• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Sunday, November 21, 2021

KUTUMIA NDIMU KWA:

10:34 PM // by Kalma // No comments

  

NDIMU,
Faida za ndimu zimekua maarufu kila kona.Hutumika kama tiba ya nyumbani kwa meno yanayouma,au njia za asili za kusafishia nyumba,ndimu hufanya yote hayo.

Kuanzia maisha yote,mpaka kwa hii post mpya,hata kwenye maandishi kibao ipo.
Nimesoma matunda mengi ya ajabu haikukosekana ndimu,na funs nyingi ndani yake na mawazo kibao kwa matumizi ya tunda ndimu.

Hizi ni zile nilozichagua mimi kukufikishia na wewe mdau wangu.
         Kuondoa sumu
Jaribu kunywa maji ya ndimu kiwe kinywaji  cha kwanza asubuhi au 20-30 dakika kabla ya kula chochote kustua gastric juisi.
unachotakiwa:
1/2 inch ya kipande cha tangawizi chembamba
Juisi  ½ ya kipande cha ndimu
2 vikombe vya maji yalochemshwa
Asali kuleta ladha
maelekezo:
Mimina maji yalochemshwa kwenye tangawizi,yaache kwa dakika tano,na kisha weka ile juisi ya ndimu na asali.
Kusafisha 
Kutoa harufu kwenye microwave:Jaza maji kwenye glass na nusu kipande cha ndimu,na kisha weka ndani ya microwave kwa dakika tano.

Kupolish /kung’arisha mbao: Tumia chupa ile ya kupulizia,weka vijiko vya chai 2 vya olive oil na juisi ya kipande cha  ndimu kuchanganya katika ½ kikombe cha maji ya uvuguvugu  ndani ya chupa.

Pulizia katika kitambaa cha kusafishia cha aina ya  pamba na tumia kufuta katika hiyo furniture.

 Metali na ubao wa kukatia(cutting wood):  nyunyizia chumvi katika nusu kipande cha ndimu na sugua Suuza na safisha.
Afya ya mdomo
Maji ya ndimu yanaweza tumika kutunzia meno.Weka juisi ya ndimu katika jino linalouma kuondoa maumivu,au sugua katika fizi kustopisha damu isitoke.Unaweza kusafisha  na kuondoa harufu ya mdomoni au pumzi,kama kusukutua maji ya ndimu kwa sekunde 30.
 Radiant Skin
Kutibu tokea ndani na nje: Ndimu ina vitamin C ,ambayo kutumia tunda  ni vizuri katika kuondoa sumu na kutuma antioxidants katika ngozi. 

Unaweza kutibu kuanzia nje kwenda ndani: chukua zest ya ndimu na sukari na loweka mchanganyiko huo na olive oil kwa dakika 30 kutengeneza scrub ya  mwili nyumbani kwako mwenyewe.
                   Anza kusugua kwenye kiwiko cha mikono,na vifundo vya miguuni,na magoti kuondoa ukavu wa hizo sehemu.


Share and Enjoy!



Friday, November 19, 2021

5 MAKOSA YA FANICHA ZA NGOZI(LEATHER)

1:35 AM // by Kalma // No comments

 5 MAKOSA YA FANICHA ZA NGOZI(LEATHER)Ni nzuri, ya kudumu,yenye kupendeza kuketi,lakini inawezekana kwamba unaharibu fanicha yako ya ngozi bila hata kujitambua? Ingawa ngozi ni fanicha  ya kudumu,na ni matokeo ya asili. Epuka makosa ya kawaida ya fanicha ya ngozi linapokuja suala la matengenezo na kusafisha pia.Kuweka au kuhifadhi Karibu na Joto na mwanga wa JuaUwekaji wa fanicha sebuleni mara nyingi hutegemea urahisi na mvuto wa kuona. Lakini, ikiwa utaweka fanicha ya ngozi karibu sana na jua linapochoma au aina yoyote ya kitu au kifaa chenye kuleta moto au hali ya hewa ya joto, unaweza kuhatarisha fanicha yako ya ngozi.Matoleo ya joto, radiator, na hita zinaweza kuleta uharibu wa fanicha za ngozi na kufubaza hii hutokea kwa  muda mrefu. Kwa kuongezea, sehemu ya jua au mwanga wake wa jua unaweza kufifisha na kuharibu fanicha  zako za ngozi, pia na kusababisha viraka vyenye rangi ya mpuko kidogo pia. Hali mbaya zaidi ni pamoja na sehemu zilichanika huwa kavu,zitasagika na kuchanika kabisa.

Kuweka Vifaa vilivyochapishwa kwenye ngoziMagazeti, majarida, na hata vitabu vingine vinaweza kuchuja kwenye fanicha ya ngozi wakati kimeachwa juu ya fanicha hiyo. Ingawa fanicha ni mahali pazuri pa kuacha vifaa vya kusoma, utastukia una nakala ya  ziada ya chapa kwa fanicha yako. Hii ni kweli haswa kwa kurasa za majarida na rangi zao zenye kupendeza au kurasa za kuchorea zilizo na michoro ya rangi juu ya fanicha izo. Ni bora kuzuia kuacha vitu kwenye ngozi kwa kipindi chochote cha muda wote.

Kutogeuza cushions mara kwa mara

Ngozi inapendekezwa iwe na umbo lake vyema mara zote, kwa hivyo wamiliki wanaweza kuwa wazembe zaidi katika kupuuza na kugeuza cushions za fanicha. Mikunjo inayoendelea kwenye kochi za ngozi haziwezekani kurekebisha kabisa. Dau bora kwa fanicha za ngozi ni kugeuza na kutoa cushions kila wiki.

kusahau kufuta vumbiFanicha za ngozi inahitaji usafi wa vumbi kila wiki.Hijalishi utatumia aina ya kitambaa cha microfiber au utatumia brush ya vacuum cleaner,kubwa na la msingi ni umakini wa kufuta vumbi kila wiki.Vumbi ni adui wa mengi,ikiwemo ngozi .Bahati kubwa adui huyu anaepukika  kirahisi kwa usafi wa mara kwa mara na wa wiki pia.

Matumizi ya vifaa visivyosahihi vya kusafishia.Wamiliki wa fanicha na vifaa vya ngozi zuia matumiziz ya sabuni na datergents,sprays, mafuta,na polishi zenye madhara au zinazoweza kuharibu ngozi kwa fanicha yako.Fuatilia kwa kina maelezo ya viwandani vya aina za dawa unazotumia na pindi kuna mkwamo tumia wataalamu.Mara nyingi kitambaa kikavu,au matumizi sahihi ya kitambaa kwa ajili ya usafi wa ngozi na maji vuguvugu ndio vitakiwavyo.Baadhi ya wataalamu wa kusafisha aina ya vifaa vya ngozi wamekubali  kipimo cha sawa kwa sawa maji na vinegar ni kizuri,hata hivyo ukijipanga kutumia kitu kingine cha kusafishia hakikisha una kua makini na madhara na faida kwa hiyo fanicha vizuri.Anagalia vizuri tag za hiyo fanicha,angalia material yaliyotumika,au wasiliana vizuri na wataalamu kina sakamia,zingatia ya kuwa usitumie product ambayo haijapendekezwa kuepusha uharibifu wowote kwa fanicha zako.

  SHARE AND ENJOY !

Thursday, November 11, 2021

KUONDOA M-BA.

1:24 AM // by Kalma // No comments

KUONDOA M-BA
M-ba(dandruff)huenda ikawa ni madhara ya ngozi kavu,au hali ya ngozi inayoitwa seborrheic dermatitis.Huweza sababishwa na eczema, psoriasis, au, kawaida zaidi,kasi ya kukua kwa fungasi anaitwa malassezia. Dawa za kutibu inaweza kuwa shampoo pamoja na zinc pyrithione, ambayo hukomesha fangasi na bacteria, ketoconazole, nayo inapambana na fangasi; coal tar na selenium sulfide,ambayo hukuza na kuua seli zilokufa katika ngozi ya kichwa; na salicylic acid, hii hulainisha flakes ambayo huondoka kwa kuoshwa.
Tumia hizi njia za asili.
Aspirin
Aspirin inafanya kazi ya (salicylic acid) kama shampoo nyingi za dawa.Chukua vidonge viwili vya asprin visage viwe unga kabisa, weka kwenye shampoo unayotumia osha nywele siku zote.Pakaa kwenye nywele kwa dakika 1-2,suuza nywele ,osha na shampoo iso na asprin.


Tea tree oil
Imegundulika kuwa shampoo zenye asilimia 5% ya mafuta ya tea tree hupunguza makali ya m-ba.Weka matone machache kwenye shampoo yako pindi unapoosha nywele.


Baking soda
Jiko lako ni ufunguo wa kutengeneza mambo mazuri,kuanzia mapishi, afya na urembo pia. Lowanisha nywele zako kisha sugua baking soda ya ujazo wa kiganja chako.Usitumie shampoo kisha zioshe.Baking soda huondoa au kupunguza fangasi ambao sababu ya m-ba.Nywele zako zinaweza zikawa kavuu mwanzoni,lakini baada ya wiki kadhaa ngozi ya kichwa itaanza kutoa mafuta ya asili,na zikafanya nywele zako kuwa nzuri na kuepusha ukoko.


Apple cider vinegar
Dr. Mehmet Oz swears juu ya  apple cider vinegar kama ni tiba ya m-ba,kama ilivyo acidity ya vinegar  ya apple hubadilisha pH ya ngozi yako, kuifanya kuwa ngumu kwa bacteria kuzaliana.Changanya robo kikombe cha vinegar ya apple na robo kikombe cha maji katika chupa ya pulizo(spray bottle) na kisha pulizia kwenye ngozi ya kichwa chako.Funika kichwa na taulo na kaa kwa dakika 15 mpaka saa nzima,osha nywele kama kawaida.Fanya hivi mara mbili kwa wiki.

Mouthwash
Kutibu m-ba waliokomaa kichwani,osha nywele kwa shampoo yako unayotumia,kisha suuza na mouthwash.Kisha tumia conditioner.Mouthwash  ni anti-fungal husaidia kulinda na m-ba ambao wanasababisha hata bacteria kukua.


Mafuta ya nazi
Crunchybetty.com amesema  coconut oil is a "tried and true" na ni tiba ya m-ba,na hunukia vizuri pia.Kabla ya kuoga,sugua 3-5 vijiko vya chai vya mafuta ya nazi katika ngozi yako na uache kwa saa nzima.Osha na shampoo kawaida.Unaweza kutumia shampoo zenye mafuta ya nazi pia.


Ndimu
M-ba hauwezi kudumu kama friji lako.Vijiko 2 vya chai vya maji ya ndimu sugua kwenye ngozi ya kichwani na osha na maji.Kisha koroga kijiko 1 cha chai ya maji ya ndimu ndani ya kikombe cha maji kisha suuza nywele kwa mchanganyiko huo.Fanya hivyo kila siku mpaka m-ba wapotee kabisa.Asidi iliyoko kwenye ndimu husaidia kubalansi pH ya ngozi yako,ambayo husaidia kuondoa m-ba pia. 


Chumvi
Chumvi nayo ni nzuri na huondoa m-ba kabla ya shampoo.Chukua saltshaker kisha nyunyizia chumvi kwenye ngozi ya kichwani.kisha sugua nywele na ngozi.Utahisi ukavu na nywele zimenywea hapo itakua tayari kuoshwa na shampoo.


Aloe vera
Usisugue aloe vera katika ngozi ya nywele kabla ya shampoo.Madhara ya kupoa kwa aloe vera husababisha kuwashwa na maumivu.




Kitunguu thoum
Kitunguu thoum ni anti-fungal huondoa vizuri na kwa haraka m-ba wanaosababisha bacteria. Saga kitunguu thoum kisha sugua kwenye ngozi ya kichwa.Kuepukana na harufu,unashauriwa uchanganye kitunguu thoum na asali na sugua kwenye ngozi kabla ya kuosha kama kawaida.

Olive oil
Kwa usiku mzima lowanisha nywele na mafuta ya olive.Sugua kwenye  ngozi ya nywele matone kumi ya mafuta kisha vaa kofia usiku kucha.Osha na shampoo yako asubuhi.Kwa tiba ya haraka,tumia shampoo ambayo ina olive oil. 




Tuesday, October 12, 2021

Kupunguza uzito – Haraka na Nzuri

6:32 AM // by Kalma // No comments

Kupunguza uzito  – Haraka na Nzuri
Unasumbuliwa na uzito? Umechoka kuhangaika?Njia hizi za asili za kupunguza huo uzito kwa haraka bila ya kuhangaika.Kuwa na umbo lenye Afya .”
Uko tayari kupungua uzito bila ya kuhangaika?unaweza ukaifanya hiyo kwa mabadiliko ya kiafya kwa mlo na jinsi ya kuishi kila siku katika maisha yako.Unahitajia,kuwa muangalifu wa kuhesabu calories ambayo ni rahisi na itapelekea kujua kiasi gani unakula pindi usipohesabu ,na baada ya muda utajikuta umejijengea mfumo ambao unakua ni tabia yako ya maisha yako huwa tena ni mazoea….!!!Japokuwa kupunguza kwako uzito utakuwa  kwa kiasi kikubwa mno kwa kujumlisha na mazoezi,na unaweza usifanye pia.Tuangalie njia za asili hizi:
Njia za kupungua uzito kwa haraka
MAJIGlass moja ya maji au green tea kabla ya kula au mara mbili kwa siku.Maji yatachukua nafasi kidogo kwenye tumbo lako,husaidia kuhisi umeshiba hata ukila kidogo.kama itashindikana kunywa glass nzima, basi kunywa kidogo kila unapopata tonge la msosi.Kinywaji cha sukari pia ni kizuri badala ya maji.Weka kipande cha ndimu katika kinywaji chako utapata ladha nzuri.TABIA
1.Hesabu calories unayopata ili kupunguza mwili itakua rahisi kwa kupunguza calories ambazo zinapatikana mwilini mwako .Zitambue calories tokea katika milo unayokula mara kwa mara ,halafu utaijumuisha hizo calories mwisho wa siku yako.Adhimia
Dhumuni au nia ni kupungua pound moja kwa  wiki.Hii ni njia salama ya kupunguza uzito,na haihitaji kuilazimishia kupungua kwa haraka.Pound moja ni sawa na calories 3500,kwa maana hiyo unahitaji  kupunguza calorie 500 kila siku kwa wiki.kula chakula ambacho kinachukua muda kumeng’enywa au kusagwa kama vile matunda,mboga mboga,nuts,legumes na jamii ya nafaka.Kula vyakula vya asili vya kuchelewa kuyeyushwa  husaidia kujihisi umeshiba kwa kipindi kirefu,na vile vile itafanya  metabolism kuwa busy  pia.Achana na bites  ndogo.Pindi unapokula epuka kuwa na mlo mwingi mdomoni.Badala yake, tafuna chakula chako kwa mpangilio.Hii itakulazimisha kula taratibu,na utakua umepangilia mlo wako vizuri na itakua rahisi kwako kujua kirahisi pindi utaposhiba
RATIBA1.Kunywa chai au kifungua kinywa ni lazma yaani haina m-badala.Haiepukiki  na usijichanganye,kwa maana hautapunguza uzito kama utaepuka chai ya asubuhi.Hata kisomi inaonyesha kunywa chai ya asubuhi  hutengeneza metabolism  kwa ajili ya kufanya kazi kutwa nzima.2.Kula kwa mpangilio maalum.Ikiwa utaweza,jaribu kula milo yako kwa mida maalum hiyo hiyo kila siku.Kula kwa kufuata  ratiba husaidia mwili wako kujiandaa na kwa utulivu ambao utaruhusu kuyeyusha kiasi cha calories3.Kama tabia yako ya kula haitabiriki au huwa unaruka ruka milo ,mwili wako hua unawekeza calories kwa ajili ya dharura4.Usipendelee kula uangaliapo tv au mbele ya computer.Kwa kufanya hivyo utajikuta akili yako haipo zaidi kwenye kula.
 5.Epuka kula kwa mfadhaiko au stress.Stress au tamaa ya kula huweza kukuongezea uzito kwasababu utakuwa umekula kupitiliza.Kula pindi hauna njaa kali huongeza tani zisizo lazima za calories kwa diet yako ambayo huweza kuondolewa kirahisi na stress
6.Acha kula usiku mkubwa au mnene.Sababu hiyo, mwili wako hautaunguza calories nyingi pindi ulalapo,ni sawa na kula tu na kulala.
          Enjoy and Share !