MAPAZIA
Pazia chumbani kwako huongeza mvuto kwa apartment.Unaweza
kushangazwa labda ni upotevu wa muda na hela kuweka pazia chumbani kwako,usiache
kuangalia faida zinazopatikana,usikose nafasi adhiim ya kuwa na pazia chumbani
kwako kwa mvuto na muonekano wa kupendeza.
Hizi ni faida za pazia chumbani:
1. LINEN HUDHIBITI JOTO
Pazia aina ya linen hufaa kwa chumba chochote nyumbani
kwako,lakini zaidi ni chumbani cha kulala(bedroom).Pazai ya Linen ni laini
yaani soft,yenye muonekano wa kifahari.Ni nzito na hufanya kazi ngumu kuliko
muonekano wake.Huleta baridi kipindi cha joto na joto kipindi cha baridi.Kama
ni mpenzi wa aina nyingine basi Linen liwe chaguo lako.Haina madhara ya aina
yoyote.
2. FARAGHA
Kama una majirani wenye tabia ya kuchungulia ndani ya nyumba
yako ,pazia huzia hilo.Hakikisha pazia za chumbani kwako sio nyepesi
hazionyeshi.Kununua pazia kubwa zaidi ya
dirisha lako,kuepusha kuonekana kupitia pembe za dirisha.
3. VUMBI
Huzuia vumbi kuingia chumbani .Pazia huchukua vumbi kutokea
sehemu karibu na eneo lenye vumbi .Hii itazuia vumbi kupenya na kusambaa
ndani.Kumbuka kufua na kukung’uta pazia mara kwa mara,zina tabia ya kushika
vumbi sana.
4.KUDHIBITI MWANGA
Kuwa na pazia chumbani hudhibiti mwanga.Kwa mchana ukiacha
wazi pazia itaingiza mwanga halisi wa jua,haina haja ya kutumia taa.Kama
huitaji mwanga,utazifunga.Hii ina tija pindi utumiapo compyuta au ukiangalia
sinema.
Kama huoni vizuri screen kwasababu jua linaangazia sana usoni,fungua
pazia vizuri zitaleta giza.Kwa upande mwingine,chagua pazia zenye rangi tulivu
huleta mwangaza usiku,hata kwa taa yenye mwanga hafifu.Njia nyingine,pazia
husaidia kupunguza matumizi ya umeme.
5.DESTURI YA PAZIA
Pazia ina desturi nyingi.Hupatikana kwa muonekano wa rangi
na mapambo tofauti mbalimbali.Kama una
mandhari fulani ya chumba chako ,unachagua kulingana na hilo.Kwa mfano,unanunua
pazia zenye kuendana na rangi ya chumba chako.
Kuwa na pazia chumbani ni faida kubwa kimazingira na
muonekano wa uzuri.Pazia hua hazilingani kwa kila mmoja ni tofauti kutokana na
mapendekezo ya kila mtu.Kuna aina nyingi tofauti za pazia la msingi ni chaguo
la moyo wako.
Unapenda pazia za chumbani kwako?tuambie ni za aina
gani,rangi je?
Share and Enjoy !
0 comments:
Post a Comment