Kwa Maisha ya kisasa kila mtu yuko busy na kazi zake,lakini wakati huo huo usafi ni muhimu na lazima kwa afya ya kujikinga na maambukizi katika mazingira.Nyumba ni zetu,cha muhimu kinachohitajika,ni usafi wa nyumba, ni jambo letu muhimu na ni jukumu kuu,kama halikufanyika vyema litaleta madhara ya maradhi.Usafi wa nyumba unaambatana na kufagia,kufuta vumbi furnitures na maeneo yote,kudeki sakafu,kung,arisha maeneo na kusugua au kufuta tiles.Usafi wa nyumba sio mgumu,ni rahisi tu.Kwa kuufanya uwe mwepesi tumia vifaa mbalimbali vilivyo masokoni.Vifaa vya usafi na zana vimeundwa maalum kwa viwango vya usafi wa nyumbani,na rahisi kuvitumia.Lengo kuu la vifaa vya usafi ni kusaidia kusafisha nyumba kwa rahisi kwa nguvu kidogo.Hizi ni list ya vifaa muhimu kwa usafi wa nyumba.Lakini,kwanza kuwe na sehemu ya kuhifadhia,ambayo itahifadhi vifaa hivyo.
Fagio:Kila nyumba lazima iwe na fagio kwa ajili ya kufagia sehemu ngumu kama vile tile,mbao,na sakafu ya zege,n.k.Ufagio umeundwa maalum kwa ajili ya kusafisha maeneo ya ndani na nje.Fagio linatakiwa kuwa sio lenye kuumiza mgongo,liwe lenye kusafisha vumbi,liwe lina sifa za kimakenikia kwa mfano lisiwe lenye madhara ya uchafu au vumbi wakati wa kusafisha,lenye gharama nafuu. Chelewa zinatakiwa kuwa flexible,zinafikika hata kwenye mikato midgo dogo.
Fagio liwe na kichwa kikubwa liweze kushika uchafu mwingi kwa Pamoja kwa muda mfupi.Shikio au mkono au fimbo la ufagio inaweza kuwa la mbao,plastic,au steel au aina yoyote.Masokoni,kuna kila aina ya fagio kama vile laini,ngumu,zenye mishikio mirefu,na yote ni kwa matumizi maalumu.
Microfiber Cloth:Microfiber cloth nyingi hutengenezwa kwa polyster au nylon,haifanani na cotton,microfiber cloth ni chaguo zuri kwa kutoa mavumbi kwasababu inakamata mavumbi mengi bila ya kuyapeperusha hewani.Microfiber cloth ni nzuri kwa kusafisha eneo lolote bila kuacha michubuo au kuacha michoro nyuma yake.
Inatumika kusafisha vioo na glass,kavu au kibichi kwa kudekia sakafu,counter tops za jikoni na kwenye jiko,sinki za bafuni,tubs na bomba za kuogea n.k.
Tambara la deki:Tambara za deki ni kubwa,nyembamba na hutengenezwa kwa coarser cotton kwa ajili ya usafi wa majumbani.Hutumika kufuta pedestals,tile,marble,na kuondoa au kufuta uchafu uliomwagika kwenye sakafu.
Fagio linalotumika kufagia uchafu na kizoleo hutumika kuzoa vumbi na uchafu kwa rahisi.
Pia ni msaada kwa kusafisha haraka kwa uchafu
uliomwagika.Kizoleo hutengenezwa kwa plastic au stainless steel kwa maumbo
tofauti tofauti na vipimo,na vina mishikio mirefu nayo.
Chamois Leather:
Chamois leather ni ngozi ya mbuzi.Inatumika kuondoa vumbi,ukungu,kusafisha fingerprints na vitu vichafu mbalimbali majumbani.Chamois leather cloth ni nzuri kwa kusafisha madirisha na vioo kwa maajabu ya mng’ao kwa madirisha ya vioo.
Kitambaa na sponji sio kila mara hutumika,tumia brush ngumu kwa kusugua na mkono kwa madoa sugu.Brush la kusugua ni nzuri kwa kusafisha sakafu na ukuta wa chooni na bafuni na unatumika kusafisha sink na grout kwa sakafu za tiles.
Zipo aina tofauti tofauti za brush kama vile za mkono kwa ajili
ya sakafu,ziko laini na za aina ya chupa n.k.
Ndoo:
Ndoo haitumiki kwa ajili ya kubeba maji pekee,lakini inaweza tumika kwa kusafisha nyumba pia kwa kudeki na matumizi mengine nyumbani.
Zipo kwa wingi za plastic au steel metal za aina tofauti kwa maumbo na size.
Mop:Miaka mingi iliyopita hadi sasa kwa baadhi tunatumia mikono kudeki sakafu.Lakini siku hizi mop zinatumika kwa kusafisha kirahisi.Mop ni kipande cha nguo,chenye uwezo wa kufyonza ambacho huunganisha kutumia kitobo kuweka gongo au mkono,ina faida nyingi za mekanikia.Ni kama ufagio tu,kuna aina tofauti za mop masokoni ikiwemo mop za kukaushia,za Kamba Kamba,impregnated dry mop,aina ya sponji,Kentucky mop,zipo za spring,zipo za waya waya,zote ni kwa kusafisha nyumbani.Zote hutumika kwa kusafisha maeneo ya sakafu ngumu.
Sponge:Sponji hutumika kusafisha jikoni na bafuni.Hutumika kuosha ukuta,vioo,glass,mbao,na upholstery.Kuna aina nyingi na tofauti kwa ukubwa wa maumbo zinapatikana sokoni kwa mtumizi tofauti ya usafi.
Squeegee:Unapomaliza kuoga safisha ukuta haraka,kabati za vioo,na tumia squeegee kufuta mabaki ya maji.Husaidia kupaacha safi na haijengi mabaki ya mapovu ya sabuni na huondoa maji pia.Hutumika kusafisha madirisha ya vioo kuondoa ukungu na uchafu,alama na mabaki ya michoro ya maji na mvuke wa maji katika vioo.
Duster:Dusters mara nyingi hutengenezwa kwa cotton laini,flannel au manyoya flani hivi zinazoshikiliwa na kifimbo.Hutumika kusafisha vumbi na kufuta maeneo tofauti.Aina tofauti za duster zinapatikana kama vile Extendible Lambswool Duster, Microfiber Duster, Ceiling Fan Duster, DustTamer Bendable Extendable Duster, Feather Duster, Static Duster, hutumika kwa kusafisha nyumbani.
Rubber Gloves:
Rubber gloves hutumika kwa kulinda mikono yako wakati wa kusafisha,haswa unapotumia dawa zenye asidi au kama una shida ya madhara ya ngozi.Vacuum Cleaner:Vacuum cleaner ni kifaa cha gharama nyumbani,lakini kinazoeleka kwa sasa.Vacuum cleaner hutumika kwa maeneo laini na magumu kama vile carpets,sakafu,ukuta na upholstery.Hurahisisha usafi na inachunga muda.
Note:
Mara zote tunza vifaa vya usafi viwe katika hali nzuri wakati mwingine utavihitaji kuvirudishia katika hali ya umbo lake zuri.Mara zote safisha vifaa umalizapo kutumia kabla ya kuhifadhi,na hifadhi vizuri sehemu kavu.Vifaa vya usafi hupunguza ugumu wa kusafisha na pia husaidia kusafisha maeneo ya kona na mikunjo ambayo kupafikia ni pagumu.Vifaa vya usafi ni rahisi kutumia na huchunga muda pia.
0 comments:
Post a Comment