• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Friday, September 27, 2013

CHOYA (Carcade/Roselle)

3:39 AM // by Kalma // 1 comment

Kwa kule Egypt zawadi ya thamani ukipenda kumpelekea mtu au familia,sio nyngine ni "bag of carcade tea" kwa maana nyingine tulozoea Choya. Kule Egypt hii  Choya au Carcade tea ni moja ya kinywaji cha tamaduni yao inayothaminika sana.

 Sifa yake kubwa ya hii ,ni rangi yake nyekundu iko poa kiukweli.  Hili ni jani limetokea kwa mmea Haibisus na hutumika zaidi kama kinywaji.
Majani haya huongezwa kwenye matunda kuleta rangi nzuri na ladha nzuri pia. Ina ladha ya uchachu ambao una tia hamu ya kula, yaani mtamu uchachu wake.
     Ina harufu nzuri ya  kipekee ya Vitamini "C" .
Ni kinywaji kizuri chenye kufurahisha na hunoga kitiwapo sukari.
     Inashauriwa kukiroweka kwa dakika tano(5) kwenye maji ya moto na kwa matokeo mazuri iache kwa dakika kumi(10).
Kwa afya nzuri na kukipata fresh kukiandaa kikiwa baridi yaani kilopoa.
    Choya hii ina muonekano au quality tofauti huanzia majani kama maua hivi madogo hadi  makubwa zaidi nayo yana virutubisho Zaidi.
        Ukitumia hii choya mara kwa mara ina faida hizi;
Ina Vitamin nyingi na mchanganyiko wa madini mengine kwa kidogo dogo kama vile Calcium. Inasaidia kuongeza upungufu wa Vitamin mwilini, Huongeza damu pia kwa mgonjwa alopungukiwa damu, Inapunguza  kiasi cha cholesterol , inakufanya ujisikie mwenye nguvu zaidi, Hupunguza stress na majanga ya nafsi, Hujenga kinga mwilini.
  Hupendeza kuongezea kwenye juisi ya matunda mengine kwa ladha nzuri na chache.

      JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua choya yako chache tia kwenye maji moto acha kwa dakika kumi,kisha chuja maji yake yale kiasi cha glass moja.

Chukua pakiti ya juisi ulonunua ila inapendezea Maaza juisi au hata ya azam mango au ya pendekezo lako.
   Mimina kwenye jagi lako la juisi kisha tia glass ya choya uloichuja , koroga,unaeza tia sukari ukipenda.

Ni nzuri na huokoa muda na gharama pia.
Huwa nawaandalia wageni wangu huifurahia na kuisifu hata kwa wengine.
 


1 comment: