Kutokana na kuwa na utumbo mdogo, watoto
hawali sana.Ndio maana ni muhimu kuwa na uhakika wa chakula wanachokula kina
lishe nyingi za kutosha na zote.Jifunze au jua jinsi ya kuweka muda wa kula kwa
watoto ili wapate hizo lishe bora kwao.
Muda wa mzuri wa kula
Kiujumla,chakula
cha nguvu ni kwa kuanzia watoto wa miezi sita (6)na kuendelea,pindi
kinapoandaliwa zingatia akili ya ulaji
wa mtoto wako.Lakini vizuri pia uzungumze na mkunga au daktari wa watoto kabla
ya kumpa mayai,samaki,citrus,na maziwa ya mtindi kama mtoto wako mdogo chini ya
mwaka kwasababu vyakula hivyo huweza kusababisha allergy.Vyakula vingine kama
nyama,matunda,na mboga mboga huweza kuanza kumlisha mtoto wa miezi 6 .Ila
kumbuka vyakula hivyo vya aina yoyote kisitambulishwe kwa mtoto wa miezi
mine(4).
Japokuwa
watoto hukua kwa utofauti,ni vizuri kutafuta ushauri wa daktari au watu wazima
dawa wale, kwa kujihakikishia pindi unapotaka kumuanzishia chakula mtoto na pia
kipi ni bora zaidi kwa huyo mtoto wako.
Ndizi
Ndizi zina wanga (carbohydrates)
mwingi,amabayo hutia nguvu,vile vile fiber kwa kusuport kulainisha mmeng’enyo
chakula tumboni.Ni kizuri na chepesi kuwa chakula cha mtoto,na huwa rahisi
kuiva kwake.Pindi unapoandaa ndizi kwa mtoto mdogo,hakikisha imeiva vizuri na
imepondeka vizuri.Kwa mtoto mkubwa anaweza kula ndizi kama ilivo yaani
nzima,lakini iwe pia imeiva vizuri iwe rahisi kwa mtoto kuisaga na kuimeza kwa
urahisi zaidi.
Viazi
vitamu
Viazi vitamu ni kizuri chenye chanzo
ya potassium, vitamin C, na
fiber na wingi wa beta-carotene, ni antioxidant ambayo husaidia kulinda aina za
magonjwa cancer na kusafisha free radicals.Watoto wengi hupenda viazi vitamu
zaidi kuliko mboga mboga kwasababu ya ladha yake ya utamu wa asili.Pindi
unapopika hivi viazi viponde au kusaga,viazi vitamu ina ulaini ambao ni rahisi
kwa mtoto kuvila,hata kwa watoto ambao ndo wanaanzishiwa kula solids au vyakula
vigumu.
Parachichi(avocado)
Parachichi(avocado)
Parachichi wakati mwingine huwa kama
mboga,lakini hilo ni tunda!Ina lishe
nyingi kuliko aina ya vyakula vingine vifananavyo na parachichi.Parachichi lina
protini nyingi katika mafungu ya matunda na ni tajiri wa mafuta (fat)-“ni
nzuri” aina hii ya mafuta inavilinda vidudu au diseases vya ugonjwa wa
moyo.Hakikisha unampa mtoto parachichi liloiva vizuri .Osha nje ya hilo
tunda,kisha menya maganda na lisage liwe laini.Sababu lina mafuta mengi kwahiyo
mara moja mtoto kushiba,mpe kidogo na chakula kingine,huweza kuwa kuku au nyama
laini.
mayai
Mayai ni mazuri.Yai leupe
huwa ni protein tu na kiini kina zinc na vitamins A, D, E, na B12.
Kiini pia kina choline, research inaonyesha ni nzuri kwa
afya ya maendeleo ya kukuza akili.Kimila,madaktari wa watoto huwa
wanashauri walezi wasiwape watoto
mayai—na sana sana ile nyeupe—mpaka baada ya mwaka kwa sababu ya matokeo ya alergy.Lakini huo ushauri kwa sasa umebadilika,na baadhi ya wataalam wanaamini kwamba mayai yacheleweshwe kwa familia ambazo zina
historia ya matatizo ya allergy.Wakati mayai ni chanzo kikuu cha protein na
lishe nyingi nyingine,shauriana na mtaalam wako pindi mtoto wako ameanza kula
vyakula kuangalia kama ni SAWA au kipindi gani itafaa kumpa mayai mtoto wako.
Kwa upande wangu nashauri mayai mazuri ni ya kienyeji na sio ya kuku wa kisasa au kizungu kwa sababu ya dawa na muda wa utotolewaji
wake pia ni mdogo.
karoti
karoti ina wingi wa beta-carotene, na
antioxidant ambayo hutoa ile rangi ya
orange.Beta-carotene hubadilishwa kuwa vitamin A mwilini
na huchukua nafasi ya kukuza ukuaji na afya ya kuona.Kupika karoti huleta ladha
ya asili yake ya utamu,ambayo hupendwa na watoto sana,ambao wamezaliwa
wanapenda ladha ya vitu
vitamu.Unapoandaa karoti kwa mtoto mdogo,hakikisha zinaiva sana hadi kuwa
laini.Kama mtoto mkubwa na anweza kula ikiwa nzima ilioiva haijalainika huwa
nzuri zaidi,unaweza kumlisha ilopikwa kidogo tu.
Maziwa ya mtindi
Maziwa ya
mtindi humpatia mtoto calcium, protein, na
phosphorus,ambazo ni muhimu kwa kukamavu au kutia nguvu,mifupa yenye afya na
meno. Maziwa ya mtindi yana probiotics,ni aina ya bacteria mzuri ambae anasidia
katika mfumo wa usagaji chakula na kusupoti immune system. Watoto wanahitaji sana mafuta
katika mlo wao,kwahiyo chagua maziwa mazuri ya mtindi ambayo yana mfuta
kidogo,au yana aina ya mafuta tofauti tofauti .Pia epuka maziwa ya mtindi ya
ladha au flavored,ambayo huwa yana sukari nyingi.Kama unahisi kuongezea
ladha,changanya na matunda yalosagwa.Mtoto chini ya umri wa mwaka huweza kuwa
na matokeo mabaya ya protein inayopatikana kwenye maziwa ya mtindi,usisite
kushauriana na daktari wa mtoto wako kabla hujampatia maziwa hayo .
Baby
cereal
Iron-fortified infant cereals humpa mtoto wako madini ya chuma yanayotakiwa
katika ukuaji wake. Watoto huzaliwa na madini ya chuma,lakini huanza kupungua
au kuisha kuanzia miezi5-6.Maziwa ya mama hayana hayo madini ya kutosha,ni
muhimu kutengeneza vyakula vyenye hayo madini chuma.Kama mtoto wako ameanza kula
vyakula,wataalam wengi wanashauri iron-fortified rice cereal ni chakula cha
mwanzo kwa sababu ni aghalabu kuleta au sababisha allergy kama nafaka
nyingine.Pindi mtoto anaendelea kukua,unaweza kuchanganya infant cereal na
matunda.Ni vizuri ikawa laini au nyepesi na matunda kama pear, peach,na plum.
Cheese
Cheese ni nzuri yenye protein –ni muhimu kwa ukuaji-- na calcium kwa
kujenga mifupa imara na meno. Cheese ina dose ya afya ya riboflavin (vitamin
B2),ambayo husaidia kubadili protein, fat, na carbohydrates katika mfumo wa
nguvu au energy. Swiss cheese kwa kawaida ni tamu na laini kwa watoto.Japo cheese huweza kuwa choking hazard,au kukatwa vipande pande. Ni
nzuri kwa watoto wanaokula vitu vizima kama kidole na hutumika kwa vitu vingine
pia .
kuku
kuku ana protein na ni chanzo cha vitamin B6,amabayo hutumika kusaidia kutia nguvu mwilini tokea kwenye vyakula.Ni muhimu kwa watoto kuanza kula mara kwa mara chakula chenye protein hata kwa uchache wake kusaidia ukuaji wa mtoto.Kama mtoto wako hapendi ladha ya kuku ile yenyewe,mchanganyie na matunda anayopenda au mboga anayoipenda.Citrus fruits
Citrus fruits, ikiwemo chungwa, ndimu, na zabibu,ni nzuri na chanzo cha vitamin
C,ambayo husaidia kutengeneza collagen inayopatikana
kwenye mishipa ,mifupa,na tissues nyingine mwilini. Vitamin C pia huponesha
palipoumia na kusaidia kuyeyuka kwa madini chuma kutokea kwenye vyakula
vingine. Citrus fruits pia ina potassium, madini amabyo yanasiadia misuli
kujikunja na kufanya kazi vizuri na kumaintain afya ya fluid balance mwilini.kuwa makini acid
isizidi kwa mtoto,ni vizuri zaidi kutompa mtoto citrus fruits mpaka baada ya
kutimiza au baada ya mwaka.
Nyama
nyekundu(red meat)
Nyama nyekundu huleta kwa urahisi ya
kuyeyusha aina ya madini chuma kwa mtoto wako.Madini chuma husaidia seli za
damu nyekundu kubeba Oxygen kwenda kwenye seli kupitia mwilini na ni muhimu kwa
kukuza akili au ubongo.Kwa bahati mbaya,upungufu wa madini chuma –ambayo huweza
sababisha madhara katika usomaji na tabia pia-ni moja wapo ya upungufu wa lishe
kawaida kwa watoto.Ndio maana ni muhimu kuhakikisha mtoto wako anayapata haya
madini chuma,kutokea kwenye nyama nyekundu,na vyanzo vingine katika mlo wake.Kwa
watoto wadogo,weka nyama yenyewe haswa,kama beef na karoti.Watoto wakubwa ambao
wanaweza kutafuna ipike vizuri kisha watumie hivyo.
Butternut Squash
Butternut squash ni nzuri kwa watoto sababu wanapenda ladha ya utamu.Ni chanzo kizuri cha antioxidant beta-carotene na pia ina vitamin C, potassium, fiber, folate, B-vitamins,na ina omega-3 fatty acids.Ni rahisi kutayarisha nyumbani kama utanunua ilo prepeeled, precut squash inayopatikana wanapotengeneza.Chemsha ichemke vizuri,kisha ikoroge mpaka ilainike.Tengeneza na uwaandalie kwa familia ni nzuri sana na ina ladha nzuri pia.Samaki
Samaki weupe,kama vile haddock na cod,ni wazuri sana kwa protein,ambayo watoto wanaihitajia kwa maendeleo ya kukua. Samaki wa mafuta , kama salmon, huleta fat-soluble vitamins na mafuta yenyewe fats, kama DHA,ambayo inakuza akili na macho na kukuza mfumo wa immune. Samaki huweza sababisha allergy,kwahiyo ongea na mtaalam wa watoto kabla hujampatia mwanao.Kama iko POA,basi utamsababishia mtoto afya nzuri.Wataalam wanashauri ni vizuri kumlisha mtoto samaki mara mbili katika mlo wake kwa wiki yenye mercury kidogo,kwakuwa ina faida nyingi za kiafya kwa mtoto.
Nyanya
Nyanya ina lycopene nyingi, pigment nyekundu katika nyanya ina fanya kazi kama antioxidant kusaidia kulinda na cansa na vijidudu vya moyo. Lycopene huweza kuyeyeuka ikafanya kazi vizuri mwilini kama nyanya itakua imepikwa vizuri na mafuta.Kwahiyo tengeneza sauce ya tomato na tambi kwa kupika nyanya na mafuta ya olive oil.Saga iwe laini kwa watoto wanaoanza kula.Sauce ya kutengeneza nyumbani ina sukari,na chumvi kidogo kuliko ya kununua,na ni nzuri kwa familia yote.Hivi huna tomato fresh?basi hata za kwenye makopo ni nzuri pia.
Nyanya ina lycopene nyingi, pigment nyekundu katika nyanya ina fanya kazi kama antioxidant kusaidia kulinda na cansa na vijidudu vya moyo. Lycopene huweza kuyeyeuka ikafanya kazi vizuri mwilini kama nyanya itakua imepikwa vizuri na mafuta.Kwahiyo tengeneza sauce ya tomato na tambi kwa kupika nyanya na mafuta ya olive oil.Saga iwe laini kwa watoto wanaoanza kula.Sauce ya kutengeneza nyumbani ina sukari,na chumvi kidogo kuliko ya kununua,na ni nzuri kwa familia yote.Hivi huna tomato fresh?basi hata za kwenye makopo ni nzuri pia.
Peas
Peas huwa ina burst pamoja na vitamin K,lishe ambazo zinafanya kazi pamoja nazo ni calcium husaidia kujenga mifupa. Peas ni chanzo cha antioxidant vitamins A na C, na pia folic acid B vitamins. Na kumuwekea peas mtoto kwenye sahani yake ita boost fiber katika mlo wake,na ni muhimu sababu wataalam wameona watoto wote na hata na watoto wakubwa pia,hawapati fiber ya kutosha.Kusaga chakula cha watoto basi peas ni rahisi sana .
Broccoli
Broccoli ni kwakweli ni chakula kizuri ,ni chanzo kikuu cha vitamin
C na pia ina beta-carotene, folic acid, madini chuma, potassium, na fiber.Kuchemsha
broccoli katika maji hupunguza karibu nusu yake ya vitamin C ilokuwemo,kwahiyo
ni vizuri kuisteam au kuweka kwenye microwave. Kama mwanao nimpenzi wa ladha ya
broccoli,mchanganyie na kitu kitamu au mboga anayoipenda ,kama viazi vitamu au butternut
squash.