Kupanga dressing table
Dressing table inavurugika sana kwa sababu ni mahala
pakuhifadhia vitu vidogo dogo vingi,kama vipodozi,dawa,vipambio,urembo wa
dhahabu,silver n.k.Hata hivyo,dressing table bado inatakiwa iwe safi mara zote
na imepangika vizuri ili iwe rahisi kupata vitu pindi utumiapo
Tips:
Toa au tupa vipodozi vyote visivyotumika.
Hii husababisha dressing table kuwa imejaa na
vurugu.Unafikiri kuwa manukato au perfumes,lotions,na vichupa mbali mbali
huonekana vizuri .Achilia mbali mawazo hayo,usifikiri hivyo.Unatakiwa utupe
vyote visivyotumika kuleta muonekano mzuri na wa kuvutia kwa dressing table
yako.Na vile vile utapata nafasi ya kutosha kwa ajili ya vingine muhimu na
vipya.
Panga kulingana na aina
Jingine,panga vitu kwa makundi kwenye dressing table.Tofautisha
mapambo,dawa,mkoba wa huduma ya kwanza,na urembo.Weka powder ya
usoni,foundation, lipstick, mascara, eyebrow pencil,na vipambio vingine kundi
lake kwasababu hutumika wakati.Kwa hiyo,unatakiwa uwe na mkebe wa kubebea
vipodozi kuhifadhi humo.Hata dhahabu,silver na mapambo ya vito na mengineyo
yakae kwenye mkebe wake.Hapo utaweka lotion, night cream, sunblock,na vingine
vinavyofanana na hivi.Kingine,utazipanga perfume kwa usafi mzuri.Kama una aina
ya manukato tofauti tofauti kwa mfano ya usiku na mchana nayo utayawekea kwa
makundi yake halikadhalika udi n.k.
Kumbukumbu za upangaji
Kitu gani unatumia sana kwa dressing table yako?Utasema ni
vya kujipambia,mashanuo na vitana,lotions, perfumes,na jeweleries. Hta dawa
hutumika pale unaposikia maumivu.Hifadhi kwenye droo vile visivyotumika mara
kwa mara na weka sehemu ya karibu vile vinavyotumika kila mara ili kuvipata kwa
urahisi.
Pendelea kupanga dressing table mara tu inapovurugika .
Tutumie dressing table yako tushare pamoja!
0 comments:
Post a Comment