KUMUOGESHA MTOTO
Watu wengi huogopa kuogesha watoto wachanga,ila ni jambo
zuri kama utatoa uoga,ni kweli ina maajabu hivi ,na kama ndio mara yako ya
kwanza pia huwa ni ngumu kidogo.
Mazoea ya mila yetu huwa kuna msaidizi pindi mama
anapojifungua na ndo hufanya kazi hizi,
ila inaonekana kuanza kuwa ngumu sababu ya ubusy na pirika za maisha kupata mtu
wa kuja kukaa na wewe kwa muda.
Isieleweke vibaya,
tabia au mila ya baadhi ya
wanawake wengine kurudi nyumbani
kwao, siishauri sana kwa kipindi cha kujifungua,kwani hupoteza nafasi kubwa ya
mume kujua tabu anayopata mke pindi mtoto anapokua mchanga,ni kipindi kizuri
cha nyote kufeel hiyo hali na ikibidi mume kutekeleza majukumu mengine.
Na kama italazimika hivyo ni sawa ila kukaa kwako na mume
wako na mtoto mchanga ni nzuri zaidi,kwani huongeza mapenzi , kuhurumiana,na
kupunguza gharama za kuendesha sehemu mbili kwa muda mmoja..
Kumuogesha mtoto ni kujenga mapenzi baina yenu.Watoto wengi
huenjoy kuwekwa kwenyemajimoto,ila wengine huitaji muda kuzoea kwa ngozi yao
mpya.
Tumia maji moto,kilo bora zaidi kwako wewe na mtoto
mwenyewe.
Fanya haya pindi unapotaka kumuogesha mtoto mchanga :
- Safisha vitu vyake vya kuogea kama sinki,au beseni ,siku hizi kuna yale special kama bafu hivi,lolote lile au kile, la msingi ulisafishe kwanza.
- Tayarisha sabuni,maji moto ya uvguvugu,mafuta,lotion,taulo,nguo za
kuvaa kama vest,diaper,nguo yenyewe,socksi,kofia,gloves kwa maeneo ya
baridi,nepi,pini ya nepi,baby shoo au blanketi la kumfunikia,n.k.
- Osha mikono yako vizuri.
- Hakikisha chumba hakina baridi,funga madirisha na milango au shusha pazia hutegemeana na hali ya hewa ya sehemu husika.
- Tia maji ya uvuguvugu kwenye sehemu ya kumuogeshea kama sinki,beseni n.k, kipimo yafunike mabega ya mtoto ukimweka,13cm(5in).
- Weka maji ya kumsuuzia kwenye chombo kingine pembeni.
- Mvue nguo zote na umsafishe kama amepuu au kukojoa,umfunge kwenye taulo safi hadi sehemu ya kumuogeshea.
- Muweke ndani ya beseni ukiwa umemshikilia kichwani na mkono wa kushoto umeegemeza shingoni kwake,asiwe amekaa, awe amelala ila shingo na kichwa viko juu ,ukiwa umemshikilia kwa nyuma,yaani mgongoni.
- Mwagie maji yakinge kwa mkono wako wa kulia, ni mtoto mdogo yasiwe mengi ,anzia kichwani upande wa uso ukiwa kama unampangusa.
- Kisha mpakae sabuni kuanzia mabegani ,kushuka mikononi na mpaka miguuni.Inashauriwa kumuogesha mtoto mchanga bila sabuni kuepusha allergy,na sabuni iwe isio na harufu na sio ya urembo,tumia sabuni za watoto.
- Msuuze kwa maji safi yaso na sabuni yalo pembeni kwenye chombo mpaka sabuni ziishe ,nayo yawe ya uvuguvugu.
- Kisha msafishe uso yaani mpanguse macho,na kona za pua kama unamkandakanda hivi na maji kidogo.
- Mfute kwa taulo safi na kavu,mfunike kwa dakikia 10 kupunguza baridi,kumletea joto mwilini,tumia blanketi.
- Mpakae mafuta au lotion ukianzia maeneo ya mgongoni huku ukimkandakanda,na sehemu nyingine.
- Mvalishe nguo safi na mkunjie blanketi.
- Mkiss kwenye paji la uso wake.
- Watoto wengi huchukua muda mfupi wakioga ni kulala.
Naamini we mama pia
utakua tayari umeoga na umekula vizuri ,huo utakua muda wako mzuri wa
kumnyonyesha mtoto alale vizuri.
TIPS:
- Usimuache mtoto mwenyewe kwenye maji hata kwa chembe dakika.
- Pendelea kumkanda viungo mtoto baada ya kuoga.
- Huweza tumia moto kumkandia kusaidia kupunguza gesi tumboni(colic).weka moto kidogo kwenye chetezo weka mikono yako juu ya ule moto ,itakua yamoto mkande au mmasage mgongoni na mwili mzima kwa kumnyoosha viungo pia.
- Baada ya kutoka jua la asubuhi ni muda mzuri wa kumuogesha,huwa hakuna baridi sana.
- Pendelea kumfanyia zoezi kwa kumkanda,ukiwa umem-beba kupunguza gesi na kumuondolea uoga mtoto.
- Piga pasi nguo za mtoto kabla ya kuvaa husaidia kuua vijidudu.
- Nguo za mtoto zisichanganywe na nguo za wengine.
- Hakikisha nguo za mtoto hazilali kambani nje,anua tu pindi
zikaukapo.Husaidia kupunguza wadudu.