• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Saturday, April 15, 2017

Usafi asilia wa chooni

2:23 AM // by Kalma // No comments

Usafi asilia wa chooni
 Dondoo

Kingine zaidi ya jiko ni ,usafi wa chooni huchukua muda mwingi na kazi sio ndogo sababu ina sehemu nyingi tofauti tofauti,ni asili yake,ni sehemu inayotaka sana usafi sababu kunatumika mara kwa mara.
Kama uko kama mimi ,lazma na utapenda kazi ya kusafisha choo.Kwa bahati nzuri mpangilio na madawa asilia yatakurahisishia kufanya haraka na vizuri chooni mwako.
 kioo
 Ni kama dirisha,unaweza kusafisha kwa mchanganyiko wa maji na vinegar katika chupa yako ya kupuliza kwa kutumia kitambaa au karatasi. Njia rahisi tumia microfiber cloth,kilowane na kingine kikavu.Au kimoja kilowane na kingine kikavu bila ya kutumia dawa aina yoyote,kwa kila usafishapo.
Counters, marumaru(tile), mabomba ya kuogea (shower),beseni la kuogea(tub)


Kama unavo hivo apo ,unaweza tumia kitambaa hicho kwa vyote.Pia ni nzuri kama utatumia kwa vibebea sabuni.
Nusu kwa nusu vinegar na maji itasafisha maru maru,counters,uso wa makabati,na vibebea sabuni
Mchanganyiko wa baking soda na maji utasafisha uchafu uloganda kwa shower na beseni la kuogea.(tumia vinegar bila maji kwa kutu na uchafu maradufu)
Kwa grout mwaga baking soda na nyunyizia hydrogen peroxide tumia mswaki kusugulia.

 Kwa kutu au uchafu mkubwa zaidi kwa tiles na tub,hizi dawa asilia husafisha vizuri sana lakini haishauriwi kutumia mara kwa mara
 Kwa maru maru za ukutani,milango ilopakaliwa rangi,madoa milangoni,nje ya choo,n.k,hizi dawa za asili husafisha vizuri zaidi.
 vyooMara moja kwa wiki,mwagia baking soda ndani ya choo igande,kisha tia kikombe kimoja cha white vinegar ndani ya maji humo kwa choo.Tumia brush nzuri ya kusugulia choo utaona madoa,kutu na harufu imekwisha kabisa.
Hii pia inatumika chini hata nje ya choo kuondoa harufu mbaya chooni. Nimegundua harufu ya mikojo ni mbaya sana(haswa kwa watoto wanaojifunza kutumia poti) na inajificha katika mikato ya choo cha kukaa hata kile cha aina nyingine ,juu ya mfuniko wa kufunikia choo na pembe za mikato.Nyumbani kwangu usafi huu hufanya kila baada ya wiki mbili .
 Namalizia kuosha choo kwa kupulizia manukato na kufuta chini kwa hydrogen peroxide.
 Manukato( Air Freshening)
 Kuna aina nyingi ya manukato sio nzuri kwa afya na haswaa kwa watoto huweza kuleta madhara,mfano kama Febreeze and Lysol spray zina dawa kali.Kunukiza chooni bila ya sumu hemu jaribu hizi za asili.
 Hizi mbili ziko njiani zitafanya nyumba yako na choo chako kunukia kiasili zaidi,hupunguza gharama za dawa na hulinda afya ya familia yako siku zote.

 Tuambie jinsi gani unasafisha choo chako? tupia maoni yako sasa!

0 comments:

Post a Comment