• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, April 13, 2017

Kusafisha dirisha la aluminium

6:30 AM // by Kalma // 1 comment

Kusafisha dirisha la aluminium
Kama nyumba yako ina vioo vya aluminium hua ni sababu ya kubeba vumbi na hewa chafu kama havisafishwi ipasavyo.Kwa bahati nzuri,kwa vifaa vichache,vinaweza takata na kunga’aa kwa muda mfupi.
Futa vumbi kwenye fremu ya madirisha
Kabla kusafisha fremu za dirisha,unachotakiwa kufuta vumbi eneo zote kwenye reli za dirisha ,nyavu na vioo vya dirisha zenyewe.Tumia kitambaa cha vumbi,au fagio dogo la manyoa la kuondoa vumbi.Tumia kifa kinachoendana na aina ya dirisha lako,fagia au futa vizuri hadi vumbi lote liishe.
Changanya dawa ya kusafishia  
Ushafuta vumbi na zimeisha,sasa changanya dawa na maji ndani ya chupa ya kupulizia,1/4 ya kikombe ya window cleaner au sabuni ya kusafishia ya maji na kikombe cha maji ya uvuguvugu.Changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutikisa chupa hadi ichanganyike vizuri .Mwishowe,chukua chupa tia maji ya vuguvugu.Huu mchanganyiko utatumika kusuuzia mwishoni ule mchanganyiko wa sabuni.

Tumia mchanganyiko wa sabuni
Ule mchanganyiko wa sabuni na maji ,pulizia kwa madirisha yako machafu iache kwa 1-3 dakika.Kisha,tumia kitambaa cha vumbi kufutia uchafu.Hakikisha dirisha limetakata,suuza na maji ya uvuguvugu na ufute na kitambaa safi kikavu kwa kukaushia.
Tip
Tumia gazeti au karatasi safi kwa mng’ao wa kioo cha dirisha.

1 comment: