KUONDOA M-BA
M-ba(dandruff)huenda ikawa ni
madhara ya ngozi kavu,au hali ya ngozi inayoitwa seborrheic dermatitis.Huweza
sababishwa na eczema, psoriasis, au, kawaida zaidi,kasi ya kukua kwa fungasi
anaitwa malassezia. Dawa za kutibu inaweza kuwa shampoo pamoja na zinc
pyrithione, ambayo hukomesha fangasi na bacteria, ketoconazole, nayo
inapambana na fangasi; coal tar na selenium sulfide,ambayo hukuza na kuua seli
zilokufa katika ngozi ya kichwa; na salicylic acid, hii hulainisha flakes
ambayo huondoka kwa kuoshwa.
Tumia hizi njia za asili.
Aspirin
Aspirin inafanya kazi ya (salicylic
acid) kama shampoo nyingi za dawa.Chukua vidonge viwili vya asprin visage viwe unga
kabisa, weka kwenye shampoo unayotumia osha nywele siku zote.Pakaa kwenye
nywele kwa dakika 1-2,suuza nywele ,osha na shampoo iso na asprin.
Imegundulika kuwa shampoo zenye
asilimia 5% ya mafuta ya tea tree hupunguza makali ya m-ba.Weka matone machache
kwenye shampoo yako pindi unapoosha nywele.
Baking soda
Jiko lako ni ufunguo wa kutengeneza
mambo mazuri,kuanzia mapishi, afya na urembo pia. Lowanisha nywele zako kisha sugua
baking soda ya ujazo wa kiganja chako.Usitumie shampoo kisha zioshe.Baking soda
huondoa au kupunguza fangasi ambao sababu ya m-ba.Nywele zako zinaweza zikawa
kavuu mwanzoni,lakini baada ya wiki kadhaa ngozi ya kichwa itaanza kutoa mafuta
ya asili,na zikafanya nywele zako kuwa nzuri na kuepusha ukoko.
Dr. Mehmet Oz swears juu ya apple cider vinegar kama ni tiba ya m-ba,kama
ilivyo acidity ya vinegar ya apple hubadilisha pH ya ngozi yako, kuifanya kuwa
ngumu kwa bacteria kuzaliana.Changanya robo kikombe cha vinegar ya apple na robo
kikombe cha maji katika chupa ya pulizo(spray bottle) na kisha pulizia kwenye
ngozi ya kichwa chako.Funika kichwa na taulo na kaa kwa dakika 15 mpaka saa
nzima,osha nywele kama kawaida.Fanya hivi mara mbili kwa wiki.
Mouthwash
Kutibu m-ba waliokomaa kichwani,osha
nywele kwa shampoo yako unayotumia,kisha suuza na mouthwash.Kisha tumia
conditioner.Mouthwash ni anti-fungal
husaidia kulinda na m-ba ambao wanasababisha hata bacteria kukua.
Crunchybetty.com amesema coconut oil is a "tried and true" na
ni tiba ya m-ba,na hunukia vizuri pia.Kabla ya kuoga,sugua 3-5 vijiko vya
chai vya mafuta ya nazi katika ngozi yako na uache kwa saa nzima.Osha na
shampoo kawaida.Unaweza kutumia shampoo zenye mafuta ya nazi pia.
Ndimu
M-ba hauwezi kudumu kama friji lako.Vijiko
2 vya chai vya maji ya ndimu sugua kwenye ngozi ya kichwani na osha na
maji.Kisha koroga kijiko 1 cha chai ya maji ya ndimu ndani ya kikombe cha maji
kisha suuza nywele kwa mchanganyiko huo.Fanya hivyo kila siku mpaka m-ba
wapotee kabisa.Asidi iliyoko kwenye ndimu husaidia kubalansi pH ya ngozi
yako,ambayo husaidia kuondoa m-ba pia.
Chumvi
Chumvi nayo ni nzuri na huondoa m-ba
kabla ya shampoo.Chukua saltshaker kisha nyunyizia chumvi kwenye ngozi ya kichwani.kisha sugua nywele na ngozi.Utahisi ukavu na nywele zimenywea hapo itakua tayari
kuoshwa na shampoo.
Aloe
vera
Usisugue aloe vera katika ngozi ya
nywele kabla ya shampoo.Madhara ya kupoa kwa aloe vera husababisha kuwashwa na
maumivu.
Kitunguu thoum
Kitunguu thoum
Kitunguu thoum ni anti-fungal
huondoa vizuri na kwa haraka m-ba wanaosababisha bacteria. Saga kitunguu thoum
kisha sugua kwenye ngozi ya kichwa.Kuepukana na harufu,unashauriwa uchanganye
kitunguu thoum na asali na sugua kwenye ngozi kabla ya kuosha kama kawaida.
Olive oil
Kwa usiku mzima lowanisha nywele na
mafuta ya olive.Sugua kwenye ngozi ya nywele
matone kumi ya mafuta kisha vaa kofia usiku kucha.Osha na shampoo yako
asubuhi.Kwa tiba ya haraka,tumia shampoo ambayo ina olive oil.
0 comments:
Post a Comment