• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Saturday, September 28, 2013

NYANYA

5:35 AM // by Kalma // No comments

Nyanya, kwa kizungu tomato, kwa kule visiwani Zanzibar al-maarufu kama "tungule".Kinajulikana sana kama "Family food"!.

Hii nyanya ni chakula kimeanzia Mexico zamani na kuenea duniani kote. Kwa sasa Spanish ndo kiungo kikubwa jikoni  ambao wanaongoza duniani.   Kiungo cha vyakula tofauti tofauti, pia ni sauce,  ni kachumbari, na ni kinywaji.

Nyanya ina utata sana imeshindikana kujulikana haswaa ni "tunda" au "mboga".
Nyanya ni nzuri kwa afya na kukinga mwili. Ina kazi ya tunda na inafanya kazi ya mboga vilevile  kwa wakati mmoja.
Waspain wao ndo walikuwa wa kwanza kuisambaza hii nyanya kuipeleka Europe huko.

      Europe mnamo 1544 kutokea kwa mtaliano mmoja aligundua aina ya tunda nyanya na wakaitambulisha Italy na ikaanza kuliwa.
  Fikiria kama ni tunda na ni mboga lazma ina faida za kutosha mwilini;
 Inaongeza kinga ya cancer ya matiti, inalinda ngozi na miale ya jua,inafanya ngozi kuwa soft,ina vitamin c kwa sanaa.

Inashauriwa ihifadhiwe ikiwa haijaoshwa na kusikokuwa na mwanga wa jua. Ikiwekwa frijini hupoteza ladha yake halisia.
Tunda nyanya likiwa na mbegu zake ina kinga ya ugonjwa wa moyo, hulinda mifupa, ini, figo, na kuweka mfumo wa damu vizuri.
Wafaransa nyanya inaitwa "pomme d'amour" kwa maana ya "love apple", wakati Italy wao "promodoro" "golden apple" .

Unajua nyanya haiwezi kuwa kitindamlo (desert) japo ni tunda, kwasababu lina "asidi" na pia sio tamu kama matunda mengine. Kwa sasa China wanaongoza kulima na kutengeneza  nyanya dunia nzima, wakifuatiwa na U.S, Uturuki, India, halafu Italy .

Tanzania na mikoa yke inalima sana nyanya lakini kwa matumizi ya ndani ya nchini humu humu tu.Chagua nyanya yenye rangi nyekundu nzurii uwapo sokoni isiwe imehorojeka,kupondeka,yenye ufa na hata kupasuka. Iwapo utapendelea iloiva sana nayo ni nzuri kwa kupikia masalo na marosti basi utaihifadhi kwenye friza lako kwa siku moja au mbili kabla, ukiitoa iache kwa dakika 30,na huwa rahisi kumenya ganda lake.Mbegu za tunda hili sio nzuri kwa mgonjwa  wa vidonda vya tumbo yaani "ulcers" kwa sababu ya acid inopatikana kwake.Hushauriwa wakati wa kuipika nyanya isitumike sufuria ya aluminium sababu ya acid nyingi ambayo ikichanganyika na metali ndani ya sufuria matokeo yake huwa chakula kitaingia aluminium na ni madhara kwa mtumiaji wa chakula hicho.

Juisi ya nyanya ambayo haina vimbegu ni nzuri kwa mtoto aliyeanza kula na nzuri kuila na maganda yake kwa afya na kinga nzuri mwilini.

   Mbegu za nyanya hutumika  kuwa chanzo cha kupata zao la tunda na mboga nyanya.











0 comments:

Post a Comment