Water cooler
Safisha water cooler kwa maji safi na crisp
Ili kuyafurahia ladha ya maji kwa chupa zetu,kusafisha water cooler na kuitunza ni jukumu letu kuu.Mara zote kuhakikisha maji ni masafi
na kifaa hicho ni kisafi ili kujilinda na mazalio ya bacteria mbalimbali.
Jinsi ya kusafisha
Ondoa chupa
iliyoisha maji kwenye cooler
Tia 1 kikombe
vinegar na 3 vikombe vya maji moto.Tumia kitambaa safi ,safisha ndani ya sehemu
inayokaa chupa ya maji.
Utamwaga maji hayo
kupitia mabomba kwenye cooler.Safisha kwa sabuni ya jikoni ya kuua vijidudu na
bacteria.kama bomba zinatoka utaosha kama vyombo kawaida.
Suuza,tumia maji
safi na salama mara mbili kwa kufungua bomba za cooler .
Rudishia vifaa ulivyotoa na weka chupa ya maji safi,na
chomeka kwenye umeme
Kama umefatisha mpangilio huo cooler yako itakua safi,na
umechukua jukumu la kuitunza vyema kiafya na kunywa maji salama.
Wasiliana na wakala wa cooler kwa usafi na marekebisho
zaidi.
Inashauriwa kila baada ya miezi sita uifanyie usafi wa kina
wa ndani na nje wa cooler yako.
0 comments:
Post a Comment