• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, December 12, 2013

NJIA 5 ZA KULAINISHA LIPS

6:04 AM // by Kalma // No comments

LIPS LAINI

Huwa napenda hali ya baridi baridi,hiki ni kipindi ambacho ngozi huanza kuwa kavu na kachu-sana sana midomo(lips). Nina ngozi iko sensitive sana ,sijui mwenzangu we ngozi yako je? Hali ya hewa huleta ukavu, allergies, hakuna anaependa ngozi yake kuwa haina mvuto mzuri hata kupata maumivu pia. 
Hizi njia tano(5)nyepesi kukuweka mdomo wako kuonekana fresh na mlaini .
 1) Tango

Kata tango vipande vipande na shikilia katika lips zako kwa 20 dakika.Maji yote katika tango yatalainisha lips zako na yatang’aza na kuponesha sehemu zilokatika.
 2) Sukari ya brown & maji

Changanya  maji kidogo katika sukari ya brown kidogo,unaweza tengeneza scrub ikawa nzuri kwa  exfoliating.Pakaa mchanganyiko huo kwenye lips zako mpaka utapohisi kulainika .
Fanya hivyo mara kwa mara kwa wiki! Hii scrub inasaidia kuondoa ngozi mfu na ngozi kavu pia..
3) chumvi & maji

Changanya vijiko 2 vya kula vya chumvi katika glasi ya maji ya uvuguvugu na subiri mpaka iyeyuke.
Chovya nguo katika maji ya chumvi hayo na shikizia katika lips zako kwa 20dakika,hii husaidia kuponesha kuungua kwa lips na kukauka kwake.
Itauma kidogo ila ndo dawa yenyewe na maumivu ni  kwa muda mfupi tu!

4) mafuta ya nazi

Kwa kufanya lips ziwe laini ,chemsha mafuta ya nazi katika microwave au hata kwenye jiko,nafasi yako! Pakaa mafuta ya moto hayo kwenye lips zako tumia kidole au cotton swab.
Unaweza pakaa hii kwa siku nzima pindi inapokauka unapakaa tena kuhakikisha mdomo wako haukauki.Hii pia huweza tumika kama lipgloss huwa mafuta yanafanya mdomo ung'are na kuonekana mng’ao mzuri.
5) Asali & Olive Oil

Kwa tiba ya usiku kucha ,changanya olive oil na asali pamoja.Asali ina antioxidants na ni antibacterial na husaidia kuponesha vidonda haraka,na olive oil itasaidia kulainisha pia.
Pakaa katika midomo yako kabla hujaendsa kulala,na lips zako zitakua laini mpaka asubuhi!

0 comments:

Post a Comment