• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Sunday, January 5, 2014

JUISI YENYE AFYA: KAROTI & TANGAWIZI

10:09 AM // by Kalma // No comments

Ningependa kushare na nyinyi wadau wangu, Juisi ya karoti na tangawizi. Ni rahisi kuitengeneza ila ni tamu vibaya mno.Mahitaji yalokuwemo kwenye hiyo juisi ni ufunguo wa virutubisho kwa lishe ya  afya nzuri,na juisi nzuri,pata karoti fresh na chungwa pia.
     Italeta mabadiliko makubwa!
 Juisi ya karoti itakupa dose kubwa ya  beta-carotene itayosaidia kuboost immune system na vile vile kuzidisha nguvu ya afya ya macho na ngozi.
Tangawizi ni kiungo kizuri nacho kinojulikana sana kwa kuongeza nguvu, kulainisha katika mfumo wa usagaji chakula, na kupunguza mafuta yalojikusanya,huongeza kitu kizuri katika juisi yako hiyo. 
Angalia machungwa fresh sokoni .Tia katika juisi yako, ila madanzi ni mazuri zaidi kama utapata.
Huifanya juisi kuwa ya asili tamu na huongeza vitamin C.
Karoti na Tangawizi .
Fungu la karoti
 Machungwa (dalanzi.)
 Tangawizi (yaweza kuwa size ya kiganja chako.)
Anza kwa kusuuza karoti — haina haja ya kumenya maganda. Ondoa kikonyo cha juu tu. Ila nazo ni nzuri katika juisi yako.
Menya machungwa yako.
Kata kata tangawizi zako baada ya ushaziosha tayari.
Tumia machungwa kama ndo maji ya kusagia matunda yako hayo.
     Furahia juisi yako na mpe na mwenzako, kilicho bora kwa afya zenu. Kisha muulize anaijua Manal shops?
Usiache kufanya hivyo nasubiria majibu yako…..!

0 comments:

Post a Comment