Ukiitamka Mbilimbi au mbirimbi zote sawa, ila sana tumezoa mbirimbi.
Umetokana na mti mbirimbi na unazaa matunda mbirimbi, asili yake ni Bara la Asia, na hapa kwetu Tanzania maarufu sana visiwani Zanzibar,huko Unguja na Pemba.
Na wahindi wanaupenda sana!! hata bara mikoani upo sana tuu.
Mmea wake kama mwaridi ,mche wake una majani mawili.
Ni tunda dogo lenye rangi ya kijani iso kooza, na ikiiva huwa rangi njano,ina vimbegu ndani na moyo pia km unopatikana kwenye ndizi mbivu hizi, ina maji mengi ndani yake.
Hutumika kama kiungo cha mchuzi ili kuleta ladha ya uchachu badala ya ndimu au limao.
Sie wanapenda sana kututania jamani! Ni kweli tunasema hivi, “Eti bora ukatwe mkarafuu kuliko mbirimbi" kwa jinsi unavopendwa kule Pemba.
Hutumika kwa achari, "appetizer" japo ina matumizi ya kutosha ikiwezekana kila mtu awe nao mti huu.
Kutengenezea salad na hata jam kwa ajli ya mkate.
Kuni zake nzuri kwa kupikia, zina waka haraka na haziishi mara.
Ina vitamin A na madini ya potasiam hutumika kutengenezea rangi.
Ni dawa Haluli ambayo ina oxalic acid ndani yake.
Ni dawa ya ngozi iloathirika kwa kujipakaa maji yake.
Inatuliza homa kali pia.
Huondoa madoa kama ya kutu ktk nguo za aina linen.
Waphilipino wao hutumia kwa kutibu kuvimba kwa mwili, homa ya mifupa .
Ina control na kupunguza tumbo,kitambi yaani Obesity.
Hatuna haja ya kuhangaika kutumia dawa za kichina , wakati mbirimbi ni kila kitu .
ACHARI YA MBIRIMBI
Kuna ya mbirimbi nzima na ya kusaga.
MBIRIMBI NZIMA
Osha mbirimbi zako kiasi, pasua kati ziwe pande mbili toa moyo wake,pilipili,vitungu maji, karoti,tangawizi, vitunguu saumu .
Sufuria lako tayari tia mafuta yakichemka kaanga vitunguu maji vikiiva tia thoum,na tangawizi ilotwangwa, vikiiva tia mbirimbi,pilipili na karoti subiri viize kwa dakika saba mpaka kumi.
Osha mbirimbi zisage kwenye mashine ya kusagia zisagike vizuri obvious utasaga na maji kiasi iwe sio nzito na sio nyepesi.
Sufuria yako tia mafuta ya kupikia kaanga vitunguu maji vikiiva tia tangawizi na vitunguu thoum vilotwangwa, vikiiva tia nyanya zako upike kama mchuzi na karoti na pilipili,mbirimbi iwe ndo kitoweo chako.
Aina hizi za mbirimbi hukaa kwa muda wa mwezi kama itakua inakaa kwenye friji.
Kama hamna friji ianike juani mara kwa mara.
Dalili yake ya kuharibika ni hutokea mapovu juu ya chombo ulohifadhia pia hutengeneza ukungu juu au kwenye mbirimbi zenyewe.