KUG'ARISHA MENO
Kuna products nyingi zinapatikana
siku hizi za kung’arisha meno yako,lakini huwa ni gharama yaani bei
kubwa.Nimejaribu njia kidogo hapa,lakini matokeo hayaonyeshi ni ya muda mrefu
au ya kudumu(sema labda haifanya kazi kwa kahawa nazokunywa).
Mwishowe nikaangalia
njia ambazo unaweza tumia nyumbani mara zote,nikagundua zipo chache ambazo
zinaweza kung’arisha meno yako na kuwa meupe.
Jaribu hizi nyumbani kufanya meno
yako yawe meupe.
Kula strawberies!
Nakumbuka nilisikia nilipokuwa
sehemu na watu tu naikumbuka hii-na ukweli kwamba,zinafanya kazi
kweli.Strawberies yana astringent ambayo yanaongeza kutoa uchafu au kutu ilo mwanzoni
,na Vitamin C,ambayo hufanya meno kuwa meupe kwa kuondoa plaque.Sijafanya
uchunguzi wa kina sana kuhusiana na matunda haya ila najua yanapatikana
supermarkets na ni bei iko juu.Ukijaaliwa kuyapata yatumie kwa kuyala,na
sugulia katika meno.
Matunda na mboga za crunchy.
Matunda na mboga za crunchy.
Crisp,mboga za crunchy kama karoti,na celery au matunda kama
apples nayo pia ni yana asili ya tengeneza meno kuwa meupe .Yanakua kama mswaki
pindi unapoyatafuna kwa kuondoa vyakula,na bacteria walobakia kwenye meno na
pia husugua kuondoa uchafu ulo juu ya meno.Kuyatafuna matunda hayo huleta
mate,ambayo ni usafi wa asili wa mdomo.Karoti ina Vitamin A,ambayo hutakiwa kwa
afya ya meno pia,na apple ina malic acid,husaidia kuyeyusha uchafu-malic acid
ni dawa ambayo hutokea kutumika kwa products nyingi za kufanya meno yawe meupe.
Maganda ya machungwa
Sehemu nyeupe ya ganda la chungwa
kwa kizungu hitwa albedo.Hii sehemu ya chungwa ina vitamin C na limonene,kwa
vingi vilokuwemo. Limonene ni ya asili kwa ajili ya kusafishia ambayo hutumika
kwa products nyingi za usafi.Maganda hayana citric acid pia,ambayo huweza
sababisha madhara katika meno yako.Siku nyingine ukila chungwa,sugulia ganda
katika meno yako na kisha ndo ulitupe!
Baking Soda & Hydrogen Peroxide
Njia hii itumike na tahadhari
,kwasababu kama itatumika sana huweza leta madhara kwa meno yako.Changanya
baking soda na hydrogen peroxide kupata “rojo”kupigia katika mswaki wako.Ina
ladha sio nzuri lakini iko vizuri kwa kung’arisha meno-najua ni geni kwako
kutumia hydrogen peroxide katika mdomo wako,lakini ni aina ya bleach ambayo
hutumika kwa dawa nyingi za kufanya meno
yawe meupe..Kama unafikiria kutumia za kununua kwa bei ghali,achana na huko
hamia njia za asili sasa!
Mdau wangu unatumia njia
gani?tujuzane!
0 comments:
Post a Comment