Hii iko serious hivi muda huu 10:30 usiku oven lako
limerowekwa na baking soda,racks za oven zimelowekwa kwa bathtub,birika la chai
(buli) linatokota maji moto kwa kusafishia juu ya oven,na mumeo kapiga magoti
hahaha…nimecheka apo!anasafisha sakafu kwa sponji kwa sababu unagundua muda
umeenda na huna dekio au tambara la usafi (mop).(kiukweli ningemwambia aache!)
Tunaita usafi wa
kina(deep cleaning),
Sakamia ikianza hii,hairudi nyuma.
Tukifanya usafi tunapendelea njia za kisasa zaidi kuboresha
kazi yetu.Sakamia hatu
tumii madawa makali sana,tumejifunza ni Baking soda kwa kusafishia
oven.
Koroga uji wa baking soda na maji pakaa kwenye oven
yako.Iache kwa usiku mzima.Unasafisha uji ulioganda kwa kupangusa na maji.Halafu,pulizia
vinegar kumalizia uchafu wa baking soda. Futa vizuri.
Muhimu:
Ufunguo muhimu wa kuitumia baking soda,pindi
unaposafisha oven,unapaswa kuipa muda ili ifanye kazi.Kusubiri kwa saa 12 au
usiku mzima ndio tiketi yake.
Asubuhi yake unasugua ndani tumia sponji,halafu futa kwa
kitambaa safi laini.Muda huo unapulizia vinegar kwa kitambaa unachopangusia
mpaka uchafu wa baking soda uishe wote.Utaona rangi ya kijivu na brown yote
imeondoka ,na sehemu zote zikibaki safi na mng’ao wa kuvutia.
Mlango wa oven
Baada ya kuloweka na baking soda,nakusugua kutoa uchafu,hapa
unaangalia kama oven yako inatoka kioo utatoa utasafisha hakikisha pameng’aa.
Zinafurahia kulowekwa kwa beseni la kuogea(bath tub)!sio
lazima beseni najua utaniuliza la kwangu lipo chumbani inakuaje?unaloweka kwa
sabuni ya kuoshea vyombo.
Muhimu:
kama umeamua kusafishia kwenye beseni hakikisha unaweka kitambaa wakati unaziloweka la sivyo zitachubua bathtub.
kama umeamua kusafishia kwenye beseni hakikisha unaweka kitambaa wakati unaziloweka la sivyo zitachubua bathtub.
Tumia maji ya uvuguvugu kuloweka zile chuma za kupikia
kukata mafuta.Tia sabuni kali acha kwa 15-20 dakika,kabla ya kusugua.
Unaweza tumia dishwasher(mashine ya kuoshea vyombo)lakini
bado haitakatishi sana.Niambie mdau wangu we ni njia gani hutumia zikang’aa?Utendelea
kusugua na kufuta kwa kitambaa kisafi laini.
Mwishowe,ni sakafu yaani floor :
Una ratiba gani ya usafi wa kina kwako?
Sakamia Cleaners
Be hygienic and smart!!
0 comments:
Post a Comment