundua kutumika iko mikononi mwako.Tumia mswaki chakavu na dawa ya meno,tumia kusugua tilea na kuondoa uchafu.Ukimaliza utasafisha uchafu uliomwagika kwenye mikono.Ni usumbufu?Tunahisi hivyo.
Dekio la kuaminika

Hii iko pale pale lakini ni kifaa  muhimu.Wataalamu baadhi wanasema maji ni kiungo muhimu kwa kusafishia tiles.Kwa hiyo,ni jinsi gani unatumia dekio lako kuleta mng’ao kwa tiles zako.Kama hilo dekio linatumika kila mahala basi hakikisha unalisafisha kwa maji ya moto kabla ya kusafishia tiles zako.Safisha vizuri ndoo ya kudekia tiles zako,weka nusu maji moto utumie kusafishia likiwa safi .
  Baking Soda
Je cooker lako au jiko la umeme linachafua tiles za ukutani jikoni kwako?Muda mwingi hautaona, lakini bakteria wanajenga humo kama hautakua makini na hilo.Njia ya kusafisha kuu kwa tiles zilong’ang’ania mafuta ni mchanganyiko wa baking soda na maji ya vuguvugu.Chukua bakuli kubwa lenye maji ya uvuguvugu ,na vijiko vya kula kadhaa vya baking soda tumia kwa kusugua tiles hizo.
Maji ya ndimu

Njia hii imezoeleka sana kwa matumizi mbalimbali majumbani inaweza kutumika kama aina ya kusafishia na kinywaji kwa upande mwingine.Kamua ndimu kwenye kitambaa,sugua kwenye tiles chafu na suuza kwa maji ya uvuguvugu.Baada ya kutumia chochote chenye asidi  futa eneo hilo na kitambaa safi laini.
Tiles zina sifa ya kusafishika haraka na zina asili ya kujilinda na layer za uchafu kwahiyo usiwe na wasiwasi wa kubadilisha kila mwaka.

Tips hizo juu ni rahisi na zitakusaidia kuleta mng’ao!

0 comments:

Post a Comment